Serikali corrupt, hali yetu na upofu wa viongozi wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali corrupt, hali yetu na upofu wa viongozi wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Profesa, Apr 2, 2012.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Serikali hii sio kiongozi wake la hasha ila watendaji wake ndio watekelezaji wakuu wa uovu huo, na mbaya zaidi ni pale ambapo hawajali hata kama Raisi au kiongozi anadhalilika... ila hawajui kitu kimoja ... yeye hataaathirika... ni kuwa serikali hiyo itaangamia na watu wake maana walio wengi ndio masikini na wenye kipato cha chini na ndio wapiga kura na sio wachache hivyo nguvu ya pesa haiwezi kamwe kushinda nguvu ya ...

  Ninamaanisha watu walioko serikalini hawaoni mbali na hawahangaiki ipasavyo kuweka mfumo wa kweli unaodumu ambapo hata akija raisi wa upinzani bado sera na mipango inabaki palepale kwa sasa wanajisaliti wenyewe bila kujijua...wanagawa viwanja na ardhi tofauti na sheria na taratibu rushwa yako tu...wanatunga na kuweka sera wakiwa mijini ndani ya kiyoyozi huku akili zao zikiwa na sumu za runinga bila kujali maslahi ya mila, desturi, jamii na hali halisi ya mtu wa kijijini mkulima wa chini na mfugaji wa asili.

  Mfano, wanapowalazimisha wafugaji kuacha uchungaji wa kuhamahama wanaangamiza mila na desturi zetu wanaua indiginous technologies (ufundi wa asili wa kisayansi wa mf matibabu, utabiri wa hali ya hewa, ubashiri wa majanga n.k), wanatoa nafasi serikalini hata idara nyeti kitaifa na za kisiasa kwa ndugu jamaa na ... bila kujali uwezo, wao watoto wao wanakwenda shule za st... academia... ambazo ada zake na mishahara yao halali havina uwiano, wanahudumiwa India na... na wanapopanga sera za Elimu na Afya wanaamini kila mtanzania ana uwezo kama wao, wana uhakika wa mlo wa siku kwa hiyo mifumuko ya bei na hali ngumu ya watu kwao inachukua muda kuwagusa maana wasipokula nyumbani watakula kwenye wekishopu ambapo mlo wa mtu mmoja unawea kuwa mlo wa familia nzima pale Tandale kwa Mfuga Mbwa, wana amini uwezo wa kulindana kwa hiyo hawana hofu na wewe. THIS IS CORRUPTION!

  Hizi ndio serikali nyingi Africa ambazo hazioni kizazi cha sasa kinachokuja ambacho hakijaathirika na sumu za Nyerere wala za Kwame wao wanaamini wanachoamini na wana nafasi ya kuuona ulimwengu kuliko mimi na wewe ambao technohama ilikuja kama mazingaombwe na ikatuchukua muda kuamini kuwa ni kitu real. Wao wamezaliwa nacho na wana spidi yakukijua na kukitumia kuliko mimi nawewe. Je Wazee wa serikali hizi wanalijua hili. HAWA NDIYO WAPIGA KURA WA 2015 kwa Tanzania na kwa nchi nyingine kutegemeana na tarehe zao za uchaguzi.

  Kama ataibuka kiongozi na si mtawala anaejua tofauti zetu wote kisiasa, kiutamaduni, ki-kizazi na hata kijamii basi akanena yale yanayoweza kutufanya tuamke natuhamasike kufanya mambo yetu yenye kuteletea maendeleo yetu, hapo ndipo tutakapokuwa na matumaini. Asieamini uwekezaji bali uwezeshaji ili watu waweze kutumia na kuvuna rasili mali zao wenyewe kwa manufaa yao wenyewe, ambaye anasimamia majadilianho sawa na mataifa ya nje katika maslahi, mwenye kijali kizazi kijacho na si cha sasa tu. Sio aliyekuwa brainwashed na mataifa malafi kwa consept ya 'uwekezaji' yenye baraka za 'taxi holiday' na milungula inayolingana na mishahara yooote na viinua mgongo vyoote kwa viongozi wahusika.

  Kwa sasa nchi nyingi za Africa hazina viongozi zina watawala, NA HILO NDILO LINALOPELEKEA MAPINDUZI KWA STAILI ZAKE MBALIMBALI.
   
 2. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Profesa umunena asante kwa uwasilishaji wa mada mzuri - simple and straight forward. Shida iko kwa viongozi wetu uliowalenga sijui kama wanasoma, na hata wakiisoma zaidi sana watakuwa busy kuona kama waweza kukusakizia vyombo nyeti vya umma vikunyamazisha.

  Wao wako zaidi kwenye message za umbea na ndiyo maana hii thread haina michango, ingekua ya umbea au any business as usual issue reply zingekuwa zinazidi 1000 hadi leo. Cha kusikitisha zaidi hii thread iko jukwa mahsusi la great thinkers.

  Umesema vema kuhusu kutojali kwa viongozi wetu na uvivu wakufikiri walionao japo hawapendi kuitwa dhaifu, nimeyanena pia katika thread zangu za karibuni - Mnyika umesema wao wamethibitisha na udhaifu na ushupavu wa voingozi wetu na ile ya mgomo wa MAs

  ukweli ni kuwa siku za viongozi wa sampuli hii zinaheasabika
   
Loading...