Serikali haiwezi kukwepa lawama ya kuadimika na kupanda kwa bei ya Saruji nchini. Waziri wa Viwanda ana kazi sana, kuna janga linatunyemelea

Hapa tuseme kuanzia last year ndio matumizi ya saruji yameongezeka, kwa wingi wa miradi ya serikali ya awamu hii naamini itakuwa inachangi, lakini pia naamini wafanyabiashara wa saruji wanaweza kuwa na siri zao kama nilivyosema kwenye issue ya sukari last time.

Hawa watu mara nyingi huwa wana tabia za kununua mzigo mkubwa na kuuweka kwenye godown kuangalia upepo utavyokuwa.
Cement sio bidhaa ya kufungia godown
 
Waziri wa Viwanda hajateuliwa! Sijui huyo atakayeteliwa atakauja na sera gani! Maaana sera ya Tanzania ya viwanda imeishia wapi.
 
Habarini wakuu na raia wenzangu wa taifa la chama kimoja, japo nna uchungu mkubwa, lakini kamwe siwezi kuwa mvivu wa kutumia kalamu yangu kuihabarisha jamii na taifa langu, nimeteseka sana kwenye hii nchi, na nimekuwa nikitamani kuona hii nchi siku moja inapiga hatua moja ama nyingine - socially, economically, politically, legally etc, lakini so far, i am disappointed big time.

*****

Kumekuwepo na malalamiko ya kuadimika kwa Cement na kwamba hata inapopatikana bei inakuwa ni juu sana karibia ongezeko la asilimia zaidi ya 55% kulinganisha na bei ya mwanzo (TZS 14,000 mpaka TZS 22,000) huku baadhi ya maeneo yakishuhudia bei ikikaribia TZS 35,000 kwa mfuko.

Wakati huo huo nimeona viongozi wa serikali; wakuu wa mikoa, wilaya, na hata wakuu wa jeshi la Polisi wakisisitiza nyakati tofauti kwamba, watamchukulia hatua yoyote ambaye watamkuta anauza kwa bei kuzidi bei ya awali, yaani TZS 14,000.

**

Kwanza kabisa niseme, serikali inahusika moja kwa moja na huu upungufu tuonaouona, na visababishi vikubwa ni 1) ‘Sera za miundombinu kwenye utawala wa awamu ya tano wa serikali ya Magufuli’. 2) ‘Serikali kufinya jithada za uwekezaji kwenye sekta ya cement’

1... Serikali ya Magufuli, ilikuja na mkazo wa kasi sana wa kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya miundombinu hapa nchini.

  • Nyerere Hydropower Plant – USD 3.9 Billion (TZS 9 Trillioni) Timeline > 2019 - 2022
  • SGR Project – USD 14.2 Billion (TZS 32.9 Trillioni) Timeline > 2019 - ?
  • Ubungo Flyover & Tazara Flyover - USD 150 Million (TZS 300 Billion)
  • Salender Ocean Bridge – USD 126 Million (TZS 292 Billion)
  • Kigongo Busisi, Daraja jipya la wami, Ikulu Dodoma, Nyumba za serikali Dodoma n.k
  • Upanuzi wa bandari na viwanja vya ndege
  • Na tumesikia kwenye hotuba ya Rais leo kwenye ufunguzi wa bunge, inaonekana shuhuli za ujenzi zitaendelea kushamiri miak miwili mpaka mitatu ijayo.


Ukiangalia takwimu, ni kwamba kwa kipindi cha utawala wa Magufuli, sekta nzima ya ujenzi (construction) imeweza kuwa na wastani wa ukuaji mkubwa sana (wastani wa asilimia 17.45% kwa miaka mitano iliyopita), na driver kubwa ikiwa ni hiyo miradi mkubwa ya ujenzi ya serikali.

View attachment 1625717

Kwa sababu, Cement ni mali ghafi muhimu sana katika sekta ya ujenzi, unapokuwa na ukuaji wa kasi sana wa sekta ya ujenzi maana yake unatakiwa kuwa na ukuaji wa kasi kubwa maradufu ya uzalishaji wa Cement ili uweze kuhudumia kikamilifu mahitaji ya sekta ya ujenzi.

Kosa kubwa lililofanyika ni kwamba, serikali wali focus zaidi kutekeleza miradi hii mikubwa ya ujenzi bila kuangalia uwezo binafsi wa uzalishaji wa viwanda vya ndani vya Cement (supply capacity).

Mbali na kutokuangalia uwezo wa uzalishaji wa viwanda vya ndani, ni kweli kwamba serikali haikuwa rafiki kwenye kuhakikisha wanawezesha mazingira ya uwekezaji kwenye viwanda vya cement, ukifuatilia fitina alizofanyiwa mwekezaji Aliko Dangote, hakika hutatofautiana na mimi kwamba kuna mahali serikali haikutimiza wajibu wake kudhibiti uimara wa soko la cement.

View attachment 1625718

2014
2015
2016
2017
2018
2019
Uzalishaji wa Cement kwa Tani - Tanzania2,809,1003,134,9004,071,4004,199,9004,509,1006,514,700
Ukuaji wa uzalishaji wa Cement - %n/a
11.6%​
29.9%​
3.2%
7.4%
44.5%​
Asilimia za ukuaji wa sekta ya ujenzi - %n/a
15.9%​
17.8%​
18.0%
17.1%
18.6%​
Wastani wa ukuaji wa pato la taifa (GDP) - %n/a
6.0%​
6.0%​
6.0%​
6.0%​
6.0%​
Multiplier ya ukuaji wa sekta ya ujenzi ukifananisha na ukuaji wa pato la Taifan/a2.652.973.002.843.10

Ukiangali hizo takwimu, viashiria dhahiri vya msukosuko wa cement vilianza kujitokeza kuanzia mwaka 2017 na 2018, ambapo utaona wazi ukuaji wa uzalishaji wa cement ulikuwa kiduchu sana (3.2% kwa 2017 na 7.4% kwa 2018) ukifananisha na ukuaji wa sekta ya ujenzi (18.0% mwaka 2017 na 17.1% mwaka 2018). Kama ni janga basi lilianzia kwenye hii miaka 2 (2017 & 2018).

Ndo mana unaona, pamoja na ongezeko kubwa la 44% kwenye uzalishaji wa cement kwa mwaka 2019, lakini bado bei ya cement ilianza ku-shoot tangu tuanza huu mwaka, ikimaanisha kwamba supply ya cement bado haitoshelezi mahitaji.

Supply of Cement = f(Demand from Government funded projects + Demand from Households + Demand for Export)


Kwa hiyo, tunachokishuhudia kwa sasa kwenye soko la cement ni kwamba, output ambayo inazalishwa na viwanda vya cement kwa sasa, karibu yote inaliwa na mahitaji kutoa miradi ya serikali, na kupelekea kufubaza output ambayo inatakiwa ikauzwe kwenye soko la wananchi.

Ndo mana sasa unakuta kwa sasa, ukienda viwandani wanakuambia bei bado ni zile zile hazijabbadilika za kwenye Tzs 13,500 lakina hawana supply ya kukupa maana yote ipo booked na contractors wa hii miradi ya serikali, matokeo yake Cement pungufu inayoingia kwenye soko la wananchi inagombaniwa na wananchi na ku trigger profit seeking behaviour ya wafanyabiashara ambao wanacapitalise inefficiency ya soko kwenye demand na supply ili kujinufaisha. Kiuchumi.

Serikali amekuwa akitumia nguvu kubwa ya mabavu aliyonayo, kutoa vitisho kwa wafanyabiashara kwamba wao ndo chanzo cha kupanda kwa bei ya cement, na kusahau kabisa kwamba yenyewe serikali ndio imekuwa haitimizi wajibu wake kikamilifu.

  • Haikutathmini uwezo wa uzalishaji wa cement kabla ya kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi, na
  • Ame discourage uwekezaji wa kiwanda kikubwa cha cement cha Dangote, mtu ambaye ana capital muscles za kuwekeza na kuzalisha cement nyingi walau kukidhi mahitaji yaliyopo kwa sasa na yatayojitokeza mbeleni, ukizingatia bado Magufuli anatilia mkazo sekta ya ujenzi.
Hatari nnayoiona kwa miaka miwili au mitatu ikiwa bado kutakuwa kuna crisis ya namna hii inayoendelea kwenye cement, ni kwamba watu na makampuni wataanza kununua cement nje ya nchi, kitu ambacho kitapelekea capital outflow nyingi, kitendo ambacho sio rafiki sana kwa hazina yetu ya fedha za kigeni – maana itabidi utumie reserve yako kununua cement nje, na pia inaweza ku trigger macro-economic imbalances kama kuongezeka kwa inflation na kupanda kwa dola dhidi ya shilingi, ambayo nayo itakuwa ni maumivu kwa serikali maana ita struggle ku service madeni ya nje ya nchi ya dola.

So, ni kwamba kuna mlima mkubwa sana wa kupanda kwa waziri wa ujenzi na viwanda wanaokuja, kuondoa uchafu wa serikali kwenye issue ya cement, ikwezekana, mwekezaji Dangote aitwe na serikali kwa hali ya dharura.

Ni mimi raia mkereketwa wa nchi ya chama kimoja.

N.Mushi
Umeitendea haki mada.
Waziri wa Viwanda na yule wa Ujenzi waanze na hili tatizo.
 
Umeitendea haki mada.
Waziri wa Viwanda na yule wa Ujenzi waanze na hili tatizo.
Yaah wa ujenzi itabidi arejee kufanya tathmini ya mahitaji yote ya cement kwenye miradi yote ya ujenzi ya serikali halafu wa viwanda aangalie uwezo wa viwanda kuzalisha hayo mahitaji. Hii miaka miwili ijayo wasipofanya kazi zao vizuri, tunaingia kwenye crisis au kuna hatari ya hii miradi kusimama
 
Umenikumbusha mbali sana mkuu, baba yangu mkubwa alinunuaga mifuko ya cement ya kutosha akafungia ndani, sasa ile sehemu sijui ilikuwa na unyevu unyevu, zile cement karibu zote zilikuwa majabali. ... Umetoa point nzuri sana mkuu
Afu Mwandishi anakuja kutafuta habari juu ya kupanda kwa bei.
Nikammwuliza bei elekezi IPO? Ni sh. Ngapi? Hajui

Nikamwambia akaiulize serikali ilishindwaje kumruhusu Dangote auze 5000 hadi 8000 kwa 50kg kama kweli inamjali mwananchi.

Pia akaulize viwanda kama vinaendelea kuzalisha inaenda wapi. Mwezi wapili huu unaenda kukata baadhi ya waliolipia cement hawajapata
 
Sukari Na Mafuta Ya Kupikia Bei Ilipanda Serikali Ikawa Inapiga Propaganda Mwijage Anazurura
Naona Cement Nayo Inaivua Nguo Serikali
Wanasema Ipo Lakini Haionekani Wakuu Wanahaha
Wafanyabiashara Wamekaza Tu 🤨😑😏😐
 
Afu Mwandishi anakuja kutafuta habari juu ya kupanda kwa bei.
Nikammwuliza bei elekezi IPO? Ni sh. Ngapi? Hajui

Nikamwambia akaiulize serikali ilishindwaje kumruhusu Dangote auze 5000 hadi 8000 kwa 50kg kama kweli inamjali mwananchi.

Pia akaulize viwanda kama vinaendelea kuzalisha inaenda wapi. Mwezi wapili huu unaenda kukata baadhi ya waliolipia cement hawajapata
Hii issue ni crisis kubwa kuliko inavoonekana. Inaonekana kama simple hivi.. ila ni issie nzito
 
Darasa/Ushauri wa bureee

Namna bora ya kudhibiti upandaji holela wa bidhaa unaofanywa na watu binafsi ni serikali nayo kujihusisha katika biashara (lakini kwa kiwango kidogo) ili ikitokea wafanya biashara binafsi wamepandisha bei kwa tamaa ya kujipatia faida kubwa 'super normal profit' yenyewe serikali inabaki kuuza kwa bei halali, serikali ikifanya hivyo wateja watakimbilia kwa serikali, wafanya biashara binafsi watajikuta wakipungukiwa na wateja, baada ya wafanyabiashara binafsi kukumbwa na kupungukiwa na wateja hurudi wenyewe kwenye bei halali

Copy to:
Waziri mteule wa Fedha & Biashara Dr. Philip Isdor Mpango

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda, Biashara & Masoko atakayeteuliwa
Mkuu ishu ni upungufu katika uzalishaji na sio usambazaji. Hata serikali ikiingi haitasaidia tatizo
 
Umechambua vizuri sana, labda niongezee kidogo, hapa swali la kujiuliza ni kwanini huo upungufu umekuja wakati huu?

Wakati ule sukari imeadimika tuliambiwa wafanyabiashara walikuwa wanaificha , kwasababu wao walikuwa wananunua kwa bei kubwa ya jumla, halafu wao wakawa wanalazimishwa kuiuza kwa bei elekezi ambayo ilikuwa ya chini.

Jana niliona taarifa mkuu wa Mkoa wa Dsm nae akitangaza bei elekezi ya mfuko mmoja wa saruji ni 15,000/= hapa tujiulize, je, hiyo bei inamlipa mfanyabiashara wa rejareja?

Kosa la msingi nionavyo ni kwa serikali kutokudhibiti bei za bidhaa kuanzia viwandani, wanaponunua kwa jumla mpaka kwa wale wafanyabiashara wa chini (rejareja) hili ndio kosa linalosababisha scarcity ya bidhaa sokoni, kwasababu huwezi kunipangia bei ya kuuza wakati mimi nimenunua kwa bei kubwa.

Pamoja na tatizo la baadhi ya viwanda kusimamisha uzalishaji, serikali lazima ijifunze kukaa chini na hawa wafanyabiashara wakubaliane bei, ili kutomuumiza mtumiaji wa mwisho, lakini pia, kutowaumiza wafanyabiashara wenyewe, kama ikilazimu, wapunguziwe hata kodi ili kufidia hasara wanayoweza kuipata kwa kuuza cement yao kwa bei ya chini ili kumkomboa mtumiaji wa kawaida.

Serekali ya CCM ipunguze kodi? Upo Sirius mkuu?

Hawa watu hawajawahi kabisa kumjali mwananchi wala mfanyabiashara. Zaidi ya kujijali wao tu.
 
Hahahaha.. mkuu wa mkoa hawa wapo kutetea ugali wao tu, bei haiwezi kuwa stabilized na matamko. Bei inakuwa stabilised kwa ku adjust supply dynamics. Yaani ili uweze kutuliza bei ya cement ni lazima kuwe na uhakika wa supply ya cement ya kutosha, cement ikipatikana kila mahali, we unadhani ni mafanyabiashara gani huyo atakubali kuuza kwa bei kubwa ili apoteze wateja??...
Short term measure, waruhusu cement ya nje kuuzwa nchini.

Angalizo
Miradi yote mikubwa ya ujenzi wawe na mikataba (inayofahamika bayana na serikali) na viwanda vyetu vya ndani

Gap, lifidiwe na import kuhudumia "household sectror"
Hii itasaidia "win win" kwa viwanda vyetu vya ndani na walaji binafsi.

Hilo la kuyumba kwa shilingi, watumie sera za kifedha na mikataba ya ushirikiano na wenzetu wenye surplus cement ikiwezekana within EA

Hatua za muda mrefu, waongeze uwezo wa ndani wa uzalishaji kwa kupanua/kufungua viwanda
 
Yaa ni kweli ndo mana umeona 2019 uzalishaji ulipanda kwa 44%. Lakini kwa issue ya wafanyabishara ku 'speculate' kwa kununua stock ya cement, tutarudi pale pale kwamba msukumo wa wewe kama mfanyabiashara ku speculate ni pale unapoona kwamba kuna uhaba, of which hiyo mtu yoyote atafanya kwa sababu binadamu wote tabia yetu ni selfishness.

Lakini nazidi kusisitiza, speculation yoyote haiwezi kufanikiwa kwenye efficiency, nikimaanisha kama unaviwanda vya kutosha na uzalishaji upo stable na unatosheleza mahitaji, hakuna mfanyabiashara hata mmoja atajisumbua kuficha stock, sijui kama umenipata hapo mkuu.
Kabisa mkuu...


Pia ili kudhibiti speculation kwa bidhaa nyeti kama hizo. Serikali inaweza kuweka kanuni kama kuzuia Ajenti mmoja kuwa na mzigo unaozidi mfano asilimia 20 ya usambazaji/mahitaji ya mkoa fulani.

Hii itasaidia hao wenye tamaa kushindwa kumiliki soko
 
Umechambua vizuri sana, labda niongezee kidogo, hapa swali la kujiuliza ni kwanini huo upungufu umekuja wakati huu?

Wakati ule sukari imeadimika tuliambiwa wafanyabiashara walikuwa wanaificha , kwasababu wao walikuwa wananunua kwa bei kubwa ya jumla, halafu wao wakawa wanalazimishwa kuiuza kwa bei elekezi ambayo ilikuwa ya chini.

Jana niliona taarifa mkuu wa Mkoa wa Dsm nae akitangaza bei elekezi ya mfuko mmoja wa saruji ni 15,000/= hapa tujiulize, je, hiyo bei inamlipa mfanyabiashara wa rejareja?

Kosa la msingi nionavyo ni kwa serikali kutokudhibiti bei za bidhaa kuanzia viwandani, wanaponunua kwa jumla mpaka kwa wale wafanyabiashara wa chini (rejareja) hili ndio kosa linalosababisha scarcity ya bidhaa sokoni, kwasababu huwezi kunipangia bei ya kuuza wakati mimi nimenunua kwa bei kubwa.

Pamoja na tatizo la baadhi ya viwanda kusimamisha uzalishaji, serikali lazima ijifunze kukaa chini na hawa wafanyabiashara wakubaliane bei, ili kutomuumiza mtumiaji wa mwisho, lakini pia, kutowaumiza wafanyabiashara wenyewe, kama ikilazimu, wapunguziwe hata kodi ili kufidia hasara wanayoweza kuipata kwa kuuza cement yao kwa bei ya chini ili kumkomboa mtumiaji wa kawaida.
Niko pamoja na wewe mkuu!

Kumbe ukiacha U Lisu huwa unakuwa na akili

Jokes tu mkuu
 
Short term measure, waruhusu cement ya nje kuuzwa nchini.

Angalizo
Miradi yote mikubwa ya ujenzi wawe na mikataba (inayofahamika bayana na serikali) na viwanda vyetu vya ndani

Gap, lifidiwe na import kuhudumia "household sectror"
Hii itasaidia "win win" kwa viwanda vyetu vya ndani na walaji binafsi.

Hilo la kuyumba kwa shilingi, watumie sera za kifedha na mikataba ya ushirikiano na wenzetu wenye surplus cement ikiwezekana within EA

Hatua za muda mrefu, waongeze uwezo wa ndani wa uzalishaji kwa kupanua/kufungua viwanda
Umeshauri vizur mkuu, uchawi upo kwenye utekelezaji
 
Back
Top Bottom