Serikali futeni uongozi wa maabara ya kupima Covid19 kwa uzembe wa kuchelewesha majibu ya vipimo makusudi

hesabu900

Member
Apr 18, 2017
78
62
Kiukweli pale Ubungo external ilipo hii maabara kuna uzembe wa hali ya juu. Abiria wanaachwa na ndege sababu ya ucheleweshaji wa majibu ya vipimo vya Corona. Watalii, Wafanyabiashara na Wageni wanalalamika.

Huu uzembe unasababisha hasara kubwa sana. Watalii na wageni wataacha kuja Tanzania sababu ya huu uzembe. TAKUKURU fuatilieni pia kuna dalili ya rushwa. Yaani wanachelewesha majibu makusudi ili watu wajae. Na wanajua mtu akisha-panic kuachwa na ndege akiambiwa atoe chochote atatoa.

Wanasema majibu yanatumwa online, Unasubiri hakuna kitu.

Waandishi wa habari tafadhali nendeni pale mkaone mrundikano wa watu wanalia kila siku na kuachwa na ndege.

Tafadhali Serikali ingilieni kati mapema. Tutapoteza wageni na watalii.
 
Back
Top Bottom