Serikali haina shamba; Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete walisaidia kwenye njaa, walikuwa na shamba?

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Najiuliza sipati jibu

Hao wazee waliwahi kuongoza nchi hii kipindi cha Nyuma.

Yaliwahi kutokea matatizo ya njaa,nakumbuka niliwahi kula buruga na ugali wa njano,hawa walikuwa na mashamba ya kutusaidia wakati wa njaa?

Kwa hiyo tumeachwa tufe?

Hivi chakula ni cha bure au zile kodi zetu ndizo zinanunua?

Serikali haina shamba?hebu rudia tena?
 
Najiuliza sipati jibu

Hao wazee waliwahi kuongoza nchi hii kipindi cha Nyumba.

Yaliwahi kutokea matatizo ya njaa,nakumbuka niliwahi kula buruga na ugali wa njano,hawa walikuwa na mashamba ya kutusaidia wakati wa njaa?

Kwa hiyo tumeachwa tufe?

Hivi chakula ni cha bure au zile kodi zetu ndizo zinanunua?

Serikali haina shamba?hebu rudia tena?

Acha kulia lia wewe.
 
Hapo ni sawa na baba kukimbia familia kipindi cha matatizo raisi ni kama baba wa familia sasa baba anapo onesha kushindwa mapema hivyo sijui watoto watakuaje
 
Mzee bure kati yetu na yeye ni nani?

Unajua mwalimu wa shule ya msingi analipia kodi ya mshahara,ya Nyumba,anajinunulia nyanya,nguo,na kila kitu.

Kati ya mwalimu na yeye nani mzee bure?

'Bora nichukiwe na watu wote lakini Ninyooshe Nchi'- JPM
 
Hapa kazi tu! Hakuna vya bure wala maneno matamu. Hakuna njaa. Wafanya biashara wamewapa chochote ili mseme kuna njaa wapewe vibali vya kuleta chakula toka nje! Hakuna njaa.

Babu yangu aliwahi kunisimulia hadithi ya ndama ambaye alikuwa anachukia kuonekana kuwa ana pembe. Akaenda akanunua kilemba na akajifunga kichwani na kuwa na amani kwa kuwa hataonekana kuwa ana mapembe. Baba wa ndama yule akamwambia, "kama una pembe au huna muda ukifika kilemba hakitakusetiri! Maana yake kuna njaa au ni janja ya mabepari, time will reveal!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom