Serikali haina kumbukumbu? Si walisema umeme wa gesi ndo suluhu au gesi haitoshi au sio yetu?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,873
Nchi ya kusadikika ni Tanzania kwa vituko hivi hatujamaliza hili linaibuka hili mipango kumi hakuna hata moja linaloisha tunaibuka na lingine.

Huyu JPM si alikuwa kwenye baraza la mawaziri la JK na walituaminisha kuwa kupatikana kwa gesi na mradi wa bomba uliogharimu zaidi ya tril 2 toka Mtwara hadi Dar kwa ajili ya gesi ya kuzalisha umeme na matumizi ya viwandani na majumbani inamaana haitekelezeki?

JPM na ccm wenzake wakatuaminisha umeme wa maji hautabiriki kwa sababu unategemea mvua na maji sio ya uhakika.

Sasa inamaana gesi yetu haitoshi kuzalisha umeme na tumejenga bomba kwa gharama kubwa kwanini? Au nayo gesi sio yetu kama makinikia ya madini?
 
Dah ila wakuu nyie mpo vizuri kwenye kupinga! Yaani kila jambo nyie mtatafuta namna ya kulitwist ili liwafaidishe. Ila ndo hivo endelea tu mangi
 
Dah ila wakuu nyie mpo vizuri kwenye kupinga! Yaani kila jambo nyie mtatafuta namna ya kulitwist ili liwafaidishe. Ila ndo hivo endelea tu mangi
Usiwe mtu wa kukariri na sio kila anayehoji ni mchaga huo ubaguzi utawatafuna. Gesi imefanya nn na mliuwa hadi watu wa mtwara kama mmeuza si mseme kila siku gesi inapanda bei na inazalishwa nchini
 
Suluhisho la uhakika ni umeme wa gas kwa sababu umeme wa gas kwa sababu mvua inyeshe au isinyeshe, umeme utazalishwa tu!!

Hata hivyo, sioni tena shamra shamra za gas zikiendelea hivi sasa!!!

Umeme wa bei nafuu ni umeme wa maji lakini huu sio wa uhakika kwa 100%.
 
Nchi ya kusadikika ni Tanzania kwa vituko hivi hatujamaliza hili linaibuka hili mipango kumi hakuna hata moja linaloisha tunaibuka na lingine.

Huyu JPM si alikuwa kwenye baraza la mawaziri la JK na walituaminisha kuwa kupatikana kwa gesi na mradi wa bomba uliogharimu zaidi ya tril 2 toka Mtwara hadi Dar kwa ajili ya gesi ya kuzalisha umeme na matumizi ya viwandani na majumbani inamaana haitekelezeki?

JPM na ccm wenzake wakatuaminisha umeme wa maji hautabiriki kwa sababu unategemea mvua na maji sio ya uhakika.

Sasa inamaana gesi yetu haitoshi kuzalisha umeme na tumejenga bomba kwa gharama kubwa kwanini? Au nayo gesi sio yetu kama makinikia ya madini?
Umeme wa maji ni rahisi kuliko gas na ni long term solution kuliko wa gas.

Kama hiyo haitoshi, kutumia umeme wa gas ni continuous higher expenses ukilinganisha na umeme wa maji.

Do not put all your eggs in one basket.
 
gesi imesaidia sana na itaendelea kusaidia, zaidi ya 60% ya umeme unaozalishwa kwa sasa unatokana na gesi, unafuatia wa maji then wa mafuta. lengo ni kuachana na umeme wa mafuta ambao ni ghari zaidi. nenda kinyerez na ubungo miradi ya umeme wa gesi inaendelea, lakini haizuii kuanzisha miradi mingine ya umeme wa maji kuanzishwa. kwa mtu mwenye akili timamu anatambua jinsi gesi ilivosaidia kupunguza uhaba wa umeme.
 
"....Governments constantly choose between telling lies and fighting wars, with the end result always being the same. One will always lead to the other...."

Anonymous
 
Kuwaamini hawa watu ni hatari kwa afya ya akili.
Kabisa

Hawatuambii kwa nini mabwawa ya mtera na kidatu yameyumba kuzalisha umeme,na je bwawa la stiglers halitayumbishwa na uhaba wa mvua

Mimi nadhani gesi ni chanzo cha uhakika kisichoathiriwa na hali ya hewa

Hizo hela za kujenga bwawa wazitumie kusambaza bomba la gesi nchi nzima na za jirani

Walituambia watasambaza gesi mpaka majumbani sambamba na mabomba ya maji
 
Tatizo la wabongo tunafuatilia sana mambo ya mitandaoni halafu hatusomi documents muhim hata moja,

Pitia website ya TANESCO utakuta documents kibao ambazo zinaelezea midadi ya uzalishaji umeme itakayojengwa mpaka 2030, utaona before 2020 TZ tunatakiwa tuwe tuzalisha 8000MW ambazo 2400 ni za gesi na 2600 ni za maji plus za kununua, upepo , na za makaa ya mawe ndo zitaleta hiyo 8000.

So wakati upanuzi wa kinyeresi 1 ukiendelea na kinyerezi 2 ukitarajiwa kukamilika early 2018 na mbia wa kinyerezi 3 ashapatikana. sasa ni wakati wa kurudi kwenye huu mradi wa mkubwa kbs wa maji ili by 2020 atleast tuwe na 5000MW
 
Kuna kitabu kimoja mwandishi simkumbuki,ila cover limeandikwa "its our time to eat"

Just Google it unakipata
 
Back
Top Bottom