Serikali iangalie kwa umakini haya magroup ambayo yanaanzishwa na Madaktari kutibia watu na kutoza pesa

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
1,694
3,982
Nipo kwenye Group moja linaitwa Group la Afya likiwa limeanzishwa na Bwana Mmoja anaitwa Mwanyika. Kwa maelezo yake ni Daktari.

Anaweza kuwa na nia nzuri ya kusaidia watu kwa ushauri na wakati fulani kuwasaidia wasiingie gharama ya kwenda hospital kutokana na ushauri anaoutoa lakini wasiwasi wangu ni kuwa huko mbeleni kunawezekana kuwa na athari flani.

Mimi nipo kwenye group hilo muda mrefu sana nikiwa na namba 3 tofauti tofauti. Kuna wakati jamaa alishawahi hata kuniomba kwa ushauri alionipa nimpoze kidogo nikamtumia tsh 20,000.

Nliona ni sawa amenisadia kwa kweli lakini nmekuja shtuka kuwa sometimes kuna watu hatuendi hosp tunategemea Uaguzi kama huu. Yeye huwa anasema mwambie dalili zako then anasema una malaria, una typhoid au unaweza kuwa na covid 19.

Nashauri magroup kama haya yaandikishwe ili kuwepo mfumo mzuri wa kuhudumia watu distance medicating/treatment. Sisi kwenye group tunashukuru sababu sasa madaktari wanafanya kazi kwa kutumia mtandao ndo mambo ya kisasa.

Inapunguza gharama za kwenda hospitali na foleni pia.
 
Umekwenda kuomba ushauri umeupata umekusaidia then unataka group lifutwe?

Hakuna shida yoyote kwa daktari kuagua mtandaoni ikibidi wafungue milango ya maabara ili lifike mahali mtu aende hospital kutafuta kipimo then asepe kwa daktari wake mtandaoni aandikiwe dawa.

Mbona dawa zinauzwa madukani na watu wananunua bila hata ya kuandikiwa na daktari, tena wanazitangaza na kumalizia matangazo yao wakisema maumivu yakizidi muone daktari.

Huo utaratibu wa tibakwa mtandao utasaidia kupunguza foleni za hospitali na pia kupunguza garama za matibabu ya kawaida. Huku kutakuwa na kaulimbiu maumivu yakizidi nenda hospitali. Safi kabisa
 
Hujielewi, hukulazimishwa kujiunga hilo group na pesa uliyompa pia ulitoa kwa sababu ya msaada aliokupa, sasa badala ujisaidie mwenyewe kujitoa huko kama unaona group halikufai, unaitaka serikali ikusaidie, hicho kichwa chako tafuta mahali ukakiweke.
 
MaCCM mna roho mbaya sana, yote hii kujipendekeza ili na wewe uonekane umeleta mada ya Uzalendo ili ulipwe pale Lumumba.
 
Akina ndodi na mwaka wanaweza wakawa wamehamia pande hizi za e-dokta. Ila ninachokiona hapa hiyo buku 20 imekuuma kinoma zaidi ya kupigwa kibuti na demu...
 
MaCCM mna roho mbaya sana, yote hii kujipendekeza ili na wewe uonekane umeleta mada ya Uzalendo ili ulipwe pale Lumumba.
Sasa kwa nini nikilipwa wewe unaumia na wala haitoki mfukoni mwako? Why are yu so hurt brother/sister?
 
Akina ndodi na mwaka wanaweza wakawa wamehamia pande hizi za e-dokta. Ila ninachokiona hapa hiyo buku 20 imekuuma kinoma zaidi ya kupigwa kibuti na demu...
Sijui kama umesoma ukaelewa.ingawa nmetumia kiswahili chepesi sana.siyo kile cha kisomi.
 
Back
Top Bottom