Serikali haiko serious kutatua matatizo ya elimu hapa nchini:

JOSE KASANO

Senior Member
Apr 23, 2013
120
93
Kila Mtanzania anajua kwamba elimu yetu kwa wakati huu iko njia panda hasa kutokana na ukweli kwamba serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi(CCM) kilichojigamba kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania kushindwa kufanya hivyo,badala yake maisha ya Watanzania yamekuwa magumu na yenye vikwazo vingi vinavyosababishwa na serikali.

Ulimwengu mzima unaiona Jamhuri ya watu wa Tanzania kamam nchi ya ajabu; maana hawajawahi kusikia mwanafunzi anahitimu elimu ya msingi ya miaka saba halafu ananchaguliwa kuingia sekondari akiwa hajui kusoma na kuandika, hawajawahi kuona serikali inatangaza matokeo ya kidato cha nne baada ya kupokea malalamiko toka kwa wananchi serikali inaamua kuyafuta matokeo na kuyachakachua ili angalau yapunguze munkali wa wananchi na kuyatangaza upya, hawajawahi kuona shule za sekondari zikiwa na mwalimu mmoja wa kuajiriwa wengine wanaokotwa mitaani, shule za sekondari hazina vitabu, shule hazina maabara, miundo mbinu ya shule zetu kwa ujumla inastaajabisha ulimwengu. WALIMU Tanzania ndio watumishi wanaoongoza kwa umaskini na kuganga njaa, mishahara ya walimu ni vichekesho vitupu, serikali imeendelea kudharau profession ya ualimu kwa kuwakandamiza na kuwanyanyasa walimu wa ngazi zote huku ikiendelea kuwalimbikizia mafungu baadhi ya watumishi wa kada zingine, mfano WABUNGE, TRA, watumshi wa afya, kilimo kimsingi hawa japo nao wanalalamika ila wao nafuu kuliko walimu.Mwalimu anapokea 200,000 (laki mbili) kwa mwezi eti ni mshahara wakati Mbongo mwingine anazipokea hizo kama posho ya kuhudhuria kikao kwa masaa! kama huu sio utani ni nini? Unategemea mwalimu anayepokea mshahara wa aina hii afanye kazi gani yenye manufaa wakati njaa inauma?

Nimefuatilia HOTUBA YA BAJETI YA KAWAMBWA kwa mwaka 2013/2014 wala haijaonesha kama kweli kuna nia ya kutatua matatizo yanayoikumba sekta ya elimu, hotuba nzima imejaa siasa ambazo haizna tija kwa Watanzania, tulitarajia tuone hotuba ikitaja kutatua tatizo sugu la kuboresha mishahara ya walimu ilingane na ya watumishi wengine serikalini kulingana na taaluma zao kama ilivyopendekezwa na Kambi ya upinzani Bungeni(Hongera Suzan Lyimo kwa hotuba nzuri maana Watanzania wameiona kuwa ndio hotuba ambayo ilipaswa kuchukuliwa na serikali na kufanyiwa utekelezaji lakini wao wanabeza tu).Tulitarajia hasa kuona HOTUBA YA KAWAMBWA IKITAJA KUMALIZA KERO ZIFUATAZO ILI KUBORESHA ELIMU KWA MOYO WA DHATI:

1. Mishahara ya walimu kulinganishwa na ya watumishi wengine kama elimu zao zilivyo mfano cheti, stashahada, shahada ya kwanza, uzamili, uzamivu na kuondoa dharau zilizopo za mtumishi wa kada nyingine mwenye elimu ya cheti kumzidi mwalimu mwenye shahada.Hili kwa kiasi kikubwa ni tatizo na ndio huwakatisha tamaa walimu kiasi cha kushindwa kutoa taaluma zao inavyopasa na matokeo yake waanaanza kufundisha kidogo darasani ili wakafundishe sana tuition(masomo ya ziada). Serikali ijifunze kwa shule za binafsi, walimu wanalipwa vizuri na ndio maana shule hizo zinafaulisha vizuri.Walimu wote wanaofundisha shule za serikali na binafsi wamesoma vyo vilevile na wakufunzi walewale ila tofauti yao ya utendaji kazi inasababishwa na mishahara inayolipwa.

2. Vitabu vya kiada vitolewe vya kutosha kwa kila shule.
3.Posho za kujikimu kwa walimu wote ila zitofautiane kulingana na mazingira.
4. Maabara zijengwe na kupewa vifaa vyote vinavyostahili kwa ajiri ya masomo ya sayansi yote.
5. Serikali ihakikishe kuwa vijana wote wanahitimu vyuo mwaka 2013 wanapangiwa vituo vya kazi mapema ili kukabiri UHABA mkubwa wa walimu uliopo nchini.Kila mwaka serikali inaajiri walimu ila wengi wao hukimbia vituo vya kazi na kwenda private kutokana na mazingira wanayokutana nayo kutokuwa rafiki.
6. Serikali ihakikishe inawapa ajira watu wenye weledi na maadili ya ualimu kusimamia elimu na sio haya masuala ya kujuana ya mtoto wa mjomba, shangazi,kaka, dada hana taaluma ama ana taaluma ya kughushi halafu ndo anapewa uofisa elimu, TSD ili kafanye nini? Nasema hivyo kwa sababau kwa sasa sekta ya elimu imejaa maofisa wenye taaluma zisizokidhi kuanzia huko kwenye Halmashauri mpaka wizarani kwenyewe.

7. Wadau wa elimu kama wazazi wapewe kipaumbele sana kutoa ushirikiano wa kutosha kufuatilia maendeleo ya watoto wao.
8.Serikali iondoe sheria kandamizi zisizo na msingi za kuwanyanyasa walimu kazini hususani wale wanaotaka kujiendeleza, wengi wao wamejikuta wakifukuzwa kazi kwa sababu ya kutafuta kuongeza taaluma zao, serikali sijui inataka walimu waendelee kuwa na UMULUGO! SIELEWI.

9.Fedha za kuendeshea shule zitolewe kwa wakati na za kutosha ili kusaidia uendeshaji wa shule kuwa rahisi.
10. Serikali ihakikishe kila shule innao umeme wa kutosha kama sio wa TANESCO basi wa SOLA ili kuzihakikishia shule kufanya kazi zake bila matatizo yoyote.

Nimewasikia baadhi ya wabunge wenye weledi usiokidhi wakiponda hotuba ya upinzani wakati kwa wananchi ilionekana kuwa ndiyo hotuba yenye mashiko.Hii tabia ya kuponda kila jambo linalofanywa na wapinzani ndilo huwafanya wananchi waendelee kuhamini kuwa wanapaswa kuweka chama kingine madarakani ili nacho angalau kiweze kuwaletea matumaini fulani hata kama ndoto zao hazitotimia lakini angalau kupunguziwa ukali wa maisha.Elimu yetu kwa zama hizi sio ufunguo wa maisha tena imekuwa ufunguo wa kuzimu.Wazazi, wanafunzi, walimu, wadau wote hawa wamekata tamaa na aina ya elimu inayotolewa na aina ya viongozi tulionao. Hivi kweli kama Waziri anatuhumiwa kughushi vyeti halafu huyohuyo ndo anapewa kuongoza wizara kama elimu(wizara mamam wa wizara zingine) tutarajie kitu gani?

Binafsi ningekuwa Philipo Mulugo NiNGEKUWA NIMEJIUZULU ZAMANI HASA KUTOKANA NA TUHUMA LUKUKI ZINAZOMKABILI; Kwanza alienda Afrika Kusini akasoma hotuba kama ya ze komedi, akaiabisha nchi huko eti Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Pemba na Zanziba, halafu muungano huo ulikuwa mwaka 1,1964! Huyu ni kiongozi gani? Amepewa tuhuma ngapi kuhusu elimu yake bila kuchukua hatua yoyote? Eti anasema wakirudia kumsema atakwenda mahakamani! Ukishaitwa mwizi wewe ni mwizi alisema Dr.Slaa hakuna jina lingine twaweza kukuita.

KAWAMBWA N MULUGO WATOKE AMA WAONDOLEWE KWENYE WIZARA HII MUHIMU ILI WAKAPELEKE UMBUMBUMBU WAO HUKO KWINGINE. Mh.Rais Kikwete Tafadhali mawziri wako hawa hawabebeki na ukiendelea kuwakumbatia adhabu utakayopewa wewe na CCM yako kutoka kwa wananchi ni kubwa mno.

RAI: TAFADHALI SERIKALI ITIMIZE YOTE YALIYOPENDEKEZWA KWENYE KAMTI YA BUNGE YA HUDUMA ZA JAMII, YA KUTOKA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI INAYOONGOZWA NA CHADEMA PAMOJA NA MAONI NA MAPENDEKEZO MBALIMBALI KAMA NILIYOAINISHA HAPA JUU.

KWA PAMOJA TUJENGE TAIFA LETU.
 
Back
Top Bottom