Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Binafsi naona Serikali hii mpaka sasa imeshajiweka katika mazingira magumu yatayopelekea kukubali mashariti magumu kutoka kwa mtu yoyote (wakiwemo wachina) anaetaka kuwekaza fedha zake katika kukamilisha miradi mikubwa ya awamu ya tano kama ule wa Bwawa la Umeme wa mto Rufiji na ule wa ujenzi wa reli ya kisiasa (SGR).
Kwa mtazamo wangu, sababu ni hizi:
1. Miradi hii imeshaanza kutekelezwa, hivyo ni lazima tupambane iishe vinginevyo itakuwa ni aibu na pigo kisiasa.
2. Tumeshatangaza kwa umma na dunia kuwa miradi hii ni lazima ikamilike na ahadi hii kwa watanzania teyari ni deni la kisiasa na pia ikifeli ni kete kwa wapinzani.
3. Tumeshaingia mikataba na wakandarasi na sijui kama mikataba tulioingia inatambua kusitishwa kwa mradi wakati wowote ule na kwasababu yoyote ile bila kuwa na gharama ya kusitisha mradi husika.
4. Kitaalamu sijui kama inawezekana/ inashauriwa kusitisha miradi ya aina hii pale inapokuwa tayari imeshaanza kutekelezwa.
5. Kusimamisha miradi hii kwa muda sidhani kama ndio itakuwa ni kusimamisha gharama za mradi kwa asilimia 100 ili hali mitambo na vitu vingine tayari viko site na kazi ya ujenzi tayari ilishaanza.
Hivyo basi, kwa kuzingatia sababu hizo hapo juu na nyingine ambazo inawezekana sijazitaja, sioni kama tutaingia kwenye meza ya mazungumzo tukiwa na jeuri ya kukataa mashariti magumu iwapo yatatolewa na Wachina au mtu mwingine yeyote atakaekuwa tayari kuokoa jahazi kwa kuwekaza fedha zake katika hii miradi.
Vile vile sidhani kama mchina au mtu mwingine yeyote ataacha ku-take advantage ya hali hii kutunyonya tofauti na ku-negotiate wakati mradi/miradi bado haijaanza kutekelezwa.
Tusubiri.