Optic nerve
Member
- Mar 18, 2019
- 19
- 20
Kipindi cha serikali ya awamu ya nne,serikali ilitilia mkazo wa kuandaa walimu wa sayansi,baada ya kuona walimu wa Physics,Chemistry, Biology na mathematics kuna upungufu mkubwa mashuleni.Moja ya mikakati ilikuwa kutoa mikopo kwa asilimia 100 kwa wanafunzi hao.Hoja yangu iko hivi,hawa walimu wakishapata ajira serikalin,licha ya kuwa na kazi nyingi mashulen ikiwa na vipindi vingi vya kufundisha,kufanya kazi ya utalaam ww maabara,gharama kubwa ya kusoma masomo ya sayansi na kutumia muda mwingi kusoma masomo ya sayansi.Licha ya matatizo kibao wanayoyapata wanalipwa mshahara mmoja kwa kiwango sawa cha elimu na wale walimu wa sanaa ambao hawana vipindi vingi vya kufundisha mashuleni.Ukiondoa hayo kwenye ulipaji wa mkopo wa elimu ya juu walimu hawa watalipa zaidi kuliko walimu wa sanaa,sasa unakuja kujiuliza mbona kipaumbele kwa walimu hawa hakipo kwenye ajira?Mfano kwenye shule zisizo na laboratory technician,walimu hawa wa sayansi wanafanya hizo kazi kwa mshahara uleule,ndio maana wengi wao wanakimbia ualimu.Serikali inatakiwa ilifanyie tathimin hili suala.