Serikali futeni elimu ya kidato cha tano na sita, haina faida

Some hii
Dunia ya leo elimu ya kidato cha 4 inatosha kumfanya kijana kusoma chuo.

Nimejaribu kukagua daftari za ndugu yangu yuko kidato cha 5, mambo wanayosoma sioni kama yana tija. Sijaona utofauti wa Mwanafunzi wa kidato cha nne na tano kitaaluma.

Vijana wengi wanapoteza muda sana kusoma kidato cha tano na sita ni vema wasome moja kwa chuo wakimaliza kidato cha nne

Au nyie mliosoma kidato cha tano na sita tuambiane imekusaidia nini? Mfano usingeenda chuo ingekunufaishaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes
Hoja yako mtoa mada INA mashiko kidogo Mimi nimiongoni mwa watu ambao nimesoma mifumo yote hiyo kupitia olevel na A level na nimesoma veta pia umeme na Nina diploma ya HRM ,hili swala kwanini halichukuliwi serious kijana kumpeleka jkt miaka miwili bora kumpeleka Veta akaosemee mechanics ,plumber n.k miaka miwili trust me hata akiamua kuendelea na chuo baadae hawazidi shindwa maisha kwa kisingizo hakuna ajira ,Alevel ni westing of time ulishawahi jiuliza wale wanao kosa sifa za ufaulu kwenda chuo kikuu wanaenda wapi ? Wanaenda college wanakutana na vijana waliomaliza a level wanaanza upya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umetoka kuvuta bange unajiona ndalichako njoo na 14 points za self-determination kwanini advance ifutwe
Nchi za Scandinavia mfano Denmark wana mfumo kama anaoelezea mtoa mada, wanafunzi wakimaliza form 4,wanakwenda University au technical college, hamna form 5 au 6..

Na ndio maana utakuta wanaohodhi Master na PhD wanakuwa bado vijana, sio huku kwetu ukimsikia mtu amehodhi PhD basi ni mzee Sana..

Naunga mkono hoja form 5 na 6 zifutwe hazina faida yoyote..
 
Utofauti wake ni nn??? Haswa unaposoma pcm vitu ni vilevle except calculus ndo as ipo A-level then izo pgm, pcb kitu gan cha tofauti, but difference ni kwamba A- level wana kuwa more advance lakin still bado, utakuta mwanafunzi kasoma pcm yeah anaenda chuo anafundishwa engineering mathematic anapata supp au karai so what's going there's nothing
We mtoa mada una matatizo binafisi
Usifananishe Adv level(PCM,PCB,PGM etc)
Na vitu vya hovyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtazamo wangu tungebadili mfumo wa elimu kuanzia chini. Watoto wasingesoma masomo kwa kiswahili. Alafu somo la kiswahili lingefutwa kabisa lisiwepo. Masomo yote yawe kwa kingereza tangu chekechea hadi chuo. Mtoto anapoteza muda hadi darasa la saba akianza form one anaanza upya kukaririshwa lugha tofauti.
Kiswahili muhimu sana mkuu,tunajivunia sana kama taifa hatuwezi kuuwa hii lugha adhimu,tutakua watumwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dunia ya leo elimu ya kidato cha 4 inatosha kumfanya kijana kusoma chuo.

Nimejaribu kukagua daftari za ndugu yangu yuko kidato cha 5, mambo wanayosoma sioni kama yana tija. Sijaona utofauti wa Mwanafunzi wa kidato cha nne na tano kitaaluma.

Vijana wengi wanapoteza muda sana kusoma kidato cha tano na sita ni vema wasome moja kwa chuo wakimaliza kidato cha nne

Au nyie mliosoma kidato cha tano na sita tuambiane imekusaidia nini? Mfano usingeenda chuo ingekunufaishaje?
Duh, maneno ya mkosaji
 
Uelewa wa mtu hauko kwenye vidato anavyosoma, Yes nilisoma advance ( PCM) Yale matopic ya coordinate 1 and 2, wave, heat, modern physcis, projection, magnetism, probability 1 and 2, set, calculus na zinginezo...zimeniongezea Nini? Ukifika chuo unakuta vijana wa FTC wako njema Sana na bado huko wamesoma physical science na baadhi ya topic za advance maths zenye umuhimu....

Elimu ya tz ni kusomea paper, mleta maada ana hoja iboreshwe elimu ya sekondari iishie form4 Kama Kenya...huko advance wangekuwa kweli kunatuongezea maarifa basi huku mtaani baada ya kumaliza chuo usingekutana na rundo la wahitimu wanaolalamika kukosa ajira
Mkuu chuo umesoma nini??
Maana umetaja topic za muhimu nyingi sana unasema hazijakusaidia kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mjinga ni wewe siyo mtoa mada,tatizo huwa mnachangia kulingana na mlivyokaririshwa. Kile kinachoongezeka kwenye masomo ya sayansi A-level wanashindwa nn kuviunganisha huku kwenye O-level na mwanafunzi ni yuleyule!??

Kwani mwanafunzi anayemaliza kidato cha nne anabadilika akienda advance!?? Muda wa miaka 4 unatosha kabisaa kuunganisha yote yaliyoko A-level. Muache kuwa mnathibitisha ujinga wenu hapa jukwaani.
Mkuu wewe ndo mjinga unachoshauri ni impossible hivi pcm ya advance matopic yote uyalete o level inawezekanaje ??

Kumbuka olevel unasoma masomo kuanzia 9 hadi 12 kwa baadhi ya shule


Yani MTU asome history, geography, civics,kiswahili English,French, divinity,na etc uongeze matopic ya a level kweli???

Mechanics tu ya alevel ni zaidi ya physics yote ya olevel kuanzia form one hadi 4


Unless unataka tufute masomo mengine kitu ambacho sidhani kama kinatija.

Mfumo ni mzuri unaoption ya kusoma high school au FTC unachagua wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama umesoma HKL sijui HGL A level haina maana kwako ulikuwa unapoteza mudaa tuu na ifutwe.. Ila kama Umesoma PCM..PCB mzee baba Bila A level speed na vitu wanayofundisha malecture chuo tungeishia kupata Zero....
👊👊👊 Kweli kabisa
 
kwani wewe unafikiri position muhimu za ajira kwenye sector ya utalii na huduma za hotel nchini zinachukuliwa na vijana wa nchi gani?.
Sasa wahudumu hoteli ndo unasema wana elimu bora kuliko sisi, hapo issue ni lugha tu hoteli kubwa nyingi zinataka MTU aliye fluent in English

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaongea usicho kijua wewe...mtu akisoma PCM Advance akifaulu ujue chuo ana wigo mpana sana kwenye kuchagua kozi ya kusoma na si lazima Awe Engineer ,ila ukishachukua diploma ya DIT ya kitu flan basi mkuu ndo ushajifunga hivyoooo....utabaki kucheza maeneo hayo hayo mkuu...
Acha uwongo bro ,,,nimesoma laboratory science and technology pale mbeya university of science and technology now nipo DIT nachukua degree ya umeme ,sema wengi wenu mnakalili sana maisha na mkiharibu f6 ndo mnatuona wa maana...huna tofauti na wazazi wanaowalazimisha watoto wasisome combination tofauti na PCB

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada hajafika Advanced au Hajasoma Science na kama angesoma Science angepata 3, 4, 6, 0 score marks. ( Ni kitu cha kawaida sana huko)
Kwa waliokwisha kukaa nje ya nchi mfano Canada & USA
Elimu yetu ipo vizuri ila kinachotakiwa baada ya Kumaliza university kama Wenzetu wanavyofanya
1. Inatakiwa Companies kutoa Job placements, job orientation, Internship, Field work kwa Fleshers. Wenzetu serikali zao inatilia sana mkazo hili swala. na Flashers wanatakiwa kulipwa some amount of money.
Mfano Japan & canada Makampuni huwachukua vijana na kuwalipa kiasi flani cha pesa+ house allowance, travelling allowance, other employee benefits. NI LAZIMA!!!!
Kuna wakati nilikwenda Japan nukakutana hoteleni ( hoteli VIP) wanachuo wakaniambia wapo intern kwenye makampuni ya petroleum & gas na wengine watapelekwa intern mpaka south Africa.
Hii inawasaidia vijana kupata uzoefu+ kujiamini katika kazi. ( hii sio kazi ya vyuo!!,)
Hawa vijana waliotoka F6 ni very intelligent & Compitent na tunawategemea wakikaa kwenye Industry within 5 yrs wanaweza kuvumbua vitu vikubwa ( R&D) tofauti ni kijana wa F4 ambae ameenda FTC kwa Division III au IV anaesifiwa kwa kufanya *Normal operation work!!!!*
Point bora kuliko zote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom