Serikali haiaminiki kwa sababu Rais wa nchi kazi imemshinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali haiaminiki kwa sababu Rais wa nchi kazi imemshinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, May 29, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #FFFFFF"]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]JK akiri serikali haiaminiki
  • Afichua kisa cha kuachwa Ma-DC

  na Mwandishi wetu
  Tanzania Daima

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]RAIS Jakaya Kikwete amekiri kuwa Watanzania wengi wamekosa imani na serikali yake kwa kile alichodai kuwa kimechangiwa na utendaji mbovu wa baadhi ya watumishi.
  Kikwete ametamka hayo jana, alipokuwa akifunga semina ya mafunzo kwa wakuu wa mikoa na wilaya iliyokuwa ikifanyika mjini hapa, na kudai kuwa utendaji mbovu wa baadhi ya watendaji wa serikali yake, umewafikisha wananchi wengi kuichukia serikali ya Chama cha Mapinduzi.

  Alisema taifa limekosa maendeleo kutokana na tabia ya baadhi ya watendaji, kujihusisha na rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma na uonevu, mambo ambayo yamewakatisha tamaa wananchi.

  Aidha aliongeza kuwa tabia ya viongozi kuchelewesha maamuzi katika kutatua kero za watu, zimekuwa zikiwakasirisha wananchi na kutoboa kuwa ndizo zilizomfanya kuwaacha baadhi ya waliokuwa wakuu wa wilaya.

  Ameongeza kuwa baadhi ya wakuu hao wa wilaya, walikiuka maadili ya utumishi ikiwa ni pamoja na ulevi uliokithiri.

  Kutokana na hali hiyo, Kikwete aliwaagiza viongozi hao kufanya kazi zao kwa uangalifu, kutotumia ubabe na kuheshimu mipaka na mgawanyiko wa majukumu yao ya kila siku.

  Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amewataka viongozi na watendaji wa serikali kujiuzulu na kuwaachia vijana wasomi nafasi hizo ili waweze kutumia elimu yao kujenga taifa.

  Alisema kuwa ni wakati muafaka kwa wazee kuwapisha vijana, watumie nguvu na elimu yao, na wao wabaki pembeni wakiwa washauri katika mambo mbalimbali, badala ya kung'ang'ania madaraka hata katika umri huo mkubwa.

  Semina hiyo ilikuwa na lengo la kutoa mafunzo kwa wakuu wa mikoa na wilaya, kabla ya kuanza rasmi kazi zao, kufuatia kuteuliwa kwao na Rais Kikwete hivi karibuni.

  Alitishia kuwafukuza kazi ikiwa watajiingiza katika udalali wa kuwatafuitia watu vyeo na na kuwa mashujaa wa kuwapiga vita wabunge wanaopigana dhidi ya ubadhirifu na kuacha kujiingiza katika kampeni za kuwalinda wagombea urais na ubunge katika maeneo yao.

  Alisema kuwa tatizo la ajira hapa nchini ni ndoto kwa sababu ya kukosekana kwa viwanda vya kutosha. Aliwapiga marufuku wakuu hao kujihusisha na ugawaji wa ardhi, bali wasimamie mazingira bora ya uwekezaji, kuwa na mahusiano bora na wananchi.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Tabia ya kuchelewa kuchukua hatua za kutatua matatizo anazionyesha yeye mwenyewe! Z'bar hata kuweje hatosema kitu, anaachaga matatizo hapa anaenda zake kubembea davos and the like.

  Huko kwenye kufuga rushwa na ubadhirifu, mmh! Sijui anajisema? Haya, sasa anajua hayo ndo yanawakasirisha watwana, anachukua hatua gani beyond tabasamu?
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  Best King'asti waswahili walisema Nyani haoni...... ukiangalia matatizo chungu nzima tangu aingie madarakani amekuwa kimyaaaa kabisa na wakati mwingine kutolewa tamko eti Rais hahusiki!!!! Anawalaumu wengine kwa utendaji mbovu, ubadhirifu wakati yeye ndiye NUMERO UNO kwa hayo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...