Serikali hii ni nzuri sana tu, mbaya ni wewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali hii ni nzuri sana tu, mbaya ni wewe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Profesa, Jun 23, 2012.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Hapa ni Jukwaa la Siasa, na Ndipo penye mashabiki wengi zaidi katika Jukwaa hili:

  Kinachoniogopesha, ni kuwa watu wanailaumu serikali na kuisema vibaya sana, kana kwamba serikali ni mtu mwingine kabisa na si wao ndani ya serikali. Hakuna jinsi serikali inaweza kusimama bila wewe na mimi hapa. Lini mtaacha kulalmika na kuanza kufikiri na kutuletea maoni humu ya miakakati kabambe ya kushughulikia haya tunayoyaona kama ni kero au kikwazo kwa nchi yetu? Ni nini tunapaswa kufanya ili kuifanya Tanzania isimame na kuwa mfano Duniani? na itatuchukua muda gani? na bila mimi na wewe kuanza kuchukua hatua hakuna kitakachotokea, hakuna cha Raisi wala Mbunge ni fikra zangu mimi na wewe unaesoma hapa kuanza kufikiri tofauti, badala ya kulalamika, taja tatizo tueleze suluhisho, tupe moyo na tuhamasishane kuona kuwa tunaweza kuileta Tanzania kwenye nafasi nzuri kabisa.

  Ninaudhiwa sana na wanaoendesha mjadala humunndani ya JF kwa ushabiki wa mambo na hisia zao binafsi ambazo haziwakilishi hoja ya jambo husika linalojadiliwa. na tabia hii ipo mpaka Bungeni. I hope hizi sio pruduct za shule zetu za siku hizi (Media za aina zote kwa hali yake). Kwakuwa shule za siku hizi ni kuwa kama hakuna jambo baya au la aibu hakuna somo (news)!

  Kibaya zaidi nashawishika kuwa watu wengi wana dhana ya kutaka kufanyiwa kila kitu ili watoke kimaisha, na ndio maana tumejenga desturi ya kulaumu, ila sidhani kama wamezuiwa kujaribu yale wanayotaka kujaribu... si serikali au jamii inawazuia, na kama taratibu zinakuwa ngumu, hayo ndiyo ya kuyasimamia yabadilishwe, na si kulaumu, ni kupambana kwa hoja kusimamia kile tunachoamini kinatufaa.

  Kwa kuwa hata kama kusingekuwa na mwanya wa ufisadi ambao wewe usingeujua kama serikali hii isingeonyesha nia ya dhati ya kuushughulikia, bado maisha yako na yangu hayatabadilika kamwe kama hutatumia fursa zilizopo. Fursa zenyewe ni kufanya juhudi katika Elimu, Biashara, Ofisini, Kuwa na moyo wa kuchangia huduma za jamii na kuwasaidia wale ambao wasiojiweza, kulipa kodi kwa wakati (maana huna uhalali wa kuilumu huduma za serikali kama huna record ya kulipa kodi) n.k. Pia na kushiriki katika mijadala ya kijamii ikiwemo mikutano ya serikali za mitaa, na kuhakikisha unatoa maoni yako yanayoboresha (sio malalamiko, kama ni lalamiko na hujui jibu basi ni fursa ya kuuliza, na kuwabana wenye wajibu wao na lazima uwe na uhakika ni wajibu wao na uujue ili iwe rahisi kushauri) kwa nguvu zako zote.

  Natamani kila mtu angepewa nafasi ya kuwa Raisi wa Tanzania, tungeheshimiana. Tuiheshimu serikali, hata iwe ya chama gani nitaiheshimu, ila tutoe maoni na ushauri wa nini kifanyike, hata kama tunaudhika, basi tueleze yale tunayoyaona ni bora, bila shaka wengi humu wa viongozi wanasoma na watajua nini cha kuchukua na nini cha kurekebisha. Mangapi tunayajua wamekuwa wakiyatoa humu? (Hope na mautumbo tunayoyasikia Bungeni hayatoki kwa baadhi yenu humu...) Please ijengeeni JF heshima.
   
 2. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  adamu malima,simbachawene,ikulu kuifanya ya mtu,kiwila,epa,watanzania tumechoka.
   
Loading...