Proud-Tanzanian
JF-Expert Member
- Nov 26, 2015
- 217
- 90
WanaJF,
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadick ameongea na vyombo vya habari na kueleza kuwa, serikali haina mpango wowote wa kulipa fidia au kutoa viwanja kwa mara nyingine kwa wakazi wote wa mabondeni ambao nyumba zao zimewekewa alama ya bomoa (X).
Mkuu wa mkoa huyo pia amewasisitiza wakazi wa mabondeni kutii agizo la serikali la kutoka mara moja kwenye nyumba hizo na kupisha ubomoaji na ametoa onyo kali kwa watakao kaidi agizo hilo la serikali.
Ikumbukwe kuwa serikali kupitia halmashauri zake imekuwa ikitoa viwanja kwa waathirika wa mafuriko ambao ni wakazi wa mabondeni kila mara mafuriko yanapo wakumba wakazi hao...ila imekuwa kawaida kwa wakazi hao kuuza maeneo waliyopatiwa na serikali na kurudi mjini kwenye maeneo yale yale yaliyoathiriwa na mafuriko.