Serikali haina kauli moja katika mambo mazito yanayogusa wananchi


Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Messages
11,889
Likes
137
Points
160
Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2010
11,889 137 160
Siku chache zilizopita Waziri Kombani alitoa kauli isiyounga mkono kuhusu mabadiliko ya katiba, na kujitetea kuwa serikali haina pesa za kushughulikia mabadiliko ya katiba na kwamba suala la madai ya Katiba ni ya akina Tundu Lisu.

Leo Waziri Mkuu anaelezea kuhusu uwezekano wa kuiandika upya au kufanyia mabadiliko baadhi ya vifungu vya Katiba.

Kwa maana hiyo kauli ya serikali inakinzana, na inatoa dalili ya kwamba kila kiongozi anaropoka anavyoona yeye bila kujadiliana na jopo la viongozi ambapo wangekuwa wanatoa kauli moja inayoeleweka. Katika uongozi huu utaratibu wa kila kiongozi binafsi kutoa kauli inayogusa utaifa ni udhaifu kwani mara kadhaa viongozi tofauti kila mmoja kutoa kauli kadiri ya maoni yake bila kuzingatia kauli inayoungwa mkono na wengi katika uongozi. Labda maana yake cheo ni dhamana?
 

Forum statistics

Threads 1,236,524
Members 475,191
Posts 29,260,902