Serikali fanyeni haya kupunguza foleni Dar!

Masakata

JF-Expert Member
Jan 2, 2011
374
137
Kati ya mambo yanayotukera wenyeji wa jiji hili la Dar,ni foleni ya magari,,yani ni KERO kubwa sana,..nikiwa mmoja ya waathirika wa hili janga naishauri serikali kufanya yafuatayo ili kupunguza walau hii foleni

1.Hili eneo la Tanganyika Packers lichukuliwe na serikali na zijengwe ofisi za kutosha na kuwepo huduma zingine za kijamii kama mabenki,hospitals n.k ili kupunguza wimbi la watu kwenda city centre,napendekeze eneo hili kwa kuwa kwanza ni eneo kubwa na halitumiki kusaidia sana jamii,,pia linaweza kupanuliwa kirahisi kwa kujichukua nyumba zilizo karibu kwa kuwalipa wamiliki fidia ambazo naamini hazitokuwa kbwa kutokana na hadhi ya nyumba zenyewe

b.Pili,ni eneo linaloweza kufikika kirahisi kwani njia hizi mbili, i mean New and old Moro rd zinapita karibu na eneo hili(hasa hii old)

c..Kuna watu wengi sana wanaotumia magari binafsi toka ukando huo mf Tegeta, Mbezi, Kunduchi, Boko, Bunju, so hawa watu wakipatiwa huduma kama ofisi wengi wao hawatokuja mjini na hivyo kupunguza foleni

2.Jambo la pilli, ni kutmika kwa reli ya kati kuleta abiria wa meeneo ya mjini, kuanzia Pugu ,na hili linawezekana ikiwa stesheni (headoffice itahamishwa kwenda Pugu, hivyo wasafiri wa treni wawe wanaenda pandia hukohuko pugu.

So kipande toka Pugu kiwe kwa ajili ya kushaffirisha watu wa Dar tu na treni za mizigo tena hizi za mizigo ziwe zinasafiri usiku tu ili kuruhusu usafiri wa watu mchana

3.Mwisho matumizi ya technologia sahihi ya taa za barabarani,..kwa uelewa wangu hivi sasa kuna program za kueziendesha taa za barabara kwa kuanagalia upande gani kuna foleni, hivyo kutoa upendeleo flani kwa upande huo, jaribuni kuwasiliana na wataalamu wa DIT na watz wengine.

Nawasilisha
 
asante Masakata kwa kuja na mawazo ya kutatua tatizo unlike wengine ambao huishia kulalamika.

Ukweli wa mapendekezo yako ni kwamba yatatumia gharama kubwa kutekelezeka na itahitajika kubadilisha saikolojia ya watu wa DSM ambao kwa asili wanaonekana kuwa wabishi na kujifanya wanajua kila kitu.

Inaelekea unaonelea hili eneo la Tanganyika Packers ndilo liko strategic tu lakini maeneo kama Kimara/Ubungo, Magomeni, Tabata yana foleni kupita kiasi lakini ukichunguza sana hizi foleni huwa ni za mida fulani ya siku maana ukija saa 6 usiku au katikati ya mchana zinakuwa hazipo!

Mapendekezo mbadala:
1. Jiji liwe na maana halisi ya jiji (yaani city) kwa kufanya shughuli zake masaa 24. Hii itaepusha wakaazi wote kuingia mjini saa 1 asubuhi na kutoka saa 10 jioni. Hapa ni kuimprove mipango miji na ulinzi ili kufanikisha hili.

2. Badala ya kufikiria kujenga projects kubwa kubwa kama za Shanghai, Jo'burg, Chicago, Tokyo, London, nk (yaani fly-overs) ambazo kwa uwezo wetu kiuchumi na aina za magari tunayotumia (makuu kuu) itakuwa vigumu kuzitumia, tufikirie kujenga diversions ndogo ndogo mfano wa daraja la reli Pugu Rd karibu na KAMATA/Shoprite. Hizi zinaweza kuendana na projects ndogo ndogo tu za ku-upgrade barabara za mitaa.
-Mfano Barabara inayotoka Tabata ikifika MADONA ipitilize kwa kunyoosha juu Mandela Rd na kuunganisha na Kigogo.
-Barabara ya Sayansi kupitia kwa Mtogole, ipite juu/au chini ya Morogoro Rd ikiendelea hivyo hadi Royola Secondary vivyo hivyo mpaka Mandela Rd maeneo ya Mwananchi.
-Barabara ya Africana (Mbezi) itafutiwe alternative ya kupitia Changanyikeni then ipite juu/chini ya Morogoro Rd/Kimara Baruti au Bucha na kuelekea Kibangu/Tabata/Bunyokwa.
-Barabara ya Changombe kupitia Maduka mawili ipitilize mpaka Maeneo ya BP (kumbuka kutoka Mivinjeni - KAMATA) tayari wanaweka double Rd

Hii ni kwa kifupi. Ki ukweli hizi barabara nilizoongelea sio DOUBLE ROAD, ni hizi tu za kawaida na gharama zake ukialinganisha hesabu za waziri Magufuli kuwa 1km inajengwa kwa 800m-1b haziwezi kufikia 100b ikijumlisha na fidia wanaoweza kuhamishwa.

Accountability ya hiyo 100b ni delays na mafuta yanayoungua kwenye hizi foleni!
 
Subirini ahadi za Kikwete si aliwa ahidi muwe na Subra 2015 kwani ishafika? Barabara za Juu Zaja..

Ile list ya Ahadi za Jk Nikizisoma natamani Kumzaba Kofi paka wangu
 
alafu hizi kauli za baadhi ya viongozi (kama sio wote!) zinakatisha tamaa na kuchefua.
Fikiria mtu amekaa kwenye kiti cha 'kunesa' ndani ya kiyoyozi alafu anasema kuwa "umeme hautapanda kwa watumiaji wadogo"
au "uchumi unakua kwa 8.5%"!!!!
....au sijui kwa sababu wanaoongea wameshajijua kuwa ndio vyanzo vya haya matatizo yote pamoja na foleni hizi!!!
Foleni ni ishara ya uchumi kukua kwa kasi- JMK!:yawn:
 
Mgufuli alisema foleni itaisha baada ya siku 100 tangu arudi ujenzi.......sijui bado hazijaisha? Mimi nashauri Kariakoo ihamishwe
 
hata mimi nilifikilia hilo mkuu kariakoo haifai kuwa pale itapunguza folleni kwa 50% iende nje ya mji!
 
asante Masakata kwa kuja na mawazo ya kutatua tatizo unlike wengine ambao huishia kulalamika.

Ukweli wa mapendekezo yako ni kwamba yatatumia gharama kubwa kutekelezeka na itahitajika kubadilisha saikolojia ya watu wa DSM ambao kwa asili wanaonekana kuwa wabishi na kujifanya wanajua kila kitu.

Inaelekea unaonelea hili eneo la Tanganyika Packers ndilo liko strategic tu lakini maeneo kama Kimara/Ubungo, Magomeni, Tabata yana foleni kupita kiasi lakini ukichunguza sana hizi foleni huwa ni za mida fulani ya siku maana ukija saa 6 usiku au katikati ya mchana zinakuwa hazipo!

Mapendekezo mbadala:
1. Jiji liwe na maana halisi ya jiji (yaani city) kwa kufanya shughuli zake masaa 24. Hii itaepusha wakaazi wote kuingia mjini saa 1 asubuhi na kutoka saa 10 jioni. Hapa ni kuimprove mipango miji na ulinzi ili kufanikisha hili.

2. Badala ya kufikiria kujenga projects kubwa kubwa kama za Shanghai, Jo'burg, Chicago, Tokyo, London, nk (yaani fly-overs) ambazo kwa uwezo wetu kiuchumi na aina za magari tunayotumia (makuu kuu) itakuwa vigumu kuzitumia, tufikirie kujenga diversions ndogo ndogo mfano wa daraja la reli Pugu Rd karibu na KAMATA/Shoprite. Hizi zinaweza kuendana na projects ndogo ndogo tu za ku-upgrade barabara za mitaa.
-Mfano Barabara inayotoka Tabata ikifika MADONA ipitilize kwa kunyoosha juu Mandela Rd na kuunganisha na Kigogo.
-Barabara ya Sayansi kupitia kwa Mtogole, ipite juu/au chini ya Morogoro Rd ikiendelea hivyo hadi Royola Secondary vivyo hivyo mpaka Mandela Rd maeneo ya Mwananchi.
-Barabara ya Africana (Mbezi) itafutiwe alternative ya kupitia Changanyikeni then ipite juu/chini ya Morogoro Rd/Kimara Baruti au Bucha na kuelekea Kibangu/Tabata/Bunyokwa.
-Barabara ya Changombe kupitia Maduka mawili ipitilize mpaka Maeneo ya BP (kumbuka kutoka Mivinjeni - KAMATA) tayari wanaweka double Rd

Hii ni kwa kifupi. Ki ukweli hizi barabara nilizoongelea sio DOUBLE ROAD, ni hizi tu za kawaida na gharama zake ukialinganisha hesabu za waziri Magufuli kuwa 1km inajengwa kwa 800m-1b haziwezi kufikia 100b ikijumlisha na fidia wanaoweza kuhamishwa.

Accountability ya hiyo 100b ni delays na mafuta yanayoungua kwenye hizi foleni!

Nami nikupongeze mkuu kwa kuja na mawazo mbadala,na ni kweli tujenge utamaduni wa kutoa alternatives(ingawa sijua kama hii serikali ni sikivu kiasi hicho),ila cha msingi sisi tuplay part yetu ya kushauri..
Kwanza tukubaliane ya kwamba kwa jinsi ambavyo jiji letu lilivyokosewa,.tatizo la foleni litatatuliwa kwa njia zaidi ya moja,hivyo nilitaja hiyo ya Tanganyika Packers kama njia mojawapo ili kupunguza suala la ofc na huduma kuwa sehemu moja..pili,hivi kiuchumi sehemu potential kama T.packers kuwa wazi vile ni sawa kweli?..kuhusu gharama mimi sidhani kwani now kuna mifuko kama PPF,NSSF,LAPF wanaweza kushirikiana na govt kuwekeza pale wakizingatia win to win situation..nadhani hili linawezekana kabisa
Hilo la Fly over naliunga mkono,lakini nalo linagharama,ila wanaweza kuanza na maeneo yale muhimu..kingine kuna hili reli ya Ubungo Maziwa to Buguruni nayo waingalie,inaweza saidia kama nilivyoshauri ile ya Pugu Posta.
 
Kati ya mambo yanayotukera wenyeji wa jiji hili la Dar,ni foleni ya magari,,yani ni KERO kubwa sana,..nikiwa mmoja ya waathirika wa hili janga naishauri serikali kufanya yafuatayo ili kupunguza walau hii foleni

1.Hili eneo la Tanganyika Packers lichukuliwe na serikali na zijengwe ofisi za kutosha na kuwepo huduma zingine za kijamii kama mabenki,hospitals n.k ili kupunguza wimbi la watu kwenda city centre,napendekeze eneo hili kwa kuwa kwanza ni eneo kubwa na halitumiki kusaidia sana jamii,,pia linaweza kupanuliwa kirahisi kwa kujichukua nyumba zilizo karibu kwa kuwalipa wamiliki fidia ambazo naamini hazitokuwa kbwa kutokana na hadhi ya nyumba zenyewe

b.Pili,ni eneo linaloweza kufikika kirahisi kwani njia hizi mbili, i mean New and old Moro rd zinapita karibu na eneo hili(hasa hii old)

c..Kuna watu wengi sana wanaotumia magari binafsi toka ukando huo mf Tegeta, Mbezi, Kunduchi, Boko, Bunju, so hawa watu wakipatiwa huduma kama ofisi wengi wao hawatokuja mjini na hivyo kupunguza foleni

2.Jambo la pilli, ni kutmika kwa reli ya kati kuleta abiria wa meeneo ya mjini, kuanzia Pugu ,na hili linawezekana ikiwa stesheni (headoffice itahamishwa kwenda Pugu, hivyo wasafiri wa treni wawe wanaenda pandia hukohuko pugu.

So kipande toka Pugu kiwe kwa ajili ya kushaffirisha watu wa Dar tu na treni za mizigo tena hizi za mizigo ziwe zinasafiri usiku tu ili kuruhusu usafiri wa watu mchana

3.Mwisho matumizi ya technologia sahihi ya taa za barabarani,..kwa uelewa wangu hivi sasa kuna program za kueziendesha taa za barabara kwa kuanagalia upande gani kuna foleni, hivyo kutoa upendeleo flani kwa upande huo, jaribuni kuwasiliana na wataalamu wa DIT na watz wengine.

Nawasilisha

Hapo kwenye rangi nyekundu pamekaaje - ni Moro au Bagamoyo rd?
 
itabidi usafiri wa UNGO u2mike ili kupunguza foleni!! .......unatoka CHARAMBE to TEGETA kwa dk. 0
 
Back
Top Bottom