Serikali haifanyi biashara hivyo inachopokea ni Ziada ( surplus) siyo Gawio ( dividend), wahasibu karibuni!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,779
141,663
Mimi siyo muhasibu lakini nafahamu kwamba gawio ni sehemu ya mapato yatokanayo katika faida ya biashara. Hivyo ili upate gawio ni lazima pawepo na faida iliyopatikana katika mwaka husika.

Ziada kwa upande mwingine ni ile bakaa inayobakia baada ya kutoa matumizi kwenye mapato ya taasisi zisizo za kibiashara. Ziada inaweza kuwepo hata kama taasisi husika haijatengeneza faida.

Naomba wahasibu na wachumi mkuje hapa mnipinge kitaaluma.

Maendeleo hayana vyama!
 
Gawio hutolewa baada ya hesabu za kampuni kukaguliwa na wakaguzi kutoa taarifa inayothibitisha kampuni husika imepata faida. Baada ya taarifa hiyo, bodi ya wakurugenzi hukas na kuamua namna faida hiyo itakavyotumika. Wanaweza wakaamua kuongeza mtaji kwa kutumia faida hiyo au kutoa gawio kwa wanahisa kulingana na his a zao
 
Sasa hiki anachodai Magufuli ni nini? Anadai gawio au pesa ya kulazimisha (extortion) ndani ya siku 60 hata kama haipo?
 
Wako sahihi.
Kuna maeneo serikali ina hisa kwenye makampuni ya kibiashara kama PUMA na ORYX. Hapa inapata gawio. Dividend.
Kwenye mashirika ya huduma kama TANAPA inapata fedha za ziada zilizobaki baada ya gharama za uendeshaji kutolewa. Surplus. Serikali wawekezaji wakuu kama TANAPA hivyo hela zote za ziada ni mali ya serikali.
Sasa kuna dhana nyingine ya kupokea fedha za huduma. Hii ni kitu kinaitwa management fee. Kwa maana hata kama shirika linapata hasara lakini lazima litenge kiasi maalumu kwenye makusanyo yao kama tozo ya kuhudumiwa na kusimamiwa na serikali. Shirika linaweza kuamua kutenga 2% ya makusanyo yao yakatunzwa kwa kuilipa serikali. Hapa ndio Magufuli amewabana hao wanaopata hasara.
Kwa kukuelemisha zaidi. Kwa makampuni ya kigeni. Hii management fee, tozo ya huduma, ndio inayotumika sana kukwepa kodi. Kampuni ya kigeni inafungua tawi tz halafu inaweka kuwa 40% ya makusano ni.management fees hivyo zinapelekwa makao makuu ya kampuni. Na hazitozwi kodi kwa sababu zinachukuliwa kama gjarama za uendeshaji hapa tz. Hivyo kila mwaka inaoata hasara. Lakini haifungwi.
 
Mimi siyo muhasibu lakini nafahamu kwamba gawio ni sehemu ya mapato yatokanayo katika faida ya biashara. Hivyo ili upate gawio ni lazima pawepo na faida iliyopatikana katika mwaka husika.

Ziada kwa upande mwingine ni ile bakaa inayobakia baada ya kutoa matumizi kwenye mapato ya taasisi zisizo za kibiashara. Ziada inaweza kuwepo hata kama taasisi husika haijatengeneza faida.

Naomba wahasibu na wachumi mkuje hapa mnipinge kitaaluma.

Maendeleo hayana vyama!
Kwanini itengwe siku maalum na irushwe mubashara??
 
Mimi siyo muhasibu lakini nafahamu kwamba gawio ni sehemu ya mapato yatokanayo katika faida ya biashara. Hivyo ili upate gawio ni lazima pawepo na faida iliyopatikana katika mwaka husika.

Ziada kwa upande mwingine ni ile bakaa inayobakia baada ya kutoa matumizi kwenye mapato ya taasisi zisizo za kibiashara. Ziada inaweza kuwepo hata kama taasisi husika haijatengeneza faida.

Naomba wahasibu na wachumi mkuje hapa mnipinge kitaaluma.

Maendeleo hayana vyama!
Aliekwambia serikali haifanyi biashara nani?
 
Nahisi kuna kitu kinaendelea huko hazina. Tuendelee kuiombea serikali isije ikaja na mkakati wa kuwaondoa watu kwenye ajira.
 
TANESCO, TTCL, NMB nk hawafanyi biashara?!
Tanesco haijawahi pata faida na haiwezi Kwa sasa ,na public utilities ,nmb gawio mbona linatolewa ? Kwa shareholders?hata ppf mfuko was jamii Crdb wanahisa nyingi wanapata gawio
 
Utuoaji wa gawio waweza kupandisha tozo kwa wateja wanaopata huduma kutoka kwa mashirika yanayotoa huduma hizo.Kwa mfano Benki yaweza kuongeza maintenance fees zawateja wao,Posta yaweza kuongeza gharama za kutunza mabox ya wateja,Bandali hivyo hivyo.Ingefaa waruhusu na wananchi wanunue hisa za Kampuni husika wakuze mitaji yao na serikali itoze kodi faida itakayopatikana kutoka kwenye HISA badala yakupata gawio kutokana surplus ya mashirika husika
 
Back
Top Bottom