Serikali haina fedha za kufanyia sherehe za Muungano lakini inanunua mashangingi 800! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali haina fedha za kufanyia sherehe za Muungano lakini inanunua mashangingi 800!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 19, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,535
  Likes Received: 81,964
  Trophy Points: 280
  Date::2/19/2009
  Serikali kutembeza bakuli sherehe za Muungano
  Tumsifu Sanga
  Mwananchi​


  SERIKALI imeamua kuomba michango kutoka taasisi na kampuni binafsi nchini kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Muungano zinazotarajiwa kufanyika Aprili 26, mwaka huu.

  Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Muungano, Muhammed Seif Khatib wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, jijini Dar es Salaam.

  Waziri Khatib alifahamisha kwamba, serikali imechukua hatua ya kuomba michango kutoka taasisi na makampuni yatakayokuwa tayari kufadhili sherehe hizo, kwa sababu hivi sasa haina fedha za kufanyia maandalizi hayo.


  Sherehe hizo ni za kutimiza miaka 45 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo husherehekewa Aprili 26, kila mwaka.

  Hii ni mara ya kwanza kwa serikali kuomba msaada huo ili kufanikisha maandalizi ya sherehe hizo, kwani mara zote imekuwa ikigharamia yenyewe.

  Alipoulizwa na waandishi wa habari iwapo kampuni au taasisi hizo hazitajitokeza kufadhili maandalizi hayo itakuwaje, alisema ana uhakika zitajitokeza.

  Waziri Khatib alisema, kampuni au taasisi itakayojitokeza kufadhili maandalizi ya sherehe hizo kwa kutoa sare, inaruhusiwa kuweka nembo yake kwa lengo la kujitangaza kibiashara.

  "Ili kufanikisha shughuli hii, sare maalumu zenye sura ya kukuza biashara kitaifa zitaandaliwa kwa washiriki na kuuzwa kwa wananchi," alisema Khatib.

  Akizungumza kuhusu sherehe hizo, alisema vijana zaidi ya 1,300 kutoka mikoa yote nchini wanatarajiwa kushiriki katika matembezi yatakayofanyika nchi nzima kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 45 ya Muungano.

  Khatib alisema, anaomba ushirikiano wa umma wa Tanzania pamoja na asasi mbalimbali za serikali na binafsi ili kufanikisha maandalizi ya sherehe hizo muhimu nchini.

  Kwa mujibu wa Waziri Khatib maandalizi ya mwaka huu yatawashirikisha vijana kutoka kila wilaya tofauti na miaka ya nyuma walipokuwa wanashirikishwa viongozi wa serikali peke yake.

  "Vijana watakaopenda kushiriki wajitokeze kwa hiari yao na si kwa kuwalazimisha, ndio maana tumesema tutashirikisha wananchi kutoka mikoa yote nchini kwa kila wilaya kutoa vijana watatu," alifahamisha Khatib.

  Alisema katika maadhimisho hayo kutakuwa na vijana wapanda baiskeli wa kujitolea wasiopungua 25 kutoka mikoani.
   
 2. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu kutokana na title ''serikari haina feza za kufanyia sherehe za muungano lakini inanunua mashangingi 800'' hapo naona wamejitahidi kidogo swala la pesa za muungano laweza kuwa si la msingi sana kuligharamia sana. Lakini mii sielewi hapa kwanini tunatumia pesa nyingi kwenye vitu ambavyo sio productive. Kama kunamtu anaweza piga hesabu ni kiasi gani Tanzania inatumia kwa mwaka kwaajiri ya sherehe mbalimbali tuzijadili maana binafsi naona kwa hali ya uchumi wetu hatupaswi kutumia pesa nyingi sana katika mambo kama hayo.

  Hata hivyo sija penda utaratibu wa serikari kuomba toka sector binafsi. Kimsingi nchi zetu zimeshindwa kusema hapana kwa baadhi ya hoja za mataifa ya magharibi kutokana na misaada tunayopokea. Jambo hili pia ndilo linaloipa CCM kigugumizi kushughurika ipasavyo na mafisadi. Natambua huu ndio mwanya wa baadhi ya sector either kuto lipa kodi vizuri au kusamehewa baadhi ya makosa katika operation zao.
   
Loading...