The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 19,254
- 42,873
Bahari una iachaje taka zote za kemikali zinatupwa humo
Mazingira ya Bahari na Ziwa yako tofauti mkuu japo yote yanahusisha maji.
Bahari una iachaje taka zote za kemikali zinatupwa humo
ni kweli kuna idadi kubwa ya wagonjwa wa kansa hasa Bunda ni vema serikali ifanye utafiti kwani kinga ni bora kuliko tiba
Na isiwe mwanza tu, maana lile ziwa ni kubwa na linahusisha mikoa kadhaa. KAMA UNAHISI TU SAWA HAKUNA TATIZO,ILA KAMA NI KWELI KUNA HAYO MAMBO HAKIKA HATA SOKO LA HAO SAMAKI LITAATHIRIKA VIBAYA MNO.....Ninahisi matumizi holela ya kemikali kama zebaki na nyinginezo zile za kusafishia madini migodini au zinazo tumiwa na wachimbaji wadogo wadogo wa madini, inawezekana hizo ndiyo huchafua mazingira mashambani, mitoni na ziwani.
Ningeshauri serikali ifanyie tafiti juu ya samaki toka ziwa Victoria, mito yote kanda hiyo unaweza kukuta jambo la kushitua.
Tafiti iende mbali na kuchunguza pia mazao toka mashambani mikoa yote ya kanda ya ziwa.
Kama chanzo kinaweza kuwa hicho nilichohisi basi tatizo linaweza kusambaa miji mikubwa kama Dar es Salaam, Dodoma, na mikoa mingine wanayo tumia samaki toka ziwa Victoria kama Sato, Sangara na Dagaa.
Sio vibaya wakichunguza na dawa za mifugo pia.
Serikali ichukue hatua tusisubiri janga kubwa.
Angalizo: Sijasema samaki wa ziwa Victoria wana tatizo.
Bandiko hili limechochewa na hoja hiyo hapo chini kama alivyochangia mjadala flani ndugu Subisubi humu jukwaani JamiiForums.
CC: Mh. Rais John Pombe Magufuli, Maskamu wa raisi Bi SSS, Waziri Mkuu MKM, Waziri wa Afya, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Uvuvi,..., .., NEMC, .. et al.
UPDATES:
Kuna baadhi ya hoja za kisiasa kama hizo hiyo hapo chini tuziepuke zitatupotosha
Tukianza kulipa sura ya ukabila au ukanda jambo hili tutakosea sana.
- Sisi wengine wa kanda mbali mbali tunakula samaki wanaotoka maeneo ya kanda ya ziwa.
- Madukani tunanunua mchele toka mkoa wa Shinyanga kama ule mchele wa Kahama.
- Tunakula ndizi toka kanda ziwa kama zile za Bukoba.
- Tunakula nyama ya ng'ombe toka kanda hiyo.
- Tunakula viazi vitamu toka kanda hiyo.
- Tunatumia asali toka kanda hiyo.
- Tuna ndugu zetu wanafanya kazi na kusoma kanda hiyo.
- Tuna ndugu zetu wanaishi na kufanya biashara kanda hiyo.
- Chakula cha kuku kinawekwa dagaa wanaotoka kanda hiyo, na baadae sisi tunakula hao kuku au mayai yao, kama unajua ABC za sayansi basi utajua hatupo salama wote tuliopo ktk huo mnyororo wa chakula(food chain).
Ubaguzi na siasa zitatumaliza ...
Walaji wa mchemsho wa samaki(sato) hapa DSM na mikoa mingine wengi ni wa kabila tofauti na wasukuma.
Bahari ni dampo kuu la taka chafuzi duniani hiyo ndio tofauti na hayo maji ya ziwa yana ishia baharini kupitia mto nileMazingira ya Bahari na Ziwa yako tofauti mkuu japo yote yanahusisha maji.
Maoni yako mazuri mkuu,Bahari ndo inajaa uchafu haswa
Sidhani kama samaki wanahusika na Cancer
Ninahisi tu, hakuna haja ya kuwatisha watu.Na isiwe mwanza tu, maana lile ziwa ni kubwa na linahusisha mikoa kadhaa. KAMA UNAHISI TU SAWA HAKUNA TATIZO,ILA KAMA NI KWELI KUNA HAYO MAMBO HAKIKA HATA SOKO LA HAO SAMAKI LITAATHIRIKA VIBAYA MNO.....
Ushauri wangu ni kwamba kuliko kuropoka na kuandika hovyo ni bora ukaripoti kwenye mamlaka husika.
Bahari ni dampo kuu la taka chafuzi duniani hiyo ndio tofauti na hayo maji ya ziwa yana ishia baharini kupitia mto nile
Mkuu umeleta hoja nzuri sana sana.Elimu kuhusu madhara ya kemikali za migodini na dawa za kuua viatirifu Wananchi wengi hawana elimu ya kutosha.
Wakazi wengi wa kanda ya Ziwa wanalima zao la Pamba na kitu ambacho ni kibaya wanachangamya na mazao mengine kama mahindi na maharage. Tatizo linakuja pale wanapotumia madawa makali kuulia viatirifu zinaathiri mazao kama Mahindi au Maharage pia kinaweza kuwa chanzo cha magonjwa mengi ya Kansa.
Pia kuna baadhi ya wakulima wanaolima mazao kama Kabeji(Cabbage) kando kando ya Ziwa wakati Kabeji zinachanua wanatumia madawa makali ya Pamba,wakati Kabeji inapojifunga dawa inakuwa ndani ya kabeji hadi inapokomaa.Hivyo basi kwa matumizi yasiyo sahihi ya madawa ya kuua viatirifu kwa mazao ambayo hayaitaji madawa makali au dawa ambazo zinachukua muda kupoteza makali nadhani pia inaweza kuwa chanzo cha magonjwa ya Kansa.
Kuna ulazima wa hizi taasisi kutoa elimu na kufanya ukaguzi kila wakati ili kuondoa hatari za visabishi vya Kansa na pia Serikali/Bunge iwape fedha za kutosha kwa ajili ya kufanya tafiti.