Serikali iache kuchezea pesa za walipa kodi, Pesa za uchaguzi Serikali za Mitaa zirudishwe hazina mara moja

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,954
48,751
Watu hawajajitokeza kujiandikisha uchaguzi wa nini? Hakuna uwanja sawa wa kufanya siasa kati ya upinzani na ccm uchaguzi wa nini? wapinzani wanachaniwa form zao uchaguzi wa nini?

Watendaji wanakimbia ofisi kisa upinzani uchaguzi wa nini.
Yote aya uliyataka mwenyewe baada ya kuzuia siasa mpaka 2020 je 2020 imefika?

Naomba okoa pesa za walipa kodi tukanunue madawati watoto wetu wamefaulu kwenda sekondari kwenda kukaa chini uku tukifanya uchaguzi fake wa mabilioni.
 
Ilikuwa busara kanuni zitenguliwe waliopo waendelee, huu uchaguzi wa mazingira haya unaongeza chuki, fitina na kuhatarisha umoja wa taifa letu. Natamani wale wazee wa inteligensia waseme neno kuahirisha kwa sababu za kiusalama.
 
Technically, badala ya kushauri yasiyowezekana, washauri wanachama wenu wasigombee kama mlivyowashauri wasijiandikishe.

Sisi tuliojiandikisha hata kama ni watano kwenye mtaa tuache tuendelee na uchaguzi maana tunajua umuhimu na uthamani wa uchaguzi.
 
Sisi Watanzania tumeamua uchaguzi usifanyike, Rais wetu mpendwa anapendwa na watanzania woote, Chama chetu CCM kinapendwa na Watanzania woote.. Kufanya uchaguzi ni kupoteza hela na muda.. Tufanye CCM imeshinda mitaa yote na hata 2020 CCM iwe imeshinda Urais, Ubunge na Udiwani majimbo yote kifupi iwe 100%.. Ikiwezekana Upinzani nao ufutwe usiwepo..
 
kwani kuna uchaguzi? mnashindana na nani wakati fomu ziko za ccm pekee
 
Hapa Kazi tu, tutawaburuza hata kwa Kamba. Maendeleo hayana chama, wakati Vasco Da Gama anavumbua dunia mlikuwa kimya, wakati Che Nkapa anauza mashirika ya umma na kufilisi nchi mlikuwa kimya.
 
Sisi Watanzania tumeamua uchaguzi usifanyike, Rais wetu mpendwa anapendwa na watanzania woote, Chama chetu CCM kinapendwa na Watanzania woote.. Kufanya uchaguzi ni kupoteza hela na muda.. Tufanye CCM imeshinda mitaa yote na hata 2020 CCM iwe imeshinda Urais, Ubunge na Udiwani majimbo yote kifupi iwe 100%.. Ikiwezekana Upinzani nao ufutwe usiwepo..
Sasa shida mzee baba Atapataje hela za mabeberu, ndio alihaha sana alipoona wananchi wamegoma kujiandikisha, akaamua siku ziongezwe ili data zibumbwe. Kutwa kuwananga mabeberu mabeberu akiugua anakimbilia huko huko, msaada anakimbilia huko huko na Kabudi wake kutembeza bakuri.
 
Uchaguzi huu wa serkali za mitaa ndio kaburi la upinzani ,tulia utaona

State agent
 
Watu hawajajitokeza kujiandikisha uchaguzi wa nini? Hakuna uwanja sawa wa kufanya siasa kati ya upinzani na ccm uchaguzi wa nini? wapinzani wanachaniwa form zao uchaguzi wa nini?

Watendaji wanakimbia ofisi kisa upinzani uchaguzi wa nini.
Yote aya uliyataka mwenyewe baada ya kuzuia siasa mpaka 2020 je 2020 imefika?

Naomba okoa pesa za walipa kodi tukanunue madawati watoto wetu wamefaulu kwenda sekondari kwenda kukaa chini uku tukifanya uchaguzi fake wa mabilioni.
Tuelekeapo 2020 nafikiri tunahitaji mjadala wa kitaifa kwa mambo mengi ya msingi ikiwemo uendeshaji wa shughuli za kisiasa zilizopo kikatiba na kisheria, na hata usimamizi wa chaguzi za ndani. Nasema hivyo kwa kuwa, hapa tulipofikia hakika tuna mkwamo mkubwa ambapo wenye dhamana wameahindwa kuusimamia kwa weledi na maadili.

Napata mashaka na matokeo halisi ya 2015, pengine hii ndiyo chanzo kikuu cha hofu kwa chama tawala. Mchana kweupe pasipo kuwa na chembe ya haya ama soni, waliokabidhiwa wanafunga ofisi na hata kwa makusudi kukataa kutoa ama kupokea fomu ya watia nia wa vyama vya upinzani, pasipo kalipio lolote!
 
Watu hawajajitokeza kujiandikisha uchaguzi wa nini? Hakuna uwanja sawa wa kufanya siasa kati ya upinzani na ccm uchaguzi wa nini? wapinzani wanachaniwa form zao uchaguzi wa nini?

Watendaji wanakimbia ofisi kisa upinzani uchaguzi wa nini.
Yote aya uliyataka mwenyewe baada ya kuzuia siasa mpaka 2020 je 2020 imefika?

Naomba okoa pesa za walipa kodi tukanunue madawati watoto wetu wamefaulu kwenda sekondari kwenda kukaa chini uku tukifanya uchaguzi fake wa mabilioni.
technically umekosea aya ya mwisho. Hapo kwenye madawati ungeweka ndege, ungesikilizwa.
 
Kabla ya vyama vingi nafikiri tulikuwa tunampigia kura mgombea mmoja, akishindanishwa na kivuli. zama zimerudi baba..
 
Technically, badala ya kushauri yasiyowezekana, washauri wanachama wenu wasigombee kama mlivyowashauri wasijiandikishe.

Sisi tuliojiandikisha hata kama ni watano kwenye mtaa tuache tuendelee na uchaguzi maana tunajua umuhimu na uthamani wa uchaguzi.

Kwa hiyo kuhujumu uchaguzi kunawezekana.
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom