Serikali iache siasa na ipandishe alama za kujiunga kidato cha Kwanza

Good People

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
945
1,819
Shule zinazozingatia Selection bado zinafanya Vizuri tatizo ni Kua serikali ilijenga shule nyingi na inafanya kila Jitihada kuzijaza pamoja na Kuchukua wanafunzi wasiokua na Uwezo hao ndo wanaleta ongezeko kubwa la wanaofeli Form four. Nimeangalia shule kama kibaha Secondary ambao wanafanya selection kwa umakini haipo top ten kutokana na Na utitiri wa shule lakini imefanya vizuri hata Tabora boys, Mzumbe nk.

Screenshot_2017-01-31-20-21-56.png
 
Ni kweli kabisa, serikali inapaswa kuzingatia ushauri huu. Tunatamani tena kuzisikia Ilboru, Mzumbe, Tabora boys, Msalato n.k

Zamani watoto wa masikini na vichwa haswa walikuwa wakipata mahali sahihi haswaa.
 
Serikali inatumia billion 21 kila mwezi kuudumia wanafunzi wasio productive ( human resources isiyotumika ) kwa nchi..........

Yaani unasomesha mtu nursery mpaka form four halafu anakuwa unproductive unatamba mtaani eti unatoa elimu bure..........

Kichekesho ni kuwa hawa vilaza wakati wanatumia mabilioni na kushindwa vibaya mitihani ya form four kuna wengine watoto wa masikini wanakusanya mabagi na kirudi nyumbani kwa kukosa mkopo wa chuo .............

Sijui ndio mfumo gani wa elimu huu.......
 
Ni kweli inatakiwa kiwango cha ufaulu kiwe juu ili kupta krim safi kabisa ya upambanaji sio ilimradi tu kapata d zake mbili eti kafaulu, ni shida
 
Hatuwezi fanya hivyo wakati ss tunaandaa wapiga kura tena kwa sera yetu ya sasa watoto wote wafike kidato cha nne, hivyo watoto wamefana vizuri tu. Hizi changamoto na watafaulu sana pindi tukikamilisha nyumba za walimu, kulipa madeni yao, kupandisha mishahara na kuwapandisha daladala kote nchini maana Dar tumefanya majaribio na matokeo yake ndo hayo.
 
Serikali inatumia billion 21 kila mwezi kuudumia wanafunzi wasio productive ( human resources isiyotumika ) kwa nchi..........

Yaani unasomesha mtu nursery mpaka form four halafu anakuwa unproductive unatamba mtaani eti unatoa elimu bure..........

Kichekesho ni kuwa hawa vilaza wakati wanatumia mabilioni na kushindwa vibaya mitihani ya form four kuna wengine watoto wa masikini wanakusanya mabagi na kirudi nyumbani kwa kukosa mkopo wa chuo .............

Sijui ndio mfumo gani wa elimu huu.......
Umeongea Ukweli Mtupu mkuu
 
I Ianzishie thread yake hii
 
Kipi bora zaidi; kuongeza kiwango cha ufaulu au kuboresha ufundishaji (quality of delivery). I think the later precedes the former. Kwa maoni yangu, hakuna maana yoyote kuongeza kiwango cha ufaulu kwenye secondary schools kama kwenye shule ya msingi "msingi" imara unaomfanya mwanafunzi afae kwenda secondary haukuwekwa. Kama bado kuna wanafunzi wanaomaliza std 7 ambao hawawezi kusoma na kuandika vizuri, kuongeza viwango vya ufaulu at "O" level kutalisaidia nini taifa?

Okay, ushauri wako mzuri lakini kwa misingi iliyopo kitakachotokea ni kupunguza idadi ya wanaojiunga na chuo na kuongeza street peddlers as result.

Mimi si mtaalamu sana ila hayo ni maoni yangu!
 
Shule zinazozingatia Selection bado zinafanya Vizuri tatizo ni Kua serikali ilijenga shule nyingi na inafanya kila Jitihada kuzijaza pamoja na Kuchukua wanafunzi wasiokua na Uwezo hao ndo wanaleta ongezeko kubwa la wanaofeli Form four. Nimeangalia shule kama kibaha Secondary ambao wanafanya selection kwa umakini haipo top ten kutokana na Na utitiri wa shule lakini imefanya vizuri hata Tabora boys, Mzumbe nk.

View attachment 465842

sina uhakika kama umewaza vizuri unachokisema kwa maana unachowaza ni shule za serikali kushindana vizuri hivyo unajaribu kushauri watanzania wasiopata maksi nzuri waishie darasa la saba.

kwa mtu mzima yeyote hawezi kubeba hoja yako kwa maana haina mantiki katika uhalisia wa maisha. katika uhalisia wa maisha kufanikiwa hakuendani na kuwa best performer kwa darasani. wapo watu wamefanikiwa katika maisha na kufanya mambo makubwa ingawa darasani walikuwa wanachechemea na wale waliokuwa vinara wamebaki kuwa watu wasio na mafanikio au kuwa na mafanikio ya kawaida. ukilitambua hilo hutakaa kamwe kumzuaia mtu asipate elimu kwa kigezo cha best performance bali mfumo wa kila mtu asome kwa kadiri anavyoweza ni mzuri.

jiulize uliosoma nao darasani je mlivyokuwa mkipangana namba ndivyo na ukubwani mlivyopangana katika kufanikiwa? kama mambo hayaendani na hilo basi ujue pendekezo lako haliboreshi bali linaleta ukiritimba wa kurudisha maendeleo ya jamii nyuma.
 
Mkuu wazo lako lina changamoto zake na huenda isiwe fair. Lengo pia ni kuifanya elimu ya sekondari (angalau FIV) kuwa elimu ya lazima kwa wote (compulsory) kama ilivyo elimu ya msingi kwa sasa.

La muhimu sio kufanya michujo mingi kwa kitu ambacho ni cha lazima kwa wote; muhimu ni kwa Serikali kuboresha miundombinu (ifananefanane na akina Feza, Marian, St. Francis, St. Joseph, Tusiime, Loyola, n.k.); kuajiri walimu competent (ikibidi hata ku-outsource kwa baadhi ya masomo kama Kiingereza); na kulipa maslahi ya walimu na watumishi wa shule vizuri na kwa wakati.

Pia motivation kwa wananfunzi kupenda shule ni muhimu. Kwa mfano nakumbuka enzi zile Government School, asubuhi chai kwa mkate, saa nne uji, mchana chakula (usually ugali maharage na mboga za majani), na kwa boarding jioni ni ama ugali/wali/makande maharage au nyama mara mbili hivi kwa wiki. Sina hakika kama hivi vitu siku hizi vinatolewa na kwa ubora.

Pia maktaba na maabara ni moyo wa shule yoyote inayojali elimu bora. Serikali ijenge maktaba na maabara bora; zenye vifaa na kuajiri watendaji wenye fani hizo. Mwanafunzi akienda maktaba apate vitabu vinavyotakiwa.

Utaratibu wa enzi zile mwanafunzi wa eneo moja kupelekwa eneo la mbali na nyumbani kwa ajili ya elimu ya sekondari ulikuwa na umuhimu wake pia. Ulisaidia sana kuwajenga watoto kiakili na hata kuleta ushindani.

Mwisho, maadili yameshuka sana siku hizi yakichagizwa na matumizi ya TEHAMA; nasikia hata adhabu za viboko na nyinginezo siku hizi zimefutwa; ha ha ha; tunapanda mbigiri tukitegemea kuvuna maharagwe.
 
Hapa tumewahi mno kuifanya elimu iwe bure wakati hata changamoto ndogo hazikufanikiwa wakati elimu inalipiwa.
Wakati tunalipia; walimu hawakutosha, vifaa havikuwepo na pia vitabu na zana nyingine zilikosekana.
Hizo billion kadhaa zingeboresha elimu yetu kwanza.
Siamini katika uwingi wa wanaojiunga. tatizo ni ukosefu wa level playing field. Kuna wengine wana kila kitu, wengine hawana chochote kabisa. Serikali, kwa kuwa imeshakosea, isiendeleze popular policies. Ijikite kwenye kuimarisha hawa wanafunzi.
 
Back
Top Bottom