Serikali iangalie tatizo la ukosefu wa ajira kwa umakini

Halaiser

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
3,992
6,290
Wasalam wanajamvi. Kwa miaka kadhaa sasa kumekuwa na tatizo la ajira Kwa wahitimu wa vyuo mbali mbali. Wengi wa vijana hao wamekuwa wakijitolea kwenye Idara na Taasisi mbali mbali za Serikali Kwa mkataba wa miezi/ mwaka mmoja. Wamekuwa wakiahidiwa na watendaji wa maeneo hayo kuwa vibali vya ajira vikitolewa basi wao watepewa vipaumbele.

Mkataba wao ukiisha wanachukuliwa wengine kwa ahadi zile zile. Sina tatizo ktk Hilo. Tatizo liko pale ambapo vijana wale wanaojitolea kwa moyo wa kizalendo kutopatiwa hata nauli pamoja na chakula cha mchana wawapo kazini. Wakati mwingine hupatiwa kiasi cha shs laki moja Hadi laki moja na nusu baada ya miezi miwili na kuendelea.

Vijana hawa wamekuwa ni mizigo Kwa wazazi/walezi kwani wao ndio wanaowagharamia. Kwa maana nyingine wazazi/walezi wamekuwa wakijitolea nao kuisaidia Serikali. Jambo ambalo kwangu naona ni kero.
 
Back
Top Bottom