Serikali: Chaguo la pili na tatu kidato cha kwanza kuwa historia, wanafunzi kuanza masomo kwa pamoja

benzemah

Senior Member
Nov 19, 2014
195
250
Leo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu ameeleza kuwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu inakwenda kuandika historia kwa kufuta suala la wanafunzi wanaoingia kama changuo la pili na la tatu (Second and Third Selection) kutokana na upungufu wa madarasa.

Waziri Ummy amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha hela za ujenzi wa madarasa zilizotolewa kwa kila Wilaya na Mkoa nchini zinatumika ipasavyo kuhakikisha ujenzi wa madarasa unakamilika ifikapo Disemba 15 mwaka huu.

Kwa hatua hiyo ina maana kwamba mwaka ujao wa masomo wanafunzi wote wa kidato cha kwanza wataanza masomo kwa pamoja jambo ambalo halijatokea nchini kwa kipindi kirefu.

Kama hili likitimia kwa wakati na ubora basi ni dhahiri neema itakuwa imeanza kurejea nchini. Baada ya hapa sasa nadhani jitihada zipelekwe kwenye kuinua hali ya maisha ya walimu na kuwapa vitendea kazi na makazi mazuri.
 
MoureenAbel

Member
Sep 24, 2021
22
75
Tunaweza tukapinga tunavyotaka ila kuna wakati inabidi tukubali kuwa baada ya muda mfupi, mambo yote anayoyafanya Rais Samia yataibadilisha nchi na kuifikisha sehemu ambapo watu wengi tulikuwa tukitamani kufika.

Leo nimemsikiliza Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu akizungumzia mgawanyo wa bilioni 302 ambazo ni sehemu ya trilioni 1.3 zilizotolewa na IMF, na kwamba wanakwenda kujenga madarasa 15,000 nchi nzima, ambapo madarasa 12,000 ni kwenye shule za sekondari na 3,000 ni kwenye shule shikizi.

Mapinduzi haya si tu yataondoa msongamano kwenye vyumba vya madarasa na wanafunzi kusoma wakiwa wamepigana migongo, lakini pia iawafanya wote watakaofaulu mwaka huu kuingia kidato cha kwanza kwa wakati mmoja. Hakutakuwa na yale mambo ya second na third selections, mzigo unatoka mara moja, watoto wanaanza masomo.

Kwa wale mnaopinga na kubisha mambo, hifadhini maneno yenu, tutakutana hapa Januari 2022, tuone ni kweli au uongo.

Rais endelea kupiga kazi. Ili dhahabu ingare, lazima ipite kwenye moto.Tumekuelewa.

WhatsApp Image 2021-10-12 at 13.15.16.jpeg
 
Paubae5

Senior Member
Oct 9, 2021
112
250
Tunaweza tukapinga tunavyotaka ila kuna wakati inabidi tukubali kuwa baada ya muda mfupi, mambo yote anayoyafanya Rais Samia yataibadilisha nchi na kuifikisha sehemu ambapo watu wengi tulikuwa tukitamani kufika...
Asee ...
 
kindafu

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,329
2,000
Tunaweza tukapinga tunavyotaka ila kuna wakati inabidi tukubali kuwa baada ya muda mfupi, mambo yote anayoyafanya Rais Samia yataibadilisha nchi na kuifikisha sehemu ambapo watu wengi tulikuwa tukitamani kufika...
Kwa taarifa yako swala la 2nd & 3rd selections kwa wanafunzi wa shule za kata & serikali haitokani tu na swala la upungufu wa vyumba vya madarasa.

Kuna watoto wengi wanashinda na kupangiwa shule ila wazazi wanaamua ama kuwapeleka shule binafsi au wanatumia njia zao kuhamishia majina ya watoto wao kwenye shule wazipendazo wao.
 
benzemah

Senior Member
Nov 19, 2014
195
250
Kwa taarifa yako swala la 2nd & 3rd selections kwa wanafunzi wa shule za kata & serikali haitokani tu na swala la upungufu wa vyumba vya madarasa.

Kuna watoto wengi wanashinda na kupangiwa shule ila wazazi wanaamua ama kuwapeleka shule binafsi au wanatumia njia zao kuhamishia majina ya watoto wao kwenye shule wazipendazo wao.
Kwa ulichoandika hapa ni wazi kuwa wewe hata 4th selection hukupata
 
Dan Zwangendaba

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
2,851
2,000
Kwa taarifa yako swala la 2nd & 3rd selections kwa wanafunzi wa shule za kata & serikali haitokani tu na swala la upungufu wa vyumba vya madarasa.

Kuna watoto wengi wanashinda na kupangiwa shule ila wazazi wanaamua ama kuwapeleka shule binafsi au wanatumia njia zao kuhamishia majina ya watoto wao kwenye shule wazipendazo wao.
Umeongea kitu kilekile. Kwamba hao wanaopelekwa kuziba nafasi za walioenda shule binafsi au shule wazipendazo wazazi kimsingi nao walifaulu ila nafasi hazikuwepo. Zingekuwepo wasingeenda kwa njia ya kuziba" nafasi bali wangeanza moja kwa moja kama wenzao.
 
kirengased

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
4,682
2,000
Tusilazimishane kuamini mambo ya kawaida kuwa nimambo ya ajaaabu...Wenzetu majirani hawana huo upuuzi wa kushindwa kudahili watoto Kenya nindogo kwetu na inawatu wachache lakini wanadahili watoto weeengi sana kutuzidi bila awamu awamu!!
Ccm inatuchelewesha sana alafu wakijakufanya wanatusisitiza kuwa jambo wafanyalo nijambo kuuubwa la maajabu!!! Studio!
Hapo Rwanda pamoja na mavita wanamadege sikunyingi nawala Raid hajitutumui kuwa anafanya maajabu sijui anacheza mwingine... yaani hamna mapropaganda yaujinga ujinga!!
Sirkali iache kutuona sisi mazuzu.
unakopa (tutalipa sisi) alafu unanunua vituvitu alafu unatuambia unaupiga mwingine!!! Vuta maviwanda,inua makilimo,boresha mifumo ya elimu,iinue haki na demokrasia,pambania uvuvi na ufugaji,kuza utalii et usijisifu kwa kukopa na kutumia,that's very low!!
MAZUZU/MAFISADI HAYATONIELEWA KABISA
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom