Serikali: Hatujalipa kuweka tangazo jengo la Burj Khalifa lililopo Dubai

Mwananchi Huru

JF-Expert Member
Nov 20, 2021
1,446
997
Msemaji wa Serikali kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema haya..

Serikali HAIJALIPIA kuweka tangazo la Tanzania katika jengo refu kuliko yote Duniani liitwalo Burj Khalifa lililopo katika Jiji la Dubai.

Tangazo hilo limewekwa kwa lengo la kuitangaza Tanzania kutokana na uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi yetu na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Utawala wa Dubai umeweka tangazo hilo kwa kutambua ziara ambayo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kaifanya Dubai na umeahidi kuendelea kuitangaza Tanzania kupitia jengo hilo maarufu.

Pia soma

===
GHARAMA zilizoelekezwa na mamlaka ya uendeshaji wa jengo refu zaidi duniani la Burj Khalifa lililoko Dubai hutoza kati ya US$ 67,000 ambazo kwa ubadilishaji fedha kwa haraka haraka inafiki TZS 150M kwa dakika 3 kuweka tangazo kwenye jengo lote hilo la Burj Khalifa.

=>Gharama kwa lisaa limoja ni jumla ya TZS 3BL,

=> Gharama kwa siku moja ni TZS42BL

=> Gharama kwa siku 30 ni TZS 2.2Trilioni,

=>Kwasababu ya mahusiano mazuri kati ya mamlaka za Tanzania na Dubai tumepewa kujitangaza bure Kabisa kwa siku 30,

Nani Kama Rais Samia Suluhu Hassan?


Hoja yangu ni nini hapa,

Kwanza, Huu ni ushahidi wa wazi kwamba sasa ni rasmi Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefunguka Kitaifa & Kimataifa,

Pili,Kupitia matangazo haya Tanzania inakwenda kupata idadi kubwa sana ya wawekezaji wa nje na watalii ambao pengine haijawahi kuwashuhudia tangu Uhuru wake,

Tatu,Rais Samia anakuwa ni Rais mwenye ushawishi zaidi kusini mwa jangwa la Sahara ndani ya muda huu mfupi ( rejelea ziara zake za Ufaransa na Ubelgiji )

Nne, Burj Khalifa ni taasisi yenye zaidi ya followers 10M kwenye akaunti zake za Tweeter, facebook,Telegram na Instagram na nimejaribu kupitia accounts hizi Tanzania ina-trend kwa kasi,
FM04B4mWYAInVdH.jpg
 
kuna mtu Tanzania aliwajaza watanzania upumbavu kiasi kwamba wao wanahisi kila kitu wanapigwa au hela zinatumika vibaya ila faida zake hilo bango hawajui ni watu wangapi watashawishika kutaka kujua hii nchi na kuja kuwekeza au kutalii na hapo ajira zitakuja na serikali itapata kodi ambayo itaendesha nchi
 
kuna mtu Tanzania aliwajaza watanzania upumbavu kiasi kwamba wao wanahisi kila kitu wanapigwa au hela zinatumika vibaya ila faida zake hilo bango hawajui ni watu wangapi watashawishika kutaka kujua hii nchi na kuja kuwekeza au kutalii na hapo ajira zitakuja na serikali itapata kodi ambayo itaendesha nchi
Mtu aje kuwekeza sababu kaona Bango ? Huyo sio Muwekezaje bali kanjanja au Machinga..., Watu wanafanya due diligence za kufa mtu na wanawekeza kwa kuona / kuangalia stability ya mambo yao na sio kubadilika kila dakika.....

Ni more cost effective kuwa na Sera za kueleweka , infrastructure za maana na labor force yenye technical know how (wawekezaji watakuja tu) unaweza hata ukaweka tangazo kwenye mwezi kila kiumbe alione ila hali halisi field ndio inafanya watu waje au wasije (na kama hali mbaya bado wanakuja fahamu kwamba wanapewa favor ambayo mtoaji anaumia) as the saying goes kibaya chajitembeza.....
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom