Serikali hamuoni hatari ya matumizi ya Dursban Insecticide mashambani?

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
11,324
17,829
Heri ya mwaka mpya wana JF.

Kuna tatizo kubwa sana lipo mtaani hasa huko vijijini kwa wakulima na mijini kwa walaji wa mazao ya mbogamboga kama nyanya na matunda ya matikiti na matango.

Tatizo ni matumizi holela ya kemikali ya sumu ya kuulia wadudu inayotumika mashambani aina ya Dursban (au chlorpyrifos) kwa jina lingine la kitaalamu.

Hii dawa au sumu ni hatari sana kwa mazingira hasa ikiliwa au ikiguswa na binadamu, nimeona inatumika sana huko mashambani tunako tafuta riziki kwenye kilimo cha matikiti n.k.

Dawa hii imesitishwa matumizi yake nchi zilizoendelea kama Marekani tangu mwaka 2000 hadi kufikia mwaka 2004.

Dawa hii ipo ktk kundi la sumu zinazofanya kazi mfano wa 'nerve gas' nadhani wengi hapa mtakumbuka tukio la 4 March 2018, la Sergei Skripal na bintiye Yulia Skripal walipo okotwa wakiwa hoi mtaani kule Salisbury nchini England.

Huyu jasusi mlakotekote (Double Agent) wa Uingereza na Urusi alikumbana na sumu inayo fanya kazi kama hii lakini yenyewe imeongezwa ukali iweze kuuwa binadamu kwa haraka sana.

Sumu hii hufanya kazi kwa kusisimua kemikali (electrochemical) inayofanya kazi ya mawasiliano kati ya mfumo wa fahamu na misuli. Inachofanya ni kusisimua (stimulate) kwenye mishipa ya fahamu kupita kiasi na kusababisha misuli au mishipa isifanye kazi vizuri na mwisho kupooza na kufa haraka sana kama mhanga akipata dozi kubwa ya hii sumu. Hii inatambulika kuwa ktk kundi la familia ya organophosphates.

Sumu hii hutumika kuuwa au kudhibiti wadudu mbalimbali kwenye mashamba, majumbani, kwenye bustani n.k. ikiwalenga wadudu kama panzi, mende, bui bui hasa aina ya utitiri (walima matikiti na nyanya wanawajua) mole cricket (sijui Kiswahili chake) nk.

Labda niwataje wachache kwa kimombo ni ants, cockroaches, aphids, fleas, wasps, and spiders na wengine wengi wanao sumbua mashambani.

Ubaya wa matumizi ya hii sumu:

Sumu hii ukiachana na kazi yake ya kuuwa wadudu waliokusudiwa pia huwadhuru viumbe wengine kama ndege, binadamu, samaki na nyuki ambao ni muhimu kwa mazingira. Hii ilipelekea mamlaka ya utunzanji mazingira ya marekani (United States Environmental Protection Agency - EPA ) kuzuwia matumizi yake nchini mwao toka mwaka 2001 baada ya kuona madhara makubwa yanayoweza kuwapata wanawake na watoto baada ya kutumia hiii kemikali mbaya na hatari.

Fikiri jinsi inavyo tumika kiholela na wajasiriamali wa kilimo wa kitanzania kwenye mabonde ya Mto Ruvu na kwingineko kisha inaingia kwenye chanzo cha maji kama mto Ruvu yanayo tumiwa na wakazi milioni kadhaa wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani!

Sitaki kuwatisha ila najaribu kukumbusha wenye dhamana wasisubiri waanga wengi wa magonjwa kama ya saratani na mtindio wa ubongo kwa watoto watakao zaliwa maeneo hayo yanayo athiriwa na hii kemikali.

Tatizo kubwa watumiaji wa hapa kwetu wengi elimu ndogo hawajuwi namna ya kuepuka kuchafua mazingira na kuji hatarisha wao na walaji wa bidhaa zao.

Nikiangalia watu wanavyo kula matikiti hapa Dar na yanayo endelela mashambani naogopa sana nini kinakuja kutokea miaka ijayo.

Shida hii pia inakuja kuletwa na dawa ya kuuwa magugu iitwayo Roundup. Hii itawamaliza sana watu maana sasa watu hukwepa gharama na usumbufu wa kufanya palizi kwa kulima au kungo'a magugu watu wanamwaga hii dawa kwisha kazi, hii dawa iki kugusa tu mwilini ile phosphate iliyomo ndani yake inaanza kuleta shida ktk mwili na kutengeneza saratani.

Round-up imesababisha kesi kubwa za madai huko Marekani baada ya wafanyakazi kwenye bustani (lawns) na mashambani kuathirika na hii kemikali.

Nawaona vijana mashambani wanaigusa wakati wanamwaga shambani bila mavazi na vifaa maalum vya kujikinga isikuguse. Wanaingia shambani kabla ya siku zinazo ruhusiwa n.k.

Tatizo hawana elimu husika, inatakiwa mamlaka husika isimamie hizi kemikali zisiuzwe na kila mtu kiholela kuwe na utaratibu flani unao fanana kama ilivyo kwa dawa za binadamu lazima uende na cheti cha daktari kisha upewe maelekezo.

Kuna hadithi (story) zingine unasikia kila siku kwamba kuna mpango wa kupunguza watu maskini wasizaliane kwa kasi kwenye nchi za dunia ya tatu. Inaonekana ni uzushi tu (Consipiracy theories).

Hakika dawa ya Dursban inahusishwa na kutumika katika kashifa hiyo ya mkakati wa kutupunguza idadi wanyonge toka nchi za kinyonge.

Bebreru sio mtu mzuri kabisa, kaweka pesa mbele kuliko utu (in Nyerere's voice or in President Magufuli's voice) hapa wasaidizi wa mzee msinifuate kama yule msanii wa kuchekesha, sio kila wakati tunaongea serious tu.

Ni kwamba baada ya kukatazwa Marekani na nchi zingine ikaonekana kampuni zilizo tengeneza kwa wingi hii sumu, na wafanyabiashra wanao imiliki kwa wingi ktk maghala yao watapata hasara kubwa hivyo ikaruhusiwa iuzwe na kupunguzwa taratibu mwisho mwaka 2004 na baada ya hapo nyingine ipelekwe nchi maskini dunia ya tatu.

"When delaying tactics have finally stopped entirely, our government then allows these known toxins to be sold to third-world countries so their population of humans and wildlife can be harmed. "

Source: hapo chini mwisho wa thread.

Na hiki ndicho kilichotokea imeletwa na inauzwa hapa Tanzania hadi kufikia mwaka 2017 nimenunua na kuitumia hii shambani kwangu baada ya kushauriwa na wakulima wenzangu, huenda hadi sasa tarehe 4 mwezi January 2020 bado ipo nyingi sana sokoni Kariakoo pale na sehemu zingine hii sumu hatari.

Someni zaidi hapo chini:

Why Banned Toxic Substances Diazinon & Dursban are Still In Use Today: An Interview with Environ
Dursban Insecticide | What is Dursban used for?
 
Watetezi wa mazingira, mtandao wa kilimo cha kijani, TBS, TFDA, wizara ya Kilimo, NEMC wote njooni hapa tujadili hili janga.
Yeyote unae mjuwa mdau ambae yupo hizo taasisi mwite hapa aje atoe hoja na ushauri.
 
Tunaofanya kilimo hai tunaonekana kama wehu kwasasa lkn muda utaongea. Wazungu wamekuja na mfumo wa certification kwa wakulima wa tz ili kuhakikisha watu wao hawali sumu.
Elimu ya kutosha inahitajika ili watu waelewe uzuri wa kula organic products na madhara ya inorganic farming. Ukiangalia mbogamboga zinavyolimwa na kutunzwa in conversational way huwezi kula. Soko la ulaya kila wiki wanatoa list ya madawa yaliyofungiwa lkn sisi tupo kimya tunaangamia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeandika kitu bora Sana Yani, Kuna Dada mmoja ana mahekari ya mpunga mbarali kule, nilimuuliza anatumia dawa gani kuua magugu akasema round up nikamuuliza Si umesikia madhara yake akasema yeye ale nini Sasa...
Yaani ni dawa nyingi mno, hizi hoho, nyanya acha tu, mtu anapuliza Leo kesho anauza..
Nafikiri mamlaka husika wangekaa chini na kufikiria nini cha kufanya. Ndo maana wanunuzi toka nje hawanunua bidhaa ovyoovyo tu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuongezea kwenye huu mjadala nyeti na wenye chachu ya kusaidia sekta ya kilimo uchumi kuwa ya tija sio tu kifedha bali na kiafya na kimazingira, ningeomba kuhoji kuhusu swala la uwepo wa hizi mbegu za kibailojia yaani mbegu zsizo za asili ambazo hutengenezwa maabara kinyume na zile za asili.

Hivi ghala ya taifa ya mbegu ipo?!

Je hizi mbegu za asili ambazo zinakuwa zinapandika tena baada ya kuoteshwa kwa maana ya kuwa recyclable zinahifadhiwa au kulimwa katika mashamba maalumu?!

Kwasababu ukitazama mbegu za kisasa zote ni kama zinalazimu matumizi ya mbolea na dawa za wadudu of which kwangu naona ni set up ya kibishara kwa mataifa yetu masikini kugeuzwa soko la pembejeo za kilimo na mashine za kilimo.

Hivi hawa vilaza/ndezi (wakalia mamlaka wanaojiita viongozi ila sifuri kabisa) wanayajua haya tunayoyajadili hapa.....?!

Naomba wadau tuejane bayana hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom