So far away
Member
- Jan 7, 2017
- 58
- 121
Awali watumishi wa Serikalini tulilalamikia sana hatua ndefu ya uhakiki wa vyeti vya watumishi serikalini ili kubaini watumidhi Hewa.
Mambo mengi yalisimama kupisha uhakiki huo. Ajira; nyongeza za mishahara; kupanda kwa madaraja; uhamisho wa watumishi nk vyote vilisimama.
Baada ya kipindi kirefu kupita serikali ikakamilisha uhakiki huo. Na mwezi Mei ndo Mh Rais alipokabidhiwa ripoti nzima ya watumishi hewa na wenye vyeti tata.
Mwanzo tulipewa watumishi hewa walogushi vyeti na tukaona wafanyakazi wenzetu katika ofisi mbalimbali walivyokuwa wakibainika na kutokomea kwa aibu.
Wiki iliyopita yakatoka majina ya wenye vyeti tata, sasa hapa ndo nikagundua kuwa nchi yetu ilikuwa imeoza kweli kwamba watumishi wengi kama nusu ni wenye vyeti vya wengine.
Kumbe hapo zamani; Mtu akifaulu kwenda advanced level (Kidato cha tano)alikuwa akimpa ndugu yake au mtu mwingine cheti kile cha form four na huyu kwenda nacho kusomea eitha ualimu; upolisi; jeshi; unesi n.k. Na wengi walifanya ivo kweli kweli. Ndo maana utakuta utata mwingi uko kwenye cheti cha kidato cha nne.
Sasa hivi watu wanahenya wanatapatapa ndugu wameanza kutupiana lawama. Alie toa cheti na aliepewa. Taaaaabu kweli kweli!!!
Sasa ivi wanashikana uchawi! Enzi hizo walipeana vyeti hiyo vya taaruma hasa vya kidato cha nne kiroho safi sasa wanaangamia.
Kuna wengine wanajifanya kichwa ngumu na wamefungasha vyeti vyao na wameenda Wizarani eti kuonesha na kuhakiki upya vyeti vyao. Mfa maji kweli.... Mimi naomba wakifika hapo wizarani wawaombe waje na wale wanaoshare cheti.
Kama cheti chako cha kidato cha nne kinafanana na cha mwingine kuanzia majina index number na mwaka wa kuhitomu. Kwa mfano kwenye list ile ya watumishi wenye vyeti tata mtumishi namba 555 Joyce Paul S0209- 0061 mwaka 1996 wa Moshi manispaa na mtumshi 322 Joyce Paul s0209- 0061 mwaka 1996 wa Geita. Basi kama mmoja ataenda kulamika basi aje na mwenzie. Aambiwe akamlete na huyo mwenye jina hilo hilo na namba hiyo hiyo na ufaulu huo nk. Hivo basi wote wakija waulizwe nani mwenye cheti orijino kati yao.
Sasa najiuliza je hao walopewa vyeti vya ndugu zao na kuomba navyo ajira na kutumikia taifa hili kwa takribani miaka 30; je hawa si wahujumu uchumi kama wengine. kwa nini wote wasiswekwe rumande na washitakiwe kwa mujibu wa sheria! Je na huyo aliyetoa cheti ( aliyemsaidia mwenzie maisha) hana hatia?