Serikali haina pesa elimu ya Juu; Wazazi watakiwa kutafuta jinsi

A-town

JF-Expert Member
Oct 25, 2011
494
169
Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi amesema serikali haina pesa waliokosa mkopo wazazi wao watafute namna.

source: ITV kipindi dakika 45 bado anaendelea na mahojiano
 
Yes amesema kweli maana iliyopo sasa ni ya sherehe zao hizo na bado wanataka zaidi ili wajurushe ila ya kusomesha watanzania hawana .
 
Tuna serikali moja tu na kwa maana hiyo kama serikali ingepitia mafungu ya wizara na kuangalia matumizi yasiyo ya lazima hela ingepatikana. Sasa hivi kuna upuuzi unaendelea kwa kila wizara kufanya maonesho ya miaka 50 ya uhuru! Hii ni mara ya pili wanafanya hivyo kwa sababu wiki ya utumishi wa umma kwa mwaka huu ilitumika kama maonesho ya miaka 50, lakini sasa wameona bado wanataka kuendeleza porojo.

Pia kuna hii tabia ya kushona sare na kofia hata kwa shughuli ndogo. Haya ni matumizi mabaya kwa nchi ambayo inasema haina uwezo wa kusomesha wananchi wake! Miaka 50 ya uhuru vipaumbele vya serikali ya ccm ni vipi?
 
Ni kweli hata sisi vipofu tunaona serikali haina hela za kufanyia maendeleo ila za anasa inazo nyingi sana,NYAMBAFU.
 
sikuona kawambwa kama kaongea professionally leo itv. He looks not confident at all. arudi udom aone utawala ulivyo mchovu na uzembe wa hali ya juu.
 
Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi amesema serikali haina pesa waliokosa mkopo wazazi wao watafute namna.

source: ITV kipindi dakika 45 bado anaendelea na mahojiano
Mnapiga kura kama vipofu, halafu mnalalama kama vichaa!
 
Kamwe hawawezi kuwaruhusu watanganyike waelimike kwa kasi hii. Ikumbukwe kua mtaji mkubwa wa magamba ccm ni ujinga wa watanganyika. Wasomi wengi wana chambua mbivu na mbichi na mbaya zaidi asilimia kubwa ya wanazuoni wanataka mabadiliko. Fine hawana pesa za kusomesha ila pesa za pombe na zinaa kuwahonga malaya zao pamoja na kusafiri dunia nzima na kulipana mishahara na marupurupu makubwa wanazo. Hawa kupe tusipoangalia wata tunyonya dam mpaka tufe. Tuwakatae tuwapinge na tupambane kudai uhuru wa kweli
 
kasema eti museveni anashangaa wanafunzi kupewa mikopo kawabwa bwana ,,,,,,,sijui mwaka jao atapewa wizara gani? maana ameshapita wzra nyingi kipindi cha mwanzo cha jk
 
Ni kweli hata sisi vipofu tunaona serikali haina hela za kufanyia maendeleo ila za anasa inazo nyingi sana,NYAMBAFU.

Hapa alikuwa anafikisha ujumbe kuwa Pesa za kusomesha watoto wa watanzania hazipo ila za kuwalipa DOWANS zipo tena kwa wingi tu! Huyu Kawa mbwa wa kung'ata mpaka watoto wa wanayemfuga!
 
Mh waziri kazungumza jana na niliridhika kwa maelezo ya kina ambayo aliyatoa. Ni kweli serikali inatumia pesa nyingi kutusomesha, tofauti na mataifa mengine. Pia bajeti ya mikopo imeongezwa, ni jitihada za wazi kuhakikisha vijana tunasoma. Nadhani nia ya serikali ni nzuri, uwezo ndo mdogo. Nashauri waziri apitie utaratibu wa kutoa mikopo upya uweze kuwabana wenye uwezo kupata mikopo tena kwa asilimia mia. Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu, nimeshuhudia dosari hiyo. Wenye uwezo kwao ndio wanaopatiwa 100% na watoto wa wanyonge wanakosa au kupata mgao kidogo.
 
Huo ni uwongo wa wazi kwamba serikali haina hela...uwongo uwongo!!
 
Mh waziri kazungumza jana na niliridhika kwa maelezo ya kina ambayo aliyatoa. Ni kweli serikali inatumia pesa nyingi kutusomesha, tofauti na mataifa mengine. Pia bajeti ya mikopo imeongezwa, ni jitihada za wazi kuhakikisha vijana tunasoma. Nadhani nia ya serikali ni nzuri, uwezo ndo mdogo. Nashauri waziri apitie utaratibu wa kutoa mikopo upya uweze kuwabana wenye uwezo kupata mikopo tena kwa asilimia mia. Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu, nimeshuhudia dosari hiyo. Wenye uwezo kwao ndio wanaopatiwa 100% na watoto wa wanyonge wanakosa au kupata mgao kidogo.

Umechukua hatua gani katika hili la wenye uwezo ndo wanapewa wasio na uwezo hawapewi. Kwa mfano mke wa RZ1 kapewa mkopo halafu masikini wanakosa! Pia mmeshafatilia pale bodi ya mikopo kunasemekana pale ukitoa rushwa unapata mkopo wala siyo issue maana wafanyakazi wa bodi ndiyo deals zao.
 
nimemwandikia waziri husika barua. Natumaini ni msikivu ataifanyia kazi
 
Tuna serikali moja tu na kwa maana hiyo kama serikali ingepitia mafungu ya wizara na kuangalia matumizi yasiyo ya lazima hela ingepatikana. Sasa hivi kuna upuuzi unaendelea kwa kila wizara kufanya maonesho ya miaka 50 ya uhuru! Hii ni mara ya pili wanafanya hivyo kwa sababu wiki ya utumishi wa umma kwa mwaka huu ilitumika kama maonesho ya miaka 50, lakini sasa wameona bado wanataka kuendeleza porojo.

Pia kuna hii tabia ya kushona sare na kofia hata kwa shughuli ndogo. Haya ni matumizi mabaya kwa nchi ambayo inasema haina uwezo wa kusomesha wananchi wake! Miaka 50 ya uhuru vipaumbele vya serikali ya ccm ni vipi?

Vipaumbele vya ccm ni kuletea UJINGA, UMASKINI na MARADHI
 
Pesa wameach katika madini yetu. Wameuza kwa asilimia 3%. sasa wanasema nini? Kwakweli saa imefika. Kama Nyerere angekuwa na roho mbaya kama hawa sijui kama wangesoma.
 
Yakulaumiwa ni loans board,hzo pesa zinazotolewa na serikali ni nying sana endapo kungekua na equal distribution,lakn kwa kuwa heslb ipo kwa ajili ya kuwaridhsha akina Riz1 ndo maana wengne hasa maskini wanakosa.
 
nafikiri mh. waziri kawambwa yupo sahihi; muda wa bure sasa umekwisha, wazazi lazima wachangie; mbona harusi na sherehe nyingine zisizo na tija mnachangia? ila elimu kazi ya serikali peke yake! mbona hamnazo nyie!!!
 
we nae acha ungese,kwan hao wanafunz wote wangepewa let say 70% wote,ungeckia malalamiko tena?watu wanalalamika iweje wengne hasa watoto wa wenye uwezo wapewe 100% halafu watoto wa maskini wanyimwe!
 
Back
Top Bottom