Serikali hii ikitoka madarakani,vyama vya wafanyakazi vitakuja kufungua kesi kudai nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma ambayo sasa haitolewi

True hata mkoloni aliyatumia kwenye kazi za nguvu sio za kutumia akili wengi walipelekwa tanga kulima mkonge na wengine makuli bandarini.Kazi za kutumia akili huwa wanachemka sana VIATU vinapwaya.

Ubaguzi mnautaka sana
 
Serikali ya awamu ya tano,kama ilivyo kwa serikali zote za CCM zilizotangulia,imeendeleza tabia ya kutolipa watu haki zake huku awamu hii ya tano ikija na maajabu ya kutotoa nyongeza ya mishahara ya kila mwaka kwa watumishi wa umma nyongeza ambayo ipo kisheria na ambayo haitolewi kwa mapenzi ya Raisi au serikali anayoiongoza bali hutolewa kwa mujibu wa sheria.

Kwakuwa nyongeza hii iko kisheria,basi ni swala la muda tu kabla ya watumishi kupitia vyama vyao vya wafanyakazi(visivyoongozwa na makada), kuja kufungua kesi mahakamani na kudai nyongeza hiyo ambayo itakuwa ni kwa mabilioni kwani katika miaka yote minne ya utawala huu, nyongeza hii imetolewa mara moja na kama sikose ni katika mwaka wa fedha uliiopita(2018/2019) ila miaka mingine yote ukiwemo mwaka huu wa wa fedha wa 2019/2020 hakuna kilichoongezwa hivyo ni wazi deni litakuwa kubwa tu.

Kama nyongeza hiyo ilitolewa kwa miaka yote niliyoitaja ukiwemo na mwaka huu wa fedha wa 2019/2020,basi niko tayari kukoselewa.

Tundu Lissu alikuwa sahihi sana kusema tuwe na sheria inayoruhusu kukamata mali za serikali kwani hii ndio njia pekee ya kulazimisha hizi serikali zilipe madeni yake.

Wao(wanasiasa) wanajilipa vizuri tena kwa wakati ila kulipa haki za watu wengine wanaona tabu(ubinafsi)!!
Yaani sio wafanyakazi tu, kuna msulululu wa watakaodai na kulipwa waliovunjiwa nyumba zao, waliofukuzwa kazi kwa dhuluma a.k.a.tumbuliwa, waliochukuliwa fedha zao maduka ya kubadilisha fedha, vyeti feki, wafanyabiashara walionyang'anywa mashamba, wanaoporwa fedha zao benki, wakandarasi, wakulima wa tumbaku, Korosho, pamba, mbaazi, waliobambikwa kesi mbalimbali wote watalipwa tu.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom