Serikali fanyeni Huduma za Afya kwa Wanafunzi ziwe bure

Drone Camera

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
13,838
2,000
Hili ni ombi kwa serikali yangu.Fanyeni huduma za afya kwa wanafunzi wetu ziwe bure.

Hili ni tatizo sana hasa kwa shule za bweni.Unakuta wanafunzi kukwepa gharama ya matibabu ambayo kimsingi hawaimudu wanashare bima za afya.

Na hapo itabidi mhusika atafute mwenzie wanaeendana muonekano kidogo ili wasimshtukie.Sasa hii inaleta usumbufu kwa wanafunzi na kuathiri mfumo wao mzima wa taaluma.

Hata hizo zahanati za shule hazitoi huduma za vipimo sanasana ni dawa za mafua,kichwa na tumbo.

Waondoleeni hizo gharama watoto wetu kama mlivyowapa elimu bure maana hata afya mnaipa kipaumbele.
Nawasilisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom