Serikali iangalie usumbufu wa mamlaka ya afya na usalama kazini (OSHA)

Mamboleo

Member
Oct 15, 2008
69
38
Pamoja na Waziri wa Sera, Ajira, Kazi vijana na walemavu Mh.Jenista Mhagama kutoa maagizo kwa waajiri nchi kuhakikisha maeneno yao ya kazi yawe yamesajiliwa na OSHA, kumekuwa na usumbufu na urasimu mkubwa kutoka kwa watumishi wa idara hiyo ya serikali dhidi ya waajiri wanaotaka kutimiza lengo na agizo la kusajili maeneo yao ya kazi.

Ukiacha usajili wa eneo la kazi " Registration of Workplace" pia kuna ukaguzi wa maeneo ya kazi unaofanywa na wakaguzi wa OSHA kwa ajili ya kupata "Compliance Licence" endapo mwajiri atakidhi matakwa yote kwa mujibu wa taratibu na sheria.

Katika eneo hili la compliance licence ndipo urasimu unapokuwepo ili kumfanya mwajiri atoe rushwa kwa wakaguzi.Kwa mfano utakuta ripoti ya ukaguzi wa afya kwa wafanyakazi-medical examination.

Wakaguzi wengi huchelewesha ripoti na hivyo kufanya zoezi zima kuchukua hata zaidi ya mwezi.Pia taratibu za ndani za Mamlaka kupitia ripoti za ukaguzi kwa ajili ya kutoa compliance licence zinakuwa na ukiritimba na kuchukua muda mrefu kwa ajili ya kujenga mazingira ya utoaji rushwa.Inakuwaje maombi ya cmpliance license yachukue zaidi ya miezi 2 au 3?

Pamoja na utendaji mzuri wa mtendaji mkuu wa mamlaka hii ni wakati muafaka kwa serikali kukagua utendaji wa OSHA kwa sababu wafanyakazi wengi na hasa wa ofisi ya ukanda wa Dar es salaam na Pwani umejaaa ubabaishaji na ukiritimba.

Pia ni wakati muafaka kwa serikali kuangalia namna ya kufanya maombi na taratibu za kutoa compliance licence na certificate of registration kufanyika kwa njia ya mtandao ili kupunguza ukiritimba.Pia mamlaka hii inapaswa kuajiri wafanyakazi wao kwa sababu baadhi ya wafanyakazi wake sio waajiriwa wa kudumu na wao pia ni chanzo cha tatizo.

Ni muhimu serikali ichukue hatua madhubuti kuondoa vikwazo vya OSHA kwa wawekezaji wa nchi hii wanaokwazika kwa utendaji mbovu kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka hii.
 
Waajiri wengi hawa comply

Acheni OSHA wafanye kazi

Waajiri timizeni matakwa ya sharia,OSHA Act,2003
 
Waajiri wengi hawa comply

Acheni OSHA wafanye kazi

Waajiri timizeni matakwa ya sharia,OSHA Act,2003
Sasa huyu kaona hawacomply kwa sababu ya ukiritimba wa hiyo idara halafu ww unasema hawacomply. What did u say?
 
sio ukiritimba.......

Kila mwjiiri ni lazima afuate na kutekelza sheria kwa mujibu wa OSHA Act,No 5 ,2003.Ila haimaanishi kuwa utekelezaji wa sheria uwe kisingizio cha ukiritimba.Ni wakati wa OSHA kujitathmini na kuomna kama wateja wake wanatendewa haki..la sivyo serikali iikague OSHA kubainisha mianya ya utekelezaji hafifu na ukiritimba unaopelekea kuwa chanzo cha rushwa.
 
OSHA wako sahihi na wako vizuri sana,.....Yule mama yuko safiii....Waajiri wanatakiwa ku comply na sio kuleta porojo......
 
OSHA wako sahihi na wako vizuri sana,.....Yule mama yuko safiii....Waajiri wanatakiwa ku comply na sio kuleta porojo......
Porojo zinaletwa na wewe?Ku comply ni sharti la kila mwajiri.Sasa wata comply vipi kwa ukuritimba wa OSHA?Compliance License kupatikana baada ya miezi 3 au 4 hata kama mwajiri ametimiza masharti yote?Tetea hoja kwa hoja la sivyo na wewe utakuwa mmoja wa wanaofaidika na mfumo mbovu wa mamlaka hii!
 
Pana usumbufu sana OSHA... Unaweza kufuata utaratibu wote mapema lakini mpaka unakuja kuipata hiyo Compliance tayari isha expire...
 
Pana usumbufu sana OSHA... Unaweza kufuata utaratibu wote mapema lakini mpaka unakuja kuipata hiyo Compliance tayari isha expire...
Ni kweli smart911..ndicho wadau wengi wanalalamikia...endapo hawatajirekebisha..wadau watawasilisha malalamiko haya kwa wahusika wakuu akiwemo Mtendaji Mkuu wa OSHA ambaye anajitahidi sana kulisimamia shirika hili ila wasaidizi wake hawafanyi ipasavyo.
 
Back
Top Bottom