Serikali Hii: Kama mnawapenda vijana wahitimu wa vyuo basi ruhusuni ajira hii kwenye taasisi zenu

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
948
1,092
Habari Tanzania!

Leo nimewiwa wazo zuri sana nimeona ni busara kulileta hapa ili Serikali (mhusika mkuu) na Vijana (walengwa) kuhusu ajira mpya ya kimapinduzi kwa vijana nchi nzima.

WAZO LA AJIRA
Vijana waruhusiwe kupata tenda ya kufanya usafi katika taasisi za Shule za Msingi na Sekondari za Serikali zilizopo karibu na vijana wanapoishi. Aidha kuanzia kijana mmoja au wawili na kuendelea itakavyopendekezwa na taasisi husika kwa kuangazia ukubwa eneo na mazingira ya shule sambamba na idadi ya wanafunzi waliopo katika shule husika.

Vijana wafanye usafi wa mazingira mfano ukataji majani, usafi maliwatoni, kudeki madarasa walau kwa wiki mara moja, upandaji bustani za maua. (Serikali kupitia Wizara ya Mazingira hapa mtatoa wenyewe miti endapo mkihitaji hiyo huduma).

UTARATIBU WA USAFI
Napendekeza usafi ufanyike siku zote za kazi tu; kuanzia saa 12:00 asubuhi mpaka SAA 2:00 asubuhi kabla vipindi vya watoto havijaanza.

OMBI KWA SERIKALI
Naomba Serikali itoe kibali kwa shule kupokea vijana kazi; mtu mmoja mmoja au kikundi au taasisi au kampuni wapige mzigo wa usafi katika taasisi tajwa.

MALIPO NA UJIRA KWA VIJANA
Kwa upande wa maslai ya vijana kuhusu malipo; shule husika itajilipia yenyewe aidha kupitia michango toka kwa jamii husika katika Mtaa au Kata Shule ilipo au zilipo; au wazazi wa watoto husika wachangishwe Tshs. 1,000 /= tu kwa kila mwezi kwa kila mwanafunzi. Hii ni kwa wote.

Hapa malipo itategemea Idadi ya wanafunzi au wa kazi wa Mtaa au Kata husika.

UMUHIMU WA WAZO HILI
1. Hapa Walimu wetu watajikita zaidi kutoa huduma ya kuwapa watoto wetu maarifa na stadi mbalimbali na upande wa watoto au wanafunzi watajikita zaidi kusoma na kuachana na utamaduni wa kuwaza kwenda na vidumu na mafagio mashuleni nk

2. Afya za walimu na wanafunzi zitaimarika na ufaulu utaongezeka maradufu.

3. Nchi itapendeza sana na itavutia kwenye mazingira ya taasisi za elimu ya Msingi na Sekondari kwa kila mtu.

NB

Tutakuza uchumi wa nchi, vijana 80% watapata ajira za moja kwa moja nchi nzima; mfano watengeneza sabuni za usafi, mifagio, wauza madumu usafi, VIFAA kinga usafi nk.

Tatizo la ajira litapungua kwa sehemu kubwa sababu vijana wataunda kampuni au taasisi ndogo ndogo za huduma tajwa hapo juu itachochea Halmashauri na TRA kujipatia mapato kirahisi bila nguvu.

Watoto watajua kazi za usafi wawapo majumbani na sio shuleni. Walio na hofu katika hilo kuhusu watoto kufanyiwa usafi mashuleni; nafasi bado ipo majumbani mwetu kuwafundisha stadi za maisha ya kila siku.

Asante sana

2021
 
Back
Top Bottom