Serikali iachane na sensa 2022 badala yake ishughulikie Katiba Mpya

Man Mvua

JF-Expert Member
Apr 12, 2016
2,184
3,517
Amani iwe juu yenu.

Jambo ambalo lipo wazi ni kwamba watanzania ni watu WABINAFSI SANA na watu wenye kufuata maslahi.

Jambo lingine ambalo lipo wazi ni kuwa KATIBA mpya ni jambo lisilo zuilika kabisa na wanaopinga au kukataa KATIBA mpya basi rudi kwenye pointi yangu hapo juu.

Mifumo mingi ya serikali inabidi ibadilishwe kupitia katiba mpya. Mfano;

Madaraka ya Rais
Kinga za viongozi
Usawa na kula keki ya Taifa
Haki za binadamu na utawala bora
Ubunge viti maalum
UDAS, UDC, URAS NA URC.

USHAURI KWA MH: RAIS SSH

Kwa kuwa mwakani kuna sensa ya watu na makazi iliyotengewa TSH 300+ bilioni ni bora kwa mwakani Wananchi wakashughulikia KATIBA MPYA halafu Sensa ya watu na makazi ikasubiri.

KUCHELEWESHWA KWA KATIBA MPYA NI SABABU TU YA KULINDA MASLAHI BINAFSI WALA HAKUNA KIPYA CHOCHOTE.
 
Sensa ni muhimu sana kwa ustawi wa wanasiasa wetu, dawa za uzazi wa mpango na the like zinakuwa justifiable.

Kama hutoi takwimu za corona, basi angalau useme ipo, kipimo ni mpaka 390,000 huko siku hizi.

Katiba isubiri, tunajenga uchumi
 
umechelewa!
ungekumbuka kuleta huo ushauri mwaka jana tungeahirisha sesa sasa wewe unaleta mwaka huu!!
umechelewa sana kila kitu kimeshaandaliwa.
katiba mpya hadi mwaka 2040.
 
watu wengine wajabu kweli badala ya kudai chakula wanadai katiba!!
kwani katiba ni chakula usema utakula ushibe?!
acheni upuuzi.
 
Dah haya nayo ni maoni ya wasomi kwamba sensa ihairishwe. Mnataka katiba kwa ajili ya wananchi au ili mshinde uchaguzi tuanzie hapo kwanza.
 
Kwahiyo unataka nchi isijuwe idadi ya watu na rasilimali zao ili iweze kuimarisha upatikanaji wa huduma za msingi kwa wanachi mpaka katiba mpya ambayo itatoa vyeo kwa wanasiasa waliopoteza umaharufu.

Swali la kujiuliza, ukitaka kujuwa eneo gani nchini halina wauguzi au waalumu au maji au hata lishe ya kutosha unagalia katiba au unagalia sensa?
 
Sensa siyo pressing issue kwa sasa, kuhesabu watu kulimletea laana mfalme Daudi, wenye uelewa wa hiki kisa watakubali......hiyo bil. 300 ingetumika kwenye miradi ya maendeleo na kufuta kodi za mafuta na ule mchango wa lazima wa solidarity fund kupunguza makali ya maisha kwa wananchi.....lakini swala la katiba mpya libaki palepale maana halina mbadala kwa hali iliyopo...
 
Kwani wakuu hii billion 300 si inabakia hapahapa ndani ya nchi au inakwenda nje?
 
Amani iwe juu yenu.

Jambo ambalo lipo wazi ni kwamba watanzania ni watu WABINAFSI SANA na watu wenye kufuata maslahi.

Jambo lingine ambalo lipo wazi ni kuwa KATIBA mpya ni jambo lisilo zuilika kabisa na wanaopinga au kukataa KATIBA mpya basi rudi kwenye pointi yangu hapo juu.

Mifumo mingi ya serikali inabidi ibadilishwe kupitia katiba mpya. Mfano;

Madaraka ya Rais
Kinga za viongozi
Usawa na kula keki ya Taifa
Haki za binadamu na utawala bora
Ubunge viti maalum
UDAS, UDC, URAS NA URC.

USHAURI KWA MH: RAIS SSH

Kwa kuwa mwakani kuna sensa ya watu na makazi iliyotengewa TSH 300+ bilioni ni bora kwa mwakani Wananchi wakashughulikia KATIBA MPYA halafu Sensa ya watu na makazi ikasubiri.

KUCHELEWESHWA KWA KATIBA MPYA NI SABABU TU YA KULINDA MASLAHI BINAFSI WALA HAKUNA KIPYA CHOCHOTE.
I support you > 100%.
 
Hebu acha ujinga wewe!!!! Hujui kama kupora uchaguzi ni kudhulumu haki na uhuru wa Watanzania kuchagua Viongozi tuwatakao? Hujui kama Serikali kudai haina pesa za kuongeza mishahara kwa miaka sita huku ikifanya yasiyo na tija kama kununua V8 Magari ya kifahari na kujenga airport chato kwa trillions 2 wakati si kipaumbele cha Watanzania ni kudhulumu Watanzania katika sekta muhimu za maendeleo?

Kwanini hutaki kuwa na subira unaharaka gani na kaitba mpya sehemu gani hupati haki yako kama binadamu?
 
Nadhani kwa serikali makini inabidi iweze kubuni aina nzuri ya kujua idadi ya watu wake kupitia mifumo bora zaidi ya kupita kila kaya.

Wakae chini na watu wazuri wa data na IT specialists waweze kuestablish National Database ambapo kila anayezaliwa au kufa information hiyo inakuwa available na kuhakikisha iyo database inakuwa up to date.

Hii ya kupita kila kaya haiko feasible tena ukizingatia life styles za sasa na watu wanavyo hustle kujitafutia maisha.
Alternatively kila Serikali ya mtaa iwajibike kujua idadi ya watu wake kila baada ya miezi sita. NBS ifanye kazi na ofisi za serikali za mitaa kuhakikisha wanapata takwimu halisi kila mwaka.

Hivi NBS kazi zao za kila siku ni nini na wana ofisi kila mkoa? Je kazi kuu ni kuandaa sensa na kunyambua data za sensa kila baada ya miaka 10?

Mbona Wakatoliki wana mfumo madhubuti ambao hata leo ukitaka kujuwa wako wangapi watakupa within a minute.
 
Back
Top Bottom