Serikali ianze kutoa leseni za daladala luxury mijini, nauli iwe elfu Mbili. Hakuna abiria kusimama

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,909
51,904
Ni wakati muafaka kwa serikali kuanza kutoa leseni za daladala luxury ambazo zitakuwa zipakia watu level seat bila wengine kusimama.

Miji yetu Ina middle class wengi kwa Sasa ambao kupanda usafiri wa daladala au mwendo Kasi ulivyo Sasa hivi ni kuwaonea .Ndio maana usafiri wa daladala haupendwi kutumiwa hata na watu Kama wahindi na waarabu na wageni wanaotembelea nchi yetu.

Tukubali Kama Kuna madaraja kwenye ndege na daladala ziwe na madaraja.First class ziwe hizo za level seat ,third class ziwe hizo basi za mwendo Kasi na hizo daladala za mbagala na gongo la mboto ambazo hujaza watu Kama mihogo na zikipakia watu huingia Hadi kupitia madishani.Napendekeza nauli iwe shilingi elfu Mbili.
 
Wazo lililochelewa kuletwa.
Mahitaji ni makubwa sana. Ukienda pale stesheni uone jinsi watu wanavyopigana vikumbo kugombania private car nauli ya she 1000/-.
Nenda mnazi mmoja, stendi kuu kkoo hapo mahitaji ni makubwa zaidi.

Ni muda muafaka sasa kurasimisha biashara hii, kwa kuwa na mawazo chanya badala ya kufikiria kuwakamata, kwani kukamata so suluhisho LA hatuondoa tatizo.

Plan A walipie tu kitambulisho cha ujasiliamali, idadi ikiwa ni kubwa serikali itatathimini iwapo wakate lesini au waendelee na kitambulisho cha mjasiliamali
 
Hata usalama wenyewe kwenye huo usafiri ni mdogo sana.
Juzi kati nilipanda mwendokasi, dah! Unaweza sema nimepewa msaada. Maana sio kwa nyomi ile. Full kukanyagana.

Hakika tunahitaji mipango madhubuti kuhakikisha usafiri kwa dar hauwi mateso
 
😁😁😁😁 Mnabanana kiasi kuwa mtu hata akiingiza mkono mfuko wa jeans kukuibia Huwezi hata shusha mikono umdake na hutajua mkono wa mwizi ukikotokea kwa mbanano Kunakuwa hadi na ugomvi wa mahali pa kushika kwenye nguzo za kushikia mikono.
 
Ni wakati muafaka kwa serikali kuanza kutoa leseni za daladala luxury ambazo zitakuwa zipakia watu level seat bila wengine kusimama.

Miji yetu Ina middle class wengi kwa Sasa ambao kupanda usafiri wa daladala au mwendo Kasi ulivyo Sasa hivi ni kuwaonea .Ndio maana usafiri wa daladala haupendwi kutumiwa hata na watu Kama wahindi na waarabu na wageni wanaotembelea nchi yetu.

Tukubali Kama Kuna madaraja kwenye ndege na daladala ziwe na madaraja.First class ziwe hizo za level seat ,third class ziwe hizo basi za mwendo Kasi na hizo daladala za mbagala na gongo la mboto ambazo hujaza watu Kama mihogo na zikipakia watu huingia Hadi kupitia madishani.Napendekeza nauli iwe shilingi elfu Mbili.
Nyie si mpo kwa ajili ya wanyonge? Sasa kwanini mnataka kuwatenga hao wanyonge?

Wazo lako wala halina maana hasa ukiangalia aina ya watu wanaogombania usafiri wa umma.. Kuna bajaj zinapaki kituoni lisaa lizima zikisubiri hao abiria matawi.. Yapo madaladala yanayotoka Tegeta hadi Morocco mara nyingi yanasotea abiria kisa tu yaneweka nauli sawa na yale yanayotoka Tegeta hadi kariakoo mbaya zaidi yameongeza tu sh. 100 kwa ziada ya yale yanayotoka Tegeta hadi Makumbusho. Sasa emb nenda kaangalie utofauti wao katika level ya kupata abiria. Fanya utafiti kwanza.
 
Mnatengeneza tatizo halafu mnapendekeza namna ya kuli-solve; akili zilezile! Wananchi wanapigana vikumbo kwenye vituo vya daladala na mwendokasi kwa sababu ya mfumo mbovu wa usafiri wa umma; wananchi wanajinyima sana ili kujinunulia viusafiri binafsi sio kwa sababu wanapenda au wana pesa sana no! Ni kwa sababu ya mfumo mbovu wa usafiri wa umma japo kwa makusudi mazima TRA inawaumiza sana kwa kodi za kijinga kana kwamba wanawakomoa.

Jibu ni rahisi tu, boresheni miundombinu boresheni public transport system; as simple as that. Kwa mfano sikuona logic ya kutengeneza njia moja barabara kwa mfano za Mbezi-Goba-Tangibovu na ile ya Mbezi-Kinyerezi-Airport; ndani ya muda mfupi tayari zimelemewa; zinatengeneza foleni ambazo hufanya wananchi wasubiri vituoni muda mrefu!. Akili ilikuwa kujenga angalau double roads onset! Pili ni hizi barabara za mwendokasi; hivi ilikuwa akili kuweka zebra kila baada ya mita 50 au 100 kweli? Matokeo yake ni foleni zisizoisha! Hakukuwa na njia nyingine bora zaidi? Au ndio akili ziliishia hapo?
 
Nyie si mpo kwa ajili ya wanyonge? Sasa kwanini mnataka kuwatenga hao wanyonge?

Wazo lako wala halina maana hasa ukiangalia aina ya watu wanaogombania usafiri wa umma.. Kuna bajaj zinapaki kituoni lisaa lizima zikisubiri hao abiria matawi.. Yapo madaladala yanayotoka Tegeta hadi Morocco mara nyingi yanasotea abiria kisa tu yaneweka nauli sawa na yale yanayotoka Tegeta hadi kariakoo mbaya zaidi yameongeza tu sh. 100 kwa ziada ya yale yanayotoka Tegeta hadi Makumbusho. Sasa emb nenda kaangalie utofauti wao katika level ya kupata abiria. Fanya utafiti kwanza.
Huduma huendana na Bei .Mnyonge ana Bei yake na huduma inayoendana na hela Yake.Middle class wengi SI wapenda daladala hizi za Sasa hivi.Wala Bajaj.Wanapenda magari luxury yasiyopoteza muda.Luxury bus hata akipata abiria watatu anaondoa gari sii sawa na hayo ya shilingi Mia tatu nauli au Mia nne nauli yanapoteza muda mwingi vituoni.Luxury hamna.Si kila mnyonge hula hoteli ya kitalii mama ntilie anamhusu.Unategemea meneja au ofisa wa serikali apande Bajaj?
 
Watembea kwa miguu naona haki zetu zinazidi kusahaulika tu, kwakua boda boda wameamua kuvamia njia zetu tulizowekewa rasmi kuzitumia na ukigoma kuwapisha unaishia kuambulia matusi.
 
Back
Top Bottom