Serikali haijali kuhusu vitu vya kihistoria, inakuwa na maana gani Royal Tour?

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
669
Royal Tour imeonesha mbuga, mlima na bahari lakini kuna vitu vingi vya kihistoria ikiwemo mifupa ya mijusi mikubwa, unyayo wa mtu wa kale, na mambo mengine ambayo ni muhimu sana kwa tafiti sio tu kwa watalii ambapo hela ambayo tungeweza kuipata ni kubwa zaidi kuliko inayopatikana kwenye utalii.

Mwaka 2016 nilipokuwa natafiti kuhusu mambo ya kale, mzee mmoja aliyekuwa Makumbusho ya Taifa alisema wazi kuwa Nyayo ya Mtu wa kale kule Laetoli, Ngorongoro haitunzwi vizuri na inaweza kufutika na kukosa watu wakwenda kuiangalia nyayo hiyo ambayo mguu wa mwanadamu wa sasa unaweza kuingia na nafasi kubwa ya miguu mingine minne ikabaki.

Aidha, mifupa ya mijusi mikubwa (Dinosaurs) na mifupa mingine ipo uingereza na Germany kwa kuwa ilichimwa wakati wa ukoloni kwa hiyo waliochimba waliondoka navyo. Hata hivyo serikali haifanyi juhudi za makusudi kurudisha vitu hivyo muhimu kwa historia na utalii. Wenzetu Nigeria wamekomaa hadi wamerudishiwa vitu vyao vya kihistoria mwaka huu. sisi bado tumelala.

Kwa ulimwengu wa sasa, ni muhimu kutangaza mlima na bahari lakini tunashindana vipi na wengine wenye bahari na milima, mathalan Everest ni mlima mkubwa zaidi kuliko Kilimanjaro. Bahari ya Sham na bahari nyeusi zina maajabu zaidi kuliko bahari ya Hindi.

Point yangu ni kuwa, nyayo ya mtu wa kale, mifupa ya mijusi mikubwa iliyookotwa Tendaguru na Luhuhu ni kati ya vitu ambavyo vingetufanya tuwe na vitu vya kipekee au vitu ambavyo vinapatikana Tanzania tu.

1653029126813.png

Nawasilisha.
Mkoba Mfuko
 
Akili ndogo tu zinakusumbuwa, umeshaangalia documentary ya Royal tour phases zote? Hii ni phase one imezinduliwa, phase two na three umeziona?
 
Yan Aya mambo yanafikirisha Sana Bilion 7 zimetumika Lakin Kuna baadhi ya vivutio havimo kwenye iyo movie ya royal tour
 
Back
Top Bottom