Tetesi: Serikali fanyeni tafiti kwenye samaki na mazao ya shamba ongezeko la wagonjwa wa saratani(cancer) kanda ya ziwa

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
11,291
17,736
Ninahisi matumizi holela ya kemikali kama zebaki na nyinginezo zile za kusafishia madini migodini au zinazo tumiwa na wachimbaji wadogo wadogo wa madini, inawezekana hizo ndiyo huchafua mazingira mashambani, mitoni na ziwani.

Ningeshauri serikali ifanyie tafiti juu ya samaki toka ziwa Victoria, mito yote kanda hiyo unaweza kukuta jambo la kushitua.

Tafiti iende mbali na kuchunguza pia mazao toka mashambani mikoa yote ya kanda ya ziwa.

Kama chanzo kinaweza kuwa hicho nilichohisi basi tatizo linaweza kusambaa miji mikubwa kama Dar es Salaam, Dodoma, na mikoa mingine wanayo tumia samaki toka ziwa Victoria kama Sato, Sangara na Dagaa.

Sio vibaya wakichunguza na dawa za mifugo pia.

Serikali ichukue hatua tusisubiri janga kubwa.

Angalizo: Sijasema samaki wa ziwa Victoria wana tatizo.

Bandiko hili limechochewa na hoja hiyo hapo chini kama alivyochangia mjadala flani ndugu Subisubi humu jukwaani JamiiForums.
Hapo kwenye kansa inabidi watu wa mwanza washauriwe kutumia,maana idadi ya watu wanaopata kansa kutoka kanda ya ziwa inazidi kuongezeka.

CC: Mh. Rais John Pombe Magufuli, Makamu wa Raisi Bi SSS, Waziri Mkuu MKM, Waziri wa Afya, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Uvuvi,..., .., NEMC, .. et al.

UPDATES:
Kuna baadhi ya hoja za kisiasa kama hiyo hapo chini tuziepuke zitatupotosha

kwa wasukuma huko
Tukianza kulipa sura ya ukabila au ukanda jambo hili tutakosea sana.

  • Sisi wengine wa kanda mbali mbali tunakula samaki wanaotoka maeneo ya kanda ya ziwa.
  • Madukani tunanunua mchele toka mkoa wa Shinyanga kama ule mchele wa Kahama.
  • Tunakula ndizi toka kanda ziwa kama zile za Bukoba.
  • Tunakula nyama ya ng'ombe toka kanda hiyo.
  • Tunakula viazi vitamu toka kanda hiyo.
  • Tunatumia asali toka kanda hiyo.
  • Tuna ndugu zetu wanafanya kazi na kusoma kanda hiyo.
  • Tuna ndugu zetu wanaishi na kufanya biashara kanda hiyo.
  • Chakula cha kuku kinawekwa dagaa wanaotoka kanda hiyo, na baadae sisi tunakula hao kuku au mayai yao, kama unajua ABC za sayansi basi utajua hatupo salama wote tuliopo ktk huo mnyororo wa chakula(food chain).

Ubaguzi na siasa zitatumaliza ...

Walaji wa mchemsho wa samaki(sato) hapa DSM na mikoa mingine wengi ni wa kabila tofauti na wasukuma.
 
Niombee Tu nikianza M.ScPH nitachukua hii tittle, though Dunia inakuwa Na mtindo WA maisha hubadilika. Bahari pia ziwa Ni large bodies kana kwamba uchavuzi wake siyo rahisi kihhivyo.
 
Serikali ipi kiongozi? Serikali unayoitaka ifanye utafiti imechoka kuliko mbwa koko.. yaani haijielewi.. samahani kwa maneno ikiwa yatawaudhi wafia chama na serikali aka sychophants
1. Serikali ina ile tume ya mazingira aka NEMC
Hakuna taasisi hopeless, incompetent and bogus kama hii NEMC.
Kwanza haina stadards za viwango vya chini vya uchafuzi vinavyotakiwa katika mazingira, bidhaa na vyakula.. yaani wapo wapo tu.. sijui walisomea nini au huwa wanaajiriwa kivipi..
Kanda ya ziwa ina migodi mikubwa ya dhahabu ipatayo sita na mamia ya vimigodi vidogo katika eneo hilo. Kijiografia, ziwa Nyanza ni kama beseni kubwa, nalo linapokea taka taka nyingi kutoka maeneo yalilolizunguka.. ikiwemo kutoka katika migodi hii.
Tulitegemea watu wa NEMC kila mwaka au miwili, wachapishe kiwango cha uchafuzi katika ziwa, hasa kwa vichafuzi vikuu mfano Mercury, Cyanide, DDT, lead.. nk
Hilo halifanyiki na hakuna wa kuwajibishwa. Hilo linatakiwa kufanyika katika maeneo mengi hapa nchini na si kwa ziwa Nyanza peke yake.
2. Pale VPO ambako NEMC ipo, jamaa wako bize na mambo ya mabadiliko ya tabia nchi aka climate change, kwa sababu kuna pesa nyingi zinatolewa na wafadhili. Kitengo cha mazingira kwa kiwango kikubwa wako bize na safari ziso na tija huku wakiacha wananchi wakiteseka na uchafuzi wa mazingira.
3. Maeneo mengi ya mijini ambako wananchi maskini wanajitafutia rizki zao yamechafuliwa kupindukia, kuanzia vimelea hatari hadi madini hatari. Nenda sehemu kama Morogoro au Dar mabondeni ambako kuna maji na wananchi huyatumia hayo kulima mboga mboga na kuwauzia maskini wenzao.. hayo maeneo ni hatari sana, yamejaa sumu za kila aina na vimelea vya kila aina.. lakini. Na watu wengi sana wanaumwa na wanakufa kutokana na mdhara hayo, NEMC wapo tu, hata kufanya utafiti na kuuchapisha ili watu waelewe ni shida, hakuna anayejali.
4. Katika mazao mengi ya nafaka hususan mahindi, wakulima hutumia sumu nyingi tena kali katika kuhifadhi nafaka hizi. Tena kuna tetesi kuwa kuna sehemu fulani watu walikuwa wakihifadhi nafaka hizi kwa kutumia madini ya uranium ( haya ni madini yatokezayo mionzi hatari).. NEMC wapo tu.. yaani hata hawana habari. Watz wanauguwa magonjwa ya ajabu, vyanzo havijulikani.. NEMC hawafanyi utafiti, na ikitokea mtafiti akafanya utafiti na kugundua taarifa za kutisha, tayari.. lazima atiwe msuko suko.
Kwa kumalizia, serikali haina nia wala mbinu za kupambana na uchafuzi wa mazingira.

Wako bize wanakimbiza pesa z UNEP na GEF wafanye matrip huko Norway na Sweden.. Watz tujijuwe tu
 
kwa wasukuma huko
Tukianza kulipa sura ya ukabila au ukanda jambo hili tutakosea sana.
  • Sisi wengine wa kanda mbali mbali tunakula samaki wanaotoka maeneo ya kanda ya ziwa.
  • Madukani tunanunua mchele toka mkoa wa Shinyanga kama ule mchele wa Kahama.
  • Tunakula ndizi toka kanda ziwa kama zile za Bukoba.
  • Tunakula nyama ya ng'ombe toka kanda hiyo.
  • Tunakula viazi vitamu toka kanda hiyo.
  • Tunatumia asali toka kanda hiyo.
  • Tuna ndugu zetu wanafanya kazi na kusoma kanda hiyo.
  • Tuna ndugu zetu wanaishi na kufanya biashara kanda hiyo.
  • Chakula cha kuku kinawekwa dagaa wanaotoka kanda hiyo, na baadae sisi tunakula hao kuku au mayai yao, kama unajua ABC za sayansi basi utajua hatupo salama wote tuliopo ktk huo mnyororo wa chakula(food chain).

Ubaguzi na siasa zitatumaliza ...

Walaji wa mchemsho wa samaki(sato) hapa DSM na mikoa mingine wengi ni wa kabila tofauti na wasukuma.
 
Tukianza kulipa sura ya ukabila au ukanda jambo hili tutakosea sana.
  • Sisi wengine wa kanda mbali mbali tunakula samaki wanaotoka maeneo ya kanda ya ziwa.
  • Madukani tunanunua mchele toka mkoa wa Shinyanga kama ule mchele wa Kahama.
  • Tunakula ndizi toka kanda ziwa kama zile za Bukoba.
  • Tunakula nyama ya ng'ombe toka kanda hiyo.
  • Tunakula viazi vitamu toka kanda hiyo.
  • Tunatumia asali toka kanda hiyo.
  • Tuna ndugu zetu wanafanya kazi na kusoma kanda hiyo.
  • Tuna ndugu zetu wanaishi na kufanya biashara kanda hiyo.
  • Chakula cha kuku kinawekwa dagaa wanaotoka kanda hiyo, na baadae sisi tunakula hao kuku au mayai yao, kama unajua ABC za sayansi basi utajua hatupo salama wote tuliopo ktk huo mnyororo wa chakula(food chain).
Ubaguzi na siasa zitatumaliza ...
Walaji wa mchemsho wa samaki(sato) hapa DSM na mikoa mingine wengi ni wa kabila tofauti na wasukuma.
Gazeti lote hili umenijibu mimi au!
 
Ningeshauri serikali ifanyie tafiti juu ya samaki toka ziwa Victoria, mito yote kanda hiyo unaweza kukuta jambo la kushitua.

Kuna waziri aliulizwa kwanini shirika letu linarusha ndege wakati ni mbovu, akajibu sababu ni kutaka shirika lisife, hata hapa wanaweza kuona kweli tatizo lipo huko ulikosema lakini watapindisha majibu ili kutoathiri biashara ya samaki huku tukiteketea
 
Kwani si kuna TBS au ni kwa biashara peke yake??lazima kuwe na mtu huko wizara ya Afya anayehakikisha vinavyoliwa na mtu ni salama, watu hawaumwi immediately.. ila accumulation of chemicals ina athari baadae
 
Hongera Titicomb kwa kuwaza kwa namna ya kipekee. Imefika wakati sasa kama chi, tujenge utamaduni wa kuthamini, huhimiza na kufanya tafiti zenye kuleta tija.

Wengi wanasema mercury au madawa ya kusafishia madini hayawezi kuwa chanzo cha saratani inayoathiri sana watu wa kanda ya ziwa. Bado haiondoi haja ya utafiti kufanyika ili kubaini kipi kinapelekea hali hiyo kutokea.

Siamini kabisa kwamba hatuna uwezo wa kufanya huu utafiti, tatizo ni nia ya dhati na tabia za kuchukulia mambo kwa mazoea.
 
Back
Top Bottom