Serikali hoi kifedha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali hoi kifedha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Dec 25, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  [​IMG]
  Na Saed Kubenea - Imechapwa 14 December 2011

  [​IMG][​IMG]
  SERIKALI ya Rais Jakaya Kikwete iko taabani kifedha. Haina uwezo wa kuajiri watumishi wapya wala kupandisha vyeo wale waliopo, MwanaHALISI limegundua.

  Sasa imeagiza ajira zote serikalini katika mwaka wa fedha wa 2011/2012 zipunguzwe kwa asilimia 50. Vilevile upandishaji vyeo upunguzwe kwa kiwango kilekile.

  Kwa hatua hii, serikali inabadilisha maamuzi ya bunge lililoidhinisha mapato na matumizi yake Juni mwaka huu.


  Serikali imekiri kutokuwa na uwezo wa kutekeleza bajeti iliyopitishwa na bunge, kuwa na vipaumbele tofauti na mashaka na vyanzo vyake vya mapato.


  "Baada ya serikali kutafakari uwezo wake kwa kuzingatia vipaumbele na vyanzo vya mapato, imeamuliwa bajeti iliyokuwa imependekezwa kwa ajili ya mishahara ya watumishi wapya na upandishaji vyeo, ipunguzwe kwa takribani asilimia hamsini, umeeleza waraka wa ikulu.


  Utekelezaji wa hatua hiyo ya serikali ulianza rasmi Novemba mwezi uliopita.

  Waraka wa serikali umesainiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma, Habu Mkwizu na kupelekwa kwa makatibu wakuu wote wa wizara, wakuu wa idara na taasisi zake nyingine.

  Matokeo ya uamuzi huu, waraka unaeleza, "ni kwamba kila mwajiri sasa atalazimika kuandaa upya mahitaji yake ya ikama (taratibu za ajira na malipo) kwa kuzingatia ukomo uliorekebishwa wa bajeti uliotolewa na wizara ya fedha kwa mwaka 2011/12."

  Kila mwajiri amepelekewa jedwali la viwango vya ajira mpya, mishahara na nyongeza; na kutakiwa kufuata mkondo huo wakati wa kuwasilisha maombi mapya ya vibali vya ajira mpya kwa mwaka huuwa fedha.

  Waraka unaagiza waajiri kuweka kipaumbele katika kutenga "nafasi za kutosha kwa ajili ya wataalam wa sekta za Elimu, Afya, Kilimo na Mifugo."


  Nakala ya waraka wa ikulu imepelekwa pia kwa Katibu Mkuu Kiongozi na Msajili wa Hazina.


  Jedwali elekezi linaonyesha kila wizara, idara na asasi/taasisi ya serikali itapata shilingi kiasi gani kwa ajili ya nyongeza ya mshahara, idadi ya ajira kwa mwaka huu na ukomo wa kiwango cha kulipa mishahara yote yakiwa katika eneo la punguzo la asilimia 50.


  Kwa mfano ikulu imebakiwa na Sh. 18,961,106 kwa ajili ya nyongeza za mishahara; itaajiri watumishi 10 na itapewa jumla ya Sh. 2,314,917,441, linaonyesha jedwali.


  Miongoni mwa waliodhinishiwa kuajiri watumnishi wengi zaidi ni Polisi (1,351), Magereza (485), Wizara ya Elimu (417), Kilimo (294), Jamii, Jinsia na Watoto (247), Maliasili (152) na Kurugenzi ya Makosa ya Jinai (111).


  Wale ambao hawataajiri hata mtumishi mmoja ni Ngome, Mahakama ya Ardhi, Mahakama ya Kazi na Jeshi la Kujenga Taifa.


  Lakini miongoni mwa waliobakiziwa fedha nyingi kwa mujibu wa ukomo matumizi kwa mwaka huu ni pamoja na Ngome (288,708,794,879), Polisi (153,274,299,225), Jeshi la Kujenga Taifa (65,562,775,137), Magereza (60,900,159,845) na Elimu (35,997,981,200).


  Kuibuka kwa taarifa ya ikulu kumekuja wakati serikali inadaiwa mabilioni ya shilingi na makandarasi wanaojenga barabara sehemu mbalimbali nchini; madeni ya walimu; kilio cha vyama huru vya wafanyakazi juu ya nyongeze ya mishahara na mikopo ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini.


  Aidha, upungufu huo wa kifedha, umeibua hofu ya kukwama kwa miradi ya maendeleo na ahadi nyingine zilizotolewa na Rais Kikwete wakati wa kampeni za urais muhula wa pili, zikiwemo ahadi za ujenzi wa barabara za ghorofa, ununuzi wa meli, viwanja vya ndege, bandari na reli.


  Vilevile, kupatikana kwa habari hizi kumekuja wiki moja baada ya Rais Kikwete kunukuliwa akisema tatizo la ajira nchini, hasa kwa vijana, ni bomu linaloweza kulipuka muda wowote kuanzia sasa.


  Kiongozi mmoja mwandamizi serikalini anasema kufutwa kwa ajira hizo mpya kutazidi kumuweka Rais Kikwete mbali na wananchi wake. Anasema wananchi wengi hawana imani na serikali kwa kuwa wanaona fedha nyingi za umma zinatumika kwenye semina na safari za viongozi.


  Kwa mujibu wa waraka wa ikulu wa tarehe 18 Novemba 2011,wenye Kumb. Na. BC. 97/109/014/15, kila mwajiri sasa ametakiwa kuandaa upya mahitaji yake ya ajira kwa kuzingatia ukomo uliotolewa.


  Waraka wa ikulu ambao umebeba kichwa cha maneno kisemacho, "Ajira mpya kwa mwaka wa fedha 2011/2012," umetumwa pia kwa makatibu tawala wa mikoa, wakurugenzi wa halmashauri za miji, manispaa na halmashauri za wilaya.


  Miongoni mwa wizara ambazo zitakuwa zimeathirika vibaya na uamuzi huo wa serikali, ni pamoja na tume ya kurekebisha sheria ambayo imepewa mamlaka ya kuajiri wataalam wasiozidi wawili na tume ya haki za binadamu na utawala bora na mahakama ya kazi ambazo zimezuiwa kuajiri kabisa.


  Waraka wa serikali unaonyesha pia kwamba katika mikoa mitano mipya iliyotangazwa na serikali mwaka jana, ni mkoa wa Katavi pekee, ambako anatoka waziri mkuu Mizengo Pinda, ulioidhinishiwa kuajiri watumishi wapya. Umeruhusiwa kuajiri wafanyakazi wapya 46.


  Haikuweza kufahamika mara moja sababu zilizofanya serikali kuruhusu mkoa wa Katavi peke yake kuajiri na kuacha mikoa mingine mipya bila hata kutajwa.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwahiyo wakati wanacheza magwaride juzi kwa mabilioni ya fedha hili halikua limewapitia akilini?Yani ningekua na uwezo ningewakamata wahusika wote niwachape viboko kabla ya kuchukua vijicenti walovyojilimbikizia nimwage pale Posta watu wajichotee.

  Kama wana akili sasa waanze kwa kupunguza posho za kijinga wanazogawana kila siku.Sio wanaofanya kazi wanaambiwa serikali haina kitu wakati waliopo juu wanafanya kuamua tu wapeane kiasi gani.
   
 3. c

  calmdowndear JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 602
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Tumetumia BILIONI 100 kwa ajili ya sherehe za miaka 50

  Tunazo pesa za RADA

  Tunazo pesa za POSHO za wabunge

  Tunawaziri wa fedha mwenye degree feki

  Get over it

  chanzo cha matatizo yetu ni hawa wanasiasa waliolelewa na Nyerere
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Dec 25, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Bongo bana!
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  yeah, sasa chznzo kimekufa, do we die with chanzo or fight to regain some air??
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Dec 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hali kama ndio hiyo iweje wabunge kuongezewa posho za kusinzia bungeni?
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,209
  Trophy Points: 280
  Tumethubutu usanii tumeuweza na sasa tunasonga mbele na usanii wetu....Nchi ina utajiri wa hali ya juu, kwa mfano dhahabu nyingi tu lakini tumewakaribisha wachukuaji na kuwaambia nyie chukueni tu tuachieni 3% inatutosha kabisa. Tunaingia mikataba ya kitaahira na akina IPTL, Symbion na makapuni mengine ya ufuaji wa umeme huku wakitaka walipwe kwa dola wakati mapato ya TANESCO yote ni pesa za madafu. Hongera Msanii kwa kuthububutu usanii na kuuweza na sasa unasonga mbele. Kigumu chama cha magamba kigumu!!!! Zidumu fikra za wasanii wa magamba!! Zidumu...Mmethubutu, mmeweza na sasa mnasonga mbele.

  NB: Huyo Mkulo kazi ya kutengeneza bajeti naona haiwezi kabisa lakini cha kushangaza bado ni Waziri wa ngawira. Nakumbuka December 2010 Serikali ilikuwa imeishiwa kabisa na kuanza kuandika barua kwa wafadhili kuomba pesa mwaka huu hali mbaya kifedha ilianza mapema zaidi, sasa sijui kwanini huyo Mkulo anaendelea kuwadanganya Watanganyika kwamba bajeti yake ni mwaka mzima kumbe huwa ni ya kati ya miezi mitatu na sita tu kisha hazina inabaki haina kitu na kuanza kuombaomba huku na kule na wakati mwingine kuchukua mikopo yenye riba kubwa sana!!!
   
 8. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #8
  Dec 25, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Si wanasinzia vizuri na kwa ustadi
   
 9. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #9
  Dec 25, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Malizia....Nyerere mkatoliki
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Dec 25, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Duh kama hali ni hiyo na haya mafuriko yaliyoharibu miundombinu itakuwaje! Kweli ng'ombe wa masikini hazai!
   
 11. Mkiliman

  Mkiliman JF-Expert Member

  #11
  Dec 25, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  damn this government!
   
 12. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #12
  Dec 25, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Nimekosa Kitufe cha "Thanks" kwa aliyeturushia maana sikulisoma gazeti hili!

  Inauma sana kuona serikali ambayo haikusanyi na kusimamia kodi na haina maono au "vission" ya Tanzania ya Baadae. Uchumi unadorora pamoja na sababu nyingine 1. Usimamizi mbovu wa Kodi 2. Poor allocation ya Financial Resources kiasi kuwa hakuna tangible returns na 3. Kuwa na viongozi ambao hawana uchungu na nchi hii ila wana uchungu na maisha yao tu! Hakuna hotuba za kusisimua zenye maono na motisha hakuna hatua madhubuti za uchumi. Tutamkubuka Mzee Ben. Inatisha... Kama ni bomu basi kipini kitakuwa kimetoka linasubiri kutikiswa...
   
 13. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #13
  Dec 25, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,139
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Kwanini hawako tayari kusema kuwa Wameshindwa Kuongoza na Kutawala Nchi wawapishe wengine....
   
 14. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #14
  Dec 25, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  chanzo ni JK aliyekataliwa na Nyerere, mambumbumbu wakampa kura za kishindo.
   
 15. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #15
  Dec 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Iko hoi tu kila siku, je itakufa?lol

  On the serious note tho, kumbukeni kuliko serikali ifilisike...
   
 16. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #16
  Dec 25, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Kwanza nina hasira cjapewa mshahara,
   
 17. M

  Meshack G Senior Member

  #17
  Dec 25, 2011
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa hali hii tuwe na imani kweli, our gvnt ina masihara sana na wasomi wake....
   
 18. M

  Meshack G Senior Member

  #18
  Dec 25, 2011
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Looh!! Umeliona hilo si utani Benjamin mkapa hakika alikuwa ni jembe lenye makali, tutamkumbuka sana..
   
 19. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #19
  Dec 25, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  People should understand that a country's budget is not only a collection of statistics but it also shows the country's priorities. The budgetary allocations as shown by the above thread are as follows:JWTZ[army] T shs. bilions-289; Police 153 billions; JKT 65 billions; Prisons 61 billions and the EducationMinistry a partry 35 billions which is about a third of what has been given to the army or police!! Bajeti allocations hizi zinaonesha wazi kuwa nchi yetu haina amani bali tuko vitani na ndio maana vyombo vya ulinzi na usalama vinatengewa fedha nyingi kuliko elimu ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wowote unaotaka kushindana katika dunia ya utandawazi. Sasa tujiulize hiyo ni vita gani tunayopigana na ni nanani mpaka tukajihami namna hiyo? Jibu ni rahisi kuwa kwa vile hatuna vita nje ya mipaka yetu vita hii itakuwa kati ya watawala na watawaliwa; bajeti ya namna hii haileti maendeleo endelevu ya nchi bali kudumaza maendeleo kwa kuwakandamiza wananchi kwa kuvihonga vyombo vya ulinzi na usalama.Naomba kutoa hoja.
   
 20. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #20
  Dec 25, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Lizzy, kutegemea walioko madarakani wawe na akili hiyo (and it's a basic logic to be honest) it is expecting too much from them! Serikali iliyoko madarakani ni disaster!

   
Loading...