#COVID19 Serikali: 34% ya Watanzania walengwa wa awamu ya kwanza wamepata chanjo ya UVIKO-19, sasa tunapeleka chanjo Vijijini

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,532
141,334
Msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa amesema takribani watu 345,000 sawa na 34% ya chanjo zilizokuja wameshachanja.
Msigwa amesema kazi kubwa imefanyika kuhakikisha watu hao wengi wamechanjwa na sasa kipaumbele kitakuwa vijijini ambako tunawapelekea chanjo huko huko.

Msigwa amesema chanjo zaidi ya milioni moja zilipokelewa kwa awamu ya kwanza na zikiisha zitaletwa nyingine.

Kimsingi tunaenda kuanzisha Wiki ya Chanjo ambayo itakuwa inasimamiwa na viongozi wote wa eneo husika kuhakikisha watu wengi zaidi wanahamasika na kuchanja.

Chanzo: TBC
 
Kuna mzee kijana wake alikuja Dar kutoka kijijini huko kuja kufanya kazi ya kuuza duka, zilipoingia chanjo tu Mzee kaanza kupiga simu mwanae arudishwe hakichome chanjo.
 
Mmh huku vijijin ndo watarudi na chanjo zao yaani n hawataki chanjo ,hata hzo mask na kunawa nawa hamna kabisa huku. Yaan maisha yanaendelea tu sku zote n sawa huku
 
Wakubali tu kuwa hili swala la chanjo limewapiga knockout. Haiwezekani mwaka mzima mkawaaminisha watu kuhusu nyungu, na kusemea vibaya chanjo halafu baadae mkapiga uturn mkitegemea watu watawafuata. Tayari walishawajengea watu imani mbaya kuhusu chanjo, kuwabadilisha mtazamo tena, sio jambo dogo.

Inahitajika akili ya ziada kufanikisha hili swala, bahati mbaya kwenye serikali na viongozi, hakuna mwenye uwezo huo. Wote uwezo wao wakufikiri uko low. Kwahiyo hizo chanjo zitawadodea tu.
 
Bado tu hazija-expire?

Tuliambiwa mwitikio ni mkubwa sana,imekuaje tena?
 
Msemaji wa serikali Bwana Msingwa leo ametoa taarifa kwa umma kwamba hadi kufikia jana tarehe 11.9.2021 tayari watanzania 345,000 wamepata chanjo ya Covid 19.

Bwana Msigwa ameongea kua kutokana na muitikio mkubwa wa watu kutaka chanjo, sasa mpango uliopo ni kusambaza zaidi chanjo kwenda vijijini ili watu wasifuate chanjo mbali na makazi yao.

Kwa mtazamo wangu, kwenye hili la chanjo serikali imechemka big time, leo karibia miezi 2 ama wiki 6 toka chanjo izinduliwe na Rais watu 345,000 tu ndio waliochanjwa. Kwa hesabu ni kwamba watu 57,000 ndio wanachanjwa kwa wiki sawa na watu 8,124 kwa siku.

Tukienda na hizi takwimu, chanjo 1,008,400 za J&J tulizoletewa na Marekani itachukua siku 124 ama miezi 4 kuzimaliza. Kumbuka tuna chanjo za msaada kama hizo milioni 11 za Covax zitaletwa, hizo zitahitaji zaidi ya miaka 4 kuisha kama tukiendelea na spidi hii. Tukumbuke pia kua chanjo toka imetengenezwa inakaa miezi 6 ndio inaisha muda wake ama ku-expire. Hatujajua hizi tulizoletewa zina muda gani toka zitengenezwe.

Na wataalamu wanasema ili ufikie herd immunity unatakiwa angalau uchanje 70% ya population yako, kwa Tanzania tunatakiwa kuchanja watu milioni 42 angalau. Kwa hapo tutahitaji miaka si chini ya 15 kumaliza kuchanjwa kwa spidi hii.

Hilo halitoshi bado tukimaliza kuchanjwa watu milioni 42, tutatakiwa kuanza kuwachanja tena booster ama baada ya miezi 6 toka tumeanza kuchanjwa tunatakiwa kuanza kuchanja booster, yaani chanjo mpya na booster ziende simultaneously.

Serikali kabla haiajaanza kununua chanjo nyingine kutoka kwenye mkopo iliochukua wa zaidi ya Trilioni moja, ifanye analysis ya uhakika, tusije kununua chanjo zika expire bila kutumiwa na halafu tukaachwa na deni kubwa la kulipa huku hela imeenda bure.
 
Wakubali tu kuwa hili swala la chanjo limewapiga knockout. Haiwezekani mwaka mzima mkawaaminisha watu kuhusu nyungu, na kusemea vibaya chanjo halafu baadae mkapiga uturn mkitegemea watu watawafuata. Tayari walishawajengea watu imani mbaya kuhusu chanjo, kuwabadilisha mtazamo tena, sio jambo dogo.

Inahitajika akili ya ziada kufanikisha hili swala, bahati mbaya kwenye serikali na viongozi, hakuna mwenye uwezo huo. Wote uwezo wao wakufikiri uko low. Kwahiyo hizo chanjo zitawadodea tu.
Mbaya zaidi ni kinywa kilekile kilihamasisha nyungu na mwendazake na kinywa hichohicho kinakuja na vaccine
 
Muitikio hafifu unatokana na mkanganyo kwa wananchi juu ya chanjo na hii ni matokeo ya msimamo wa awali wa Serikali kuhusu chanjo!

Tunampuuza Askofu Gwajima lakini hii ndio impact yake, watu wana ignore sana suala la chanjo na kuona kama serikali ina play game fulan hivi.

Lakini in real sense bado kuna maswali mengi sana juu ya uwepo wa COVID 19, mikusanyiko bado, no social distancing, nobody who is minding this business, no masking but nguvu kubwa ilitumika kwenye chanjo ambapo majority kama hawaelewi kipi wafanye .

Mbaya zaidi wananchi wanaona kama nguvu kubwa inatumika kuhamasisha chanjo bila kueleza Nini kilichosababisha serikali mwanzoni ku ignore chanjo.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Nina wasiwasi waliochanja hawafiki hata elfu kumi. CCM kwa kipika takwimu hawajambo. Au wamechanja na yale mapapai plus kondoo😂😂
 
Back
Top Bottom