Serikali: Familia ya Majuto na Kanumba wameshalipwa fedha walizokuwa wanadai kutokana na kazi zao walipokuwa hai

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,479
9,234
25e6ecbf63c8160982824cb09450021f

Serikali imesema kuwa imeokoa na kurejesha mamilioni ya fedha kwa familia za marehemu Mzee Majuto pamoja na familia ya marehemu Steven Kanumba kupitia mikataba ya kazi walioingia wakiwa hai.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi katika hafla ya kukabidhi nyaraka za uhamishaji wa COSOTA kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara kwenda Wizara ya Habari.

“Familia ya Marehemu Mzee Majuto mpaka sasa tumewarejeshea TZS milioni 65 na familia ya Marehemu Steven Kanumba tumeirejeshea TZS milioni 20 kutoka katika mikataba ya kazi waliyokuwa wameingia,” amesema Dkt. Abbasi .

Aidha, amewahakikishia wasanii kuwa serikali ipo macho na inalinda kazi zao kuhakikisha wananufaika na sanaa na sio kuwa masikini wenye majina maarufu.

Zoezi la kuhamisha COSOTA limekamilika ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli alilolitoa Julai 12 mwaka huu jijini Dodoma akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, wasanii na wageni wengine aliowaalika Ikulu ya Chamwino kwa ajili ya chakula cha mchana.
 
Baba Kanumba Mungu amempenda zaidi
Kabakia mzazi mmoja ambaye ndio mama,atakula jasho la mwanae
Sijui kwa mzee Majuto,maana aliacha mke na watoto wengi
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom