Serikali Iandae Utaratibu Maalumu Juu Ya Magari Haya

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Wadau Naomba Nitoe Ushauri Ufuatao Kuhusu Matumizi Ya Baadhi Ya Magari.
Sio Lengo Langu Kuingilia Biashara Za Watu,Kuzungumzia Ubora Wa Aina Fulani Ya Chombo Cha Usafiri, Wala Kuwafundisha Mamlaka Husika Utekelezaji Wa Kazi Zao. Nimesukumwa Tu Na Hisia Zangu Za Huruma Kutokana Na Matukio Japo Sina Takwimu Sahihi Ya Ajali Zinahusisha Magari Sana Has a Yale Yanayoinika Na Wengi Kuwa Yana Speed Kali Na Ni Ya Kisasa Zaidi.
Nazi gumzia Magari Aina Ya Subaru,Alteeza,Mark X.
Karibuni Wadau Kwa Maoni
 
Hayana speed kali ila yanaendeshwa na watu wasiojitambua! Mark X haiwezi kufikia speed ya gari kama BMW 318/320I, VW Golf, Audi A4,X5 etc!

mtu anaona sifa kuchukua video kafikisha mshale wa speed mwisho kwenye toyota barabara ya kitanzania, hajafunga mkanda, unakuta katupiamo caste mbili, gari ata service unakuta ya kubangaiza, tairi kaweka linglong mchina... kila angle inagoma apo, lazma ajali itokee!
 
Hayana speed kali ila yanaendeshwa na watu wasiojitambua! Mark X haiwezi kufikia speed ya gari kama BMW 318/320I, VW Golf, Audi A4,X5 etc!

Kweli Mkuu...kuna watu wanapenda kumwaga moto...udereva mzuri ni ule wa kujihami..kwanza ukiwa dereva mzuri barabara yenyewe inakuonesha uendeshe vipi gari...yanini kuminyana? Ibaki tu mapenzi ya Mungu.
 
Hapa mjini Kuna mtu ana toyota supra speed 300km/h,Horse power 750 sijui mnataka huyo afanyaje sasa?
 
Kuna baadhi ya gari ni hatari na ni heshima hata kuzimiliki tu:

~Mercedes Benz
~Any V8 engine cars
~All Jeeps
~Gari za Kimarekani(Lincolin, Mustag, Maserati n.k)
~European Cars
~Germany Cars(VW, Audi, Benz, LandRover & RangeRover n.k)
~Subaru Zote

Nakuhakikishia Hutojuta.
 
Wadau Naomba Nitoe Ushauri Ufuatao Kuhusu Matumizi Ya Baadhi Ya Magari.
Sio Lengo Langu Kuingilia Biashara Za Watu,Kuzungumzia Ubora Wa Aina Fulani Ya Chombo Cha Usafiri, Wala Kuwafundisha Mamlaka Husika Utekelezaji Wa Kazi Zao. Nimesukumwa Tu Na Hisia Zangu Za Huruma Kutokana Na Matukio Japo Sina Takwimu Sahihi Ya Ajali Zinahusisha Magari Sana Has a Yale Yanayoinika Na Wengi Kuwa Yana Speed Kali Na Ni Ya Kisasa Zaidi.
Nazi gumzia Magari Aina Ya Subaru,Alteeza,Mark X.
Karibuni Wadau Kwa Maoni
Kwanini unakuwa muoga namna hiyo?
Kama unajua jambo kumfundisha mtu sio kosa, kumuelekeza pia ni kutimiza wajibu muhimu kwenye jamii unayoishi.
Ondoa hofu uliyotengenezewa kwa kutandikwa makofi mawili matatu na polisi huku wakikuuliza "unanifundisha kazi mimi! Eeh unanifundisha kaaazi. Pwaaaaaa!"

Ulichokiandika ni pure mafundisho.
 
Wadau Naomba Nitoe Ushauri Ufuatao Kuhusu Matumizi Ya Baadhi Ya Magari.
Sio Lengo Langu Kuingilia Biashara Za Watu,Kuzungumzia Ubora Wa Aina Fulani Ya Chombo Cha Usafiri, Wala Kuwafundisha Mamlaka Husika Utekelezaji Wa Kazi Zao. Nimesukumwa Tu Na Hisia Zangu Za Huruma Kutokana Na Matukio Japo Sina Takwimu Sahihi Ya Ajali Zinahusisha Magari Sana Has a Yale Yanayoinika Na Wengi Kuwa Yana Speed Kali Na Ni Ya Kisasa Zaidi.
Nazi gumzia Magari Aina Ya Subaru,Alteeza,Mark X.
Karibuni Wadau Kwa Maoni
Mkuu wangu shida haipo kwenye magari hao uliyoainisha. Tatizo lipo kwa madereva.Gari nyingi zina speed kali siku hizi, ajali husababishwa na madereva.
 
Hayana speed kali ila yanaendeshwa na watu wasiojitambua! Mark X haiwezi kufikia speed ya gari kama BMW 318/320I, VW Golf, Audi A4,X5 etc!
Mercedes INA 320/kmh. Hayo uliyotaja hayafikii. Sema Barbara zetu ki ukweli Max inatakiwa iwe 80/kmh. Au 50mph.
 
Mercedes INA 320/kmh. Hayo uliyotaja hayafikii. Sema Barbara zetu ki ukweli Max inatakiwa iwe 80/kmh. Au 50mph.
nilichokiaona hapa shida ipo kwa madereva na sio gari! akili ya dereva ndio mustakbali wa safari!
All in all Mercedes ipo stable barabarani zaidi ya Mark X.
 
Nadhani hoja sio gari hoja ni dereva.... Nimekuwa na na Kigari kinaitwa Alfa Romeo speed 300, issue ni wanaoziendesha hizo gari.... Kama huna mafunzo maalumu ya kukimbiza magari ww ni mtumiaji tu, Ukifika 80kph Tulia... Ukitaka kumaliza kisaani uagane na nyonga. Sikumbuki Mara ya mwisho nimevuka 70 na hiki kibaby woka changu.
 
Tatizo sio magari tatizo ni uendeshaji hayo magari uliyoyataja kwanza ni mazuri na very confortable shida ni uendeshaji mbona Paul Walker alikufa kwa ajali akiendesha gari yenye thamani zaidi ya bilioni moja ya kitanzania!? Sasa pale shida ni ile Porsche au uendeshaji wa Paul.

Ajali nyingi ni uzembe wa madereva kuwa spidi kali na kutokuwa makini barabarani kupita magari sehemu mbaya bila kuangalia...
 
Back
Top Bottom