Serikali haina taarifa za shule kufungwa

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,832
2,790
na Lucy Ngowi



SERIKALI imesema kuwa haina uhakika kama wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika Manispaa ya Tabora, wamerudishwa nyumbani baada ya shule kufungwa kutokana na wazabuni kusitisha huduma ya chakula katika shule zao.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza, alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake mwishoni mwa wiki iliyopita, juu ya hatima ya wazabuni waliositisha kutoa huduma ya chakula katika shule za sekondari za serikali pamoja na vyuo vya walimu.

“Sina hakika kama wanafunzi wako nyumbani, sina hakika na hilo kwa kuwa sijapata taarifa ya kiofisi mezani kwangu,” alisema Mahiza.

Kwa maelezo ya naibu waziri huyo, hatima ya wazabuni hao itajulikana baada ya hazina kutoa pesa hizo, kwa kuwa ni haki yao kulipwa.

Alikiri kuwa, wazabuni hao wanaidai serikali sh bilioni tisa na kuongeza kuwa ni wajibu wa serikali kulipa pesa hizo.

Hivi karibuni iliripotiwa kuwa, shule za Manispaa ya Tabora zilifungwa kutokana na wazabuni kusitisha huduma ya chakula, kwa kuwa hawajalipwa madeni yao na serikali kwa muda mrefu.

Baadhi ya wanafunzi walilalamikia kitendo hicho kwa kusema kuwa, kitawaathiri katika mitihani yao waliyokuwa wanatarajia kuifanya siku za karibuni.

Shule hizo ni Kazima, Milambo, Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora na Shule ya Sekondari ya Wasichana Tabora.

Hata hivyo, mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari ya Bwiru iliyoko Mwanza, Elia Kisuu, aliwaondoa hofu wazazi ambao watoto wao wanasoma katika shule hiyo, kwa kuwaeleza kuwa, shule yake haina tatizo la chakula na wala haijafungwa.

Bwiru ni moja ya shule ambazo wanafunzi waliozungumza na gazeti hili waliitaja kuwa imefungwa.

Wakati mkuu huyo wa Sekondari ya Bwiru, akitoa kauli hiyo, kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa, akihojiwa na Idhaa ya Kiwahili ya BBC, alikiri kuwa hali ni mbaya kwa shule hizo za Mkoa wa Tabora, kwani wazabuni wamesitisha huduma katika shule hizo na kusababisha shule hizo kufungwa.

Taarifa kama hii ukisoma unaelewa kabisa kwamba baadhi ya Mawaziri hawapo "duniani" hivi hata vyombo vya habari tu hawasomi, kama waziri mwenye mamlaka kwanini asichukue simu akapiga kuwasiliana na shule husika ili kuchukua hatua "eti anasubiri taarifa zije ofisini" Hiyo ndiyo ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya? Najihisi bado tupo enzi ya "Mfagio wa Chuma"
 
Kuna waziri anajua faida za media na umuhimu wake....
Ila nakuambia most ya meza za mawaziri kumejaa magazeti ya UDAKU na siyo hard news... Wao wanajiona ndio news yenyewe hivyo wala haiwahangaishi kusaka news ila udaku ndiyo haswaa wanachangamkia as news.....

Ushahidi wa hilo ni kutokana na kauli namatendo yao.
 
hivi ni bajeti zinazopangwa huwa hazikidhi mahitaji ?? au ndio zinaingia kwenye mifuko ya mafisadi?
au wanataka kurudisha yale mambo ya miaka ya nyuma shule zijitegemee kwa vyakula nk ,kuna baadhi ya shule kwa kipindi cha zamani waliziita shule za kilimo walikuwa wanalima chakula chao wenyewe na ilikuwa kazi kweli kweli!huu uzao wa leo kweli wataweza?
 
Jana nilikuwa wizara fulani, sitaitaja maana nimeliona hili wizara nyingine pia. Computer ya afisa mmoja ilikuwa ina-play music video na bila aibu ameiegesha kila anayeingia hapo anaona - kana kwamba ni kitu cha kawaida kabisa. Mbele yake wamekaa watu wengine (nadhani ni wafanyakazi wa pale wizarani) wakijadili jambo na mwingine anasoma gazeti. Hiyo ilikuwa majira ya saa tano na nusu.


.
 
Niliarifiwa kwamba Mzumbe sekondari wangefunga shule jana baada ya wazabuni wa chakula kugoma.

Wakuu wa mashule wameshapata tabu sana kuhusu hili swala.



.
 
Wizara ya Kilimo hapa Dar imekatiwa umeme maana wanadaiwa.

Kuna swala la mishahara. Kuna thread humu inayozungumzia wafanyakazi wa serikali ambao hawajalipwa mishahara kwa miezi kadhaa?
Hii shida imekuwepo hapo nyuma lakini inadaiwa kipindi hiki cha Kikwete hali inastaajabisha.
Sio tu wale wa ngazi za chini wanaoathirika.

Do you know anybody who is selling a rifle?
I prefer a snipper's rifle please.



.
 
Jana nilikuwa wizara fulani, sitaitaja maana nimeliona hili wizara nyingine pia. Computer ya afisa mmoja ilikuwa ina-play music video na bila aibu ameiegesha kila anayeingia hapo anaona - kana kwamba ni kitu cha kawaida kabisa. Mbele yake wamekaa watu wengine (nadhani ni wafanyakazi wa pale wizarani) wakijadili jambo na mwingine anasoma gazeti. Hiyo ilikuwa majira ya saa tano na nusu.


.

hii ninaikubali kwani niliwahi kutembelea idara fulani kikazi muda wa saa tano ahsubui nikakuta ofice zoooote zipo empty kwani wadau wameenda kunywa chai (halafu lunch ni saa sita mchana hapo)... Shame shame shame of shame
 
....Wizara ya Kilimo hapa Dar imekatiwa umeme maana wanadaiwa..............
[/COLOR]

Duh eheeee hiii ndo karne ya 21...
Ina maana hela ya bajeti imeisha mapema.
Halafu hapo ole wao gari ya mheshimiwa iishiwe mafuta watatafutana..
 
Back
Top Bottom