MESHACK WARIOBA
JF-Expert Member
- Mar 29, 2017
- 1,068
- 1,167
Ndugu Mbona Umekazania Kenya, Wapi kwenye thread Yangu nimesema Kenya? Soma vizuri uniambie wapi nimezungumzia kuhusu Kenya? Mimi sifahamu Elimu ya Kenya; Sasa sijui Kenya wewe unaitolea wapi Ndugu yangu; Mimi nimesema as per experience ya huku nilipo,na nilipopita;yn mtoto wa primary kenya ana upeo kuliko mtz wa second year
Na Nilichozungumzia ni kwamba Kijana wa Key Stage 4, Ana uwezo wa Kudeliver Specific category ( Hapa nimemaanisha kwamba Wao wanaanza Specialization ya career Mapema, Between hiyo 14 and 16 years wengi wanaweza Kudeliver kitu kinachoonekana(Paana at the End of Stage four kuna Study Project(Unachagua kitu cha kufanya); Compared to Tz Mtu wa Form four hata kama atakuwa na Upeo Mkubwa wengi wanakuwa bado hawajajikita kwenye career husika (Si wote ila wengi), Huku Hiyo Key Stage four Computer wanasoma Basics Of Programming, of which kwa elimu ya Tz, hayo mambo ni Mwaka wa Pili kwa mtu wa IT na CS; Maana form 4 and 6 wanasoma tu Basic Subject, kama wakisoma Computer basi ni Office packages tu.
Hicho ndicho nilichokiona, Mimi nilipokuja Huku TAD(Technology Architecture and Design) ilikuwa inanipa shida, japo baadae nilikuja Ku-master Vizuri; Ila ni kwasababu hawa vijana wao wamesoma Basics of it tayari on their 16's(Nami Umri wangu ulikuwa umeenda by then)
Sasa Kijana wa Second Year Tz, ndio anaanza Specialization kujikita kwenye fani husika aipendayo; Wachache sana Tz wanaweza kujikita kwenye Fani aipendayo akiwa form 4 au form 6, Labda mzazi atengeneze mazingira Nyumbani, of which hiyo labda ni kwa wazazi wenye vipato vikubwa. Lakini pia lazima Ughaibuni Masomo yako ni Key Element za Skills kuliko Kukariri mambo, na huu ni Ukweli ( Kumbuka kuna Kukariri na Kuhariri)
Hivyo ndugu yangu mimi nimezungumzia kwa kona hiyo; Niwie radhi kama nimekukwaza, lakini JF ni sehemeu ya Kueleza Mtazamo, na Mtazamo wa Mtu sio Sheria.
Kinachotofautisha Mtu na Mtu ni Mtazamo alionao juu ya Kitu fulani; Kichatofautisha Mpagani ma Mkristo na Muislamu ni Perspective waliyonayo juu ya MUNGU; Kinachomtofautisha tajiri na Maskini pia ni Mtazamo; Hata Muslim kwa muslim wanaweza wakapishana mtazamo kwenye baadhi ya mambo.
Kila Mtu yuko sawa kwa kadiri ya Mtazamo na usawa wake;
Hata wewe Upo sawa kabisa kwa kadiri ya usawa na Mtazamo wako; Ijapokuwa Haukuwa na haja ya Kutoa Matusi kwa kujibu nilichosema, hiyo sio ustaarabu ndugu.