Serikali iandae sherehe kubwa kuadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwa Mwalimu Nyerere

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,495
51,089
Hakuna chembe ya shaka, Mwalimu Nyerere alikuwa zawadi kubwa ambayo Mwenyezi Mungu alitupa sisi Watanzania na Afrika.

Tarehe 13 April mwaka 2022 Mwalimu atatimiza miaka 100 tangu kuzaliwa kwake. Bado mwaka mmoja na miezi michache

Hii ni fursa nzuri sana ya kumuenzi Mwalimu, na kuitangaza nchi yetu na kuikumbusha dunia na Afrika mchango wa Mwalimu katika ukombozi wa bara la Afrika.

Pia ni nafasi adhimu ya kutumia tukio hilo kuvutia watalii mwaka huo. Kama hili tukio tukilitumia vizuri, tukaalika watu, wasomi, wana umajimui wa Afrika (Pan Africanists), watu waliofanya kazi na mwalimu na wanaomjua kwa haika tunaweza kupata watu wengi sana watakaokuja nchini kwa ajili ya tukio hilo.

Kwa hiyo nashauri yafuatayo
1. Kuanzia sasa serikali iunde kamati ya kufanikisha hilo.

2.Wizara ya utalii iwee strategy ya kutumia fursa hiyo ya birthday ya mwalimu kuleta watalii nchini kuadhimisha tukio hilo

3. Vyuo vyetu vya elimu ya juu viandae kongamano zito na la kihistoria kukumbuka miaka 100 ya kuzaliwa mwalimu Julius Kambarage Nyerere

4. Wizara ya michezo iandae michezo, mabonanza, mashindano mbalimbali ya kukumbukia miaka 100 ya kuzaliwa muasisi.

5. Tunataka Lipigwe gwaride moja matata sana ili kumuenzi muasisi huyu mzalendo makini.

6. Wizara ya Utamaduni itafute Muigizaji nchini au nje ya nchi acheze Sinema ya Mwalimu wakati anapigania uhuru (Eddie Murphy anafanana sana na Nyerere alipokuwa kijana). Mandela ana sinema zake, kwa nini mpaka leo hii hakuna sinema moja ya nguvu kumhusu Mwalimu, mkombzi wa Afrika?

Maandalizi yaanze ili ikifika mwaka 2022 tumuenzi Mwalimu inavyostahiki
 
Katika visherehe sivitaki na sijawahi fanya wala kushiriki, ni hivi vi birth day

Otherwise kuhusu mada. Huyu jamaa pale juu sherehe sio kipaumbele chache. Elewa hilo
 
Back
Top Bottom