Serikali hatimaye yakiri ilichokwepa kwa miaka karibu minne!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali hatimaye yakiri ilichokwepa kwa miaka karibu minne!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 8, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  JK Aunda Tume Kutayarisha Mfumo Mpya Wa Mikopo Elimu Ya Juu
  [​IMG]

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTEUZI WA TUME YA KUTAYARISHA MFUMO MPYA WA KUGHARIMIA/KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU


  Katika hotuba yake ya kukizindua rasmi Chuo Kikuu cha Dodoma Novemba 25, 2010, Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete aliahidi mambo makubwa mawili kama ifuatavyo, nanukuu:

  Moja: “Kuhusu mikopo ya elimu ya juu napenda kuwahakikishia wazazi na wanafunzi kuwa tutaendelea kuongeza fedha katika mfuko huo ili wanafunzi wengi zaidi wanufaike. Tumefanya hivyo katika miaka mitano iliyopita na tutafanya hivyo siku za usoni. Serikali iliongeza fedha za mikopo kutoka shilingi bilioni 56.1 mwaka 2005/06 hadi kuwa shilingi 237 bilioni mwaka 2010/11 na wanafunzi waliopatiwa mikopo hiyo wameongezeka kutoka 16,345 hadi 69,921. Haya ni mafanikio makubwa na naahidi kuwa tutafanya vizuri zaidi ili tuwafikie wanafunzi wengi zaidi; na

  Pili: Pia tutautazama upya mfumo mzima wa utoaji wa mikopo ikiwepo na utendaji kazi wa Bodi ya Mikopo kwa nia ya kuuboresha na kuleta ufanisi zaidi. Mawazo ya wadau wakiwemo wamiliki wa vyuo, wahadhiri na wanafunzi, yatasaidia sana”.

  Ili kutekeleza ahadi hiyo ya Pili, Mheshimiwa Rais ameteua Tume ya wataalam 11 kufanya mapitio ya mfumo na uendeshaji wa Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini kwa lengo la kuimarisha utoaji wa mikopo hiyo. Tume inatakiwa kufanyakazi kwa siku 60, kuanzia tarehe 14 Februari 2011 na kuwasilisha ripoti yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi tarehe 15 Aprili 2011.

  Tume hiyo itaongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Makenya Abraham Maboko.

  Wajumbe wengine wa Tume hiyo ni Bw. Masoud Mohamed Haji, Ofisa Uhusiano wa Kimataifa, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Zanzibar; na Dkt. Eliawony Kristosia Meena, Mhadhiri Mwandamizi (Elimu), Chuo Kikuu cha Tumaini Arusha.

  Wengine ni Bw. Daniel Paul Magwiza, Naibu Katibu, Tume ya Vyuo Vikuu; Bibi Sarah K. Baharamoka, Mkurugenzi Msaidizi (Uandishi Sheria), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Profesa Penina M. Mlama, Mkurugenzi Mtendaji wa Tawi la Tanzania la Taasisi inayopigania Elimu kwa Wanawake (Campign for Female Education Tanzania Chapter).

  Katika Tume hiyo pia yumo Bw. Deo Mbasa Daudi, Ofisa Taaluma, Chuo cha Usimamizi wa Fedha, ambaye ni Rais Mstaafu wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam-DARUSO (2007/2008), na Katibu Mkuu Mstaafu wa DARUSO (2006/2007); Bw. Kassim Almasi Umba, Makamu Mkuu wa Chuo (Utawala na Fedha), Chuo Kikuu cha Kiislamu, Morogoro; Bw. Anderson Y. Mlambwa, Mkurugenzi wa Mikopo, Benki ya CRDB; Prof. Wilbert Abel, Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Bibi Rosemary Rulabuka, Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Elimu Tanzania.

  Tume itateua Makamu Mwenyekiti kutoka miongoni mwa Wajumbe. Sekretarieti ya Tume hiyo itatokana na Wajumbe kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi; Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; na Ikulu.

  Hadidu za Rejea za Tume hiyo ni pamoja na kuchambua kwa kina Sheria Na. 9 ya mwaka 2004, iliyounda Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu, na Kanuni zake na kubainisha vifungu vinavyohitaji marekebisho kulingana na hali halisi ya utoaji mkopo na kuangalia upya vigezo na sifa zinazozingatiwa katika utoaji wa Mkopo endapo vinakidhi haja na mahitaji halisi ya waombaji na taifa kulingana na makusudio ya kuundwa kwa Bodi ya Mikopo.

  Nyingine ni kuangalia kwa kina muundo wa Bodi na ufanisi wake katika utoaji na urejeshwaji wa mikopo na kutoa mapendekezo na kuchunguza kiini cha malalamiko na mahusiano yasiyoridhisha kati ya Bodi na Wanafunzi, Bodi na Taasisi ya Elimu ya Juu na kati ya Bodi na Wizara ya Elimu na kutoa mapendekezo ya namna ya kurejesha mahusiano mazuri.

  Hadidu nyingine za rejea ni kuchambua mfumo mzima wa namna ya kubaini wanafunzi wanaohitaji mikopo (Means Testing) ili kuibua mapungufu yake na kupendekeza taratibu za kuuboresha au kuwa na mfumo mbadala na kuangalia mambo yanayosababisha mifuko mingine kama vile “Resource Endowment Fund” wa Maliasili unafanikiwa na Nchi nyingine zenye mazingira kama ya Tanzania zinavyofanikiwa kugharimia Elimu ya Juu kwa mfumo wa Mikopo.

  Nyingine ni kutoa ushauri na mapendekezo yatakayowezesha Mkopo utolewe kwa wanafunzi wengi wahitaji wa Elimu ya Juu ili kuondoa lawama zilizopo na kushughulikia mambo mengine yoyote yatakayoweza kuboresha mfumo huo kwa kadri inavyoonekana inafaa.

  Ni matumaini ya Serikali kwamba baada ya Tume hiyo kukamilisha kazi yake, itatoa ushauri utakaosaidia kujibu malalamiko mbalimbali kuhusu utendaji kazi wa Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu.

  Mizengo P. Pinda (Mb)

  WAZIRI MKUU

  6 Februari 2011

  My Take:
  Kama wangesikiliza tulipoanza kulalamikia hili dubwasha wala wasingefika hapa. Na kwa vile ni watu wale wale wenye fikra zile zile naweza kuahidi kuwa watakuja na matokeo yale yale...
   
 2. D

  Deo JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,190
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kama Rais Kikwete hawajui wamiliki wa Dowans basi na Papa hajui Vatican ilipo! Feb 5, 2011.

  Sawa kabisa Dowans ni sawa na Vatikani kwa Papa na Ikulu kwa kikwete
   
 3. l

  limited JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hakuna wizaa inayosimamia vyuo vikuu? where the hell are we going every thing ni tume ni nini hasa hasa kinachotokea kwa viongozi wetu? kwa nini watu hwawajibishwi kunapotokea matatizo ya kiutendaji serekalini?
  so ina maana kila mtu atafanya madudu akijua at the end itakuja tume kujadili mie sielewi tunaenda wapi
   
 4. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tume tume tumeeeeeee na KODI zetu......hii inamaanisha wizara ya Elimu pamoja na kuwa na wasomi na wataalamu bado tu iko sidelined kati jambo kama hili?

  Kimantiki na kiufundi utekelezaji unaweza kuleta utata maana utakuwa wa kitu walicholetwa wengine kutoka nje watafute suluhu wakati wahusika wapo tu hapo wanakula viyoyozi badala ya kufanya kazi hii.


  Anyway, ngoja tu tukubali.

  Pia pamoja na msukumo wa hoja kutoka kwa wapinzani na wanafunzi wenyewe, ninawasiwasi isijekuwa imeanzishwa kwa pupa ili kusettle some circumstances halafu matokeo yasiwe na political commitment nyuma yake

  Tuombe tu kamati ije na suluhisho la tatizo hili ambalo limekuwa na utata toka kuanzishwa kwake
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sijaona uwakilishi wa wanafunzi wahusika hapo yaani waliogoma.mwanafunzi wa 2008 ambaye 5000 ilimtosha hataweza kutetea madai ya 10000 kwa sasa.
  Ushauri:TUME IWEKE KANDO SIASA HATA KAMA MIGOMO ILICHOCHEWA NA WANASIASA.
   
 6. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  mimi naona hapo ni kiini macho. Je serikali (wizara husika) imeshindwa kutafsiri na kufanyia kazi sheria ya mikopo ya 2004? Hizi tume ni wizi wa wazi wa mali ya umma. Je wajumbe wake wanalipwaje? Ingefaa pia na gharama itakayoingia Tume iwekwe wazi. Pia vigezo vilivyotumika kuchagua wajumbe viainishwe wazi. Vinginevyo sheria ya mikopo irudishwe Bungeni ikaandikwe vizuri.
   
Loading...