Serikali, fungeni mipaka mahindi yasisafirishwe nje hali ya mavuno sio mazuri

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,283
3,274
Wizara husika angelieni upya maamuzi yenu ya vibali vya biashara ya uuzaji wa mahindi ambayo imezidi kushamiri kutokana na njaa iliopo Somalia pamoja na Kenya.

Gunia la plastiki sita kwa hapa Kiteto Manyara kwasasa limefikia 46,000 kipindi hiki cha mavuno ukilinganisha na mwaka jana ambapo kipindi cha mavuno lilikua 20,000. Mfumuko wa bei (inflation) umesababishwa na kuongezeka kwa uhitaji kutokana na usafirishwaji nje pamoja na uhaba kwani mavuno sio mazuri mwaka huu.

Msipochukua hatua watanzania watakufa njaa kwa kuokoa maisha ya wasomali.
 
Sikubaliani na kufunga mipaka hata kidogo. Nini maana ya kulima kibiashara? Suluhu si kufunga mipaka, bali ni huyo anayefikiria kufunga mipika anunue kwa bei kubwa ili wakulima wasishawishike kuuza nje.
 
Suluhisho ni Serikali kuyanunua mahindi hayo kwa bei hiyo ambayo mkulima anaikimbilia huko aendako kuuza. Kufunga mpaka ni kukaribisha magendo na rushwa tu.
 
Wizara husika angelieni upya maamuzi yenu ya vibali vya biashara ya uuzaji wa mahindi ambayo imezidi kushamiri kutokana na njaa iliopo Somalia pamoja na Kenya.

Gunia la plastiki sita kwa hapa Kiteto Manyara kwasasa limefikia 46,000 kipindi hiki cha mavuno ukilinganisha na mwaka jana ambapo kipindi cha mavuno lilikua 20,000. Mfumuko wa bei (inflation) umesababishwa na kuongezeka kwa uhitaji kutokana na usafirishwaji nje pamoja na uhaba kwani mavuno sio mazuri mwaka huu.

Msipochukua hatua watanzania watakufa njaa kwa kuokoa maisha ya wasomali.

kenya watapigana vita...huwa njaa haiwatoki hata pakiwa na hali nzuri ya hewa.sasa this time tz nao wana njaa mtagombania.
 
...[/QUOTE]

Gharama tulizotumia kutunza mashamba yetu serikali yako itaturusdishia? wewe kauzu sana unajua gharama za mkulima?

Wewe ungekuwa mshauri mzuri kama ungesema serikali inunue mahindi ya wakulima kulingana na bei ya soko ili ihifadhi kama wanavyofanya wafanyabiashara.Hii ingewasaidia wakulima to recoup their cost of production na kupata faida
.
 
Suluhisho ni kuongeza kilimo cha mahindi kwa sababu yana soko tayari. Hii ni opportunity kwa Tz kufanya biashara na nchi za nje. Si bora hata tuitwe wakulima basi????kila kitu hatuwezi sisi????
 
Watu bado wana mawazo mgando ya mwaka 47!!!!

Hebu jiweke kwenye nafasi ya mkulima na ufikirie athari za kulazimishwa kuuza kwa bei ndogo!
 
Wizara husika angelieni upya maamuzi yenu ya vibali vya biashara ya uuzaji wa mahindi ambayo imezidi kushamiri kutokana na njaa iliopo Somalia pamoja na Kenya.

Gunia la plastiki sita kwa hapa Kiteto Manyara kwasasa limefikia 46,000 kipindi hiki cha mavuno ukilinganisha na mwaka jana ambapo kipindi cha mavuno lilikua 20,000. Mfumuko wa bei (inflation) umesababishwa na kuongezeka kwa uhitaji kutokana na usafirishwaji nje pamoja na uhaba kwani mavuno sio mazuri mwaka huu.

Msipochukua hatua watanzania watakufa njaa kwa kuokoa maisha ya wasomali.

Wakati wakulima wanainamisha mgongo kupariria SERIKALI iliwasaidia? Madawa na Ruzuku vyote vinadakiwa hewani na watu wa serikalini halafu leo kwenye kuuza uwapangie wapi wauze?
 
Chakula kipo chakutosha maghara ya kule katavi, s'wanga, mbozi na songea yamejaa mahindi na hakuna kwa kupeleka. 2nawakaribisha hao wanunuzi tuje tuwauzie yakwetu hatuna kwakupeleka
 
Chakula kipo chakutosha maghara ya kule katavi, s'wanga, mbozi na songea yamejaa mahindi na hakuna kwa kupeleka. 2nawakaribisha hao wanunuzi tuje tuwauzie yakwetu hatuna kwakupeleka

Kenya wanahitaji mahindi ya Manyara kupitia soko la Kibaigwa, Manyoni, na kilosa haya ndiyo mahindi ya kiwango, mengine huko unakosema hayana viwango kwa ni full kutumia pembejeo wakati yanayohitajika ni yanayolimwa using traditional approach.

Wakenya juzi wamelizwa shs.300million pale kibaigwa pale ndiyo yanapatikana mahindi kiwango.Hayo ya songea katavi na mbozi ni full chemical.ukisikia mipaka imefungwa ujue target ni maize from Kibaigwa market, manyara, manyoni and kilosa
 
Hayo mawazo ni ya kumwonea mkulima. Mara nyingi mkulima anaonekana ni mtu wa kuyumbishwa yumbishwa tu wakati yeye ni majsiriamali kama Barrick, Richmond, Azam na wengineo. Mkulima alivyokuwa analima aliwekeana mkataba na serikali? Kama serikali inajali sana wananchi wake ingeanzisha utaratibu wa kuwa na maghala ya chakula cha akiba kwa wingi na kununua mazao kutoka kwa wakulima kwa bei ya soko. Tena tuwashukur sana wakulima wa Tanzania kwa juhudi zao na kuweza kilisha taifa kwa kutumia nguvu mtu, utashi na uvumilivu katika mazingira duni.
 
Suluhisho ni kuongeza kilimo cha mahindi kwa sababu yana soko tayari. Hii ni opportunity kwa Tz kufanya biashara na nchi za nje. Si bora hata tuitwe wakulima basi????kila kitu hatuwezi sisi????

Hewaaa!!! umenena vema watanzania tuchangamkie fursa kama hizi.
 
.....[/QUOTE]

Si ndio maana ya soko huria?Yaani mipaka ifungwe halafu wakulima waendelee kuuza mahindi yao kwa hasara? acha demand and supply itawale soko.

Njaa ikija watakuwa na mahela mifukoni na wao watanunua chakula! Kwa mitazamo kama hii ndio maana wakulima wa Tanzania hawaondokani na umaskini uliokithiri.

Ukiwakataza wasiuze mahindi yao nje, ndo yale yale mnasema serikali ndio iuze mahindi nje.
 
Umenikera saaaaaana,huu upuuzi umeutoa wapi.Jaribu kilimo onev year uone ss wakulima tunavyopata shida
 
Back
Top Bottom