Serikali: Huko mbele bunge ndilo litaamua kama Tozo ziendelee, zirekebishwe au zisitishwe, wao ndio walitunga hii sheria.

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Akijibu maswali ya waandishi wa habari leo mjini Iringa msemaji wa serikali Gerson Msigwa amesema serikali ni sikivu ndio maana wananchi walipolalamikia tozo ilichukua hatua haraka ikitumia Uwezo alionao Waziri wa fedha kurekebisha kanuni

Msigwa amesema Tozo ni swala la kisheria lililopitishwa bungeni hivyo huko mbele ni bunge hilo hilo litakaloamua kurekebisha au kufuta tozo kwani wao ndio watunga sheria.

Source: TBC
 
Bunge lipi sasa?,hili la CCM ambao wabunge wenyewe wanaomba Kiundwe chombo huru cha kuisimamia serikali?
 
Akijibu maswali ya waandishi wa habari leo mjini Iringa msemaji wa serikali Gerson Msigwa amesema serikali ni sikivu ndio maana wananchi walipolalamikia tozo ilichukua hatua haraka ikitumia Uwezo alionao Waziri wa fedha kurekebisha kanuni

Msigwa amesema Tozo ni swala la kisheria lililopitishwa bungeni hivyo huko mbele ni bunge hilo hilo litakaloamua kurekebisha au kufuta tozo kwani wao ndio watunga sheria.

Source: TBC
Ana Maanisha wale Ma Zuzu sio ?
 
Back
Top Bottom