Serikali: CHADEMA inapewa pesa kutoka nje kuleta machafuko Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali: CHADEMA inapewa pesa kutoka nje kuleta machafuko Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fareed, Mar 7, 2011.

 1. F

  Fareed JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Matamshi haya ya Sophia yanaonesha kuwa serikali ya Kikwete inaamini kuwa foreign governments are funding CHADEMA ili kifanye maandamano na kuleta vurugu nchini.

  Watawala wanajiaminisha kuwa eti CHADEMA inawalipa wale maelfu ya Watanzania wanaojitokeza kwenye maandamano.

  Msimamo wa serikali ya Kikwete imenikumbusha ya Gadaffi wa Libya ambaye US President Ronald Reagan alimuita kama "The Mad Dog of the Middle East" way back in 1986.

  Gaddafi alisema: "Wananchi wa Libya wananipenda sana. Wanaoshiriki maandamano wamelishwa madawa ya kulevya na Al Qaeda na Marekani."

  Pia kwa kusema "Kama kuna matatizo yoyote, serikali itayashuhulikia," hii ina maana kuwa watawala hawatambui matatizo lukuki ya wananchi wa Tanzania ambao ni kama kila mmoja kabeba gunia la misumari -- mgao wa umeme, Dowans, ufisadi, umasikini, ukosefu wa ajira, mfumuko wa bei, maisha magumu, kuporomoka kwa elimu, afya duni, ukosefu wa maji, maradhi, viongozi serikalini kutokuwa na maadili, wananchi kunyimwa haki zao, na mengineo mengi.

  The CCM government is in denial.
   
 2. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  this woman must be mad!
   
 3. Unyanga

  Unyanga JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mfano wako wa gaddafi na mada yako mezani haviendani! Jaribu kuleta mfano relevant na mada yako
   
 4. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Ama kwel mambo yanavyozd kuwa magumu ndipo ninapogundua kuwa kumbe CCM ina vilaza(poyoyo) weng sana. Huyu mama naye keshajihakishia uwepo wake ktk hyo group ya vlaza..... Jaman ngoja ninywe chai halafu baadaye ntawasilisha majina yote ya vilaza waliopo ccm...
   
 5. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hiyo ndiyo aina ya viongozi wenye nguvu ndani ya CCM. Kama kuna matatizo yoyote, inamaana yeye hajui kuwa kuna matatizo. Serikali ya CCM imeshindwa kushughulikia matatizo kipindi cha nyuma itawezaje sasa? Wameshindwa kazi wawaachie wengine wafanye.
   
 6. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2011
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Mfano wa Ghaddafi ni sawa kabisa. Yametokea maandamano ya kudai demokrasia Libya Ghaddafi akadhani kuna mkono wa nje (na unga). Sasa yako maandamano ya kudai uongozi bora Tanzania, Sophia Simba amedhani kuna mkono wa nje. Vinashabikiana vizuri tu.

  Ni haki ya kikatiba kwa vyama vya siasa kufanya maandamano ya kuhamasisha wananchi. Viongozi wa CCM waache kuogopa. Ila kati yao wako waliopanga maandamano ya kuishinikiza serikali (UVCCM) na hiyo ni sawa tu.

  Sophia is not ministerial material. Si huyu huyu alikuwa anapoteza muda kupanga wanawake wavae nini?

  Wanaojitokeza kukemea CHADEMA wanatafuta umaarufu tu. Hawana chochote wala si lolote.
   
 7. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  Maneno ya Simba yana mantiki, si rahisi kuandaa maandamano kila kukicha, unahitaji bajeti nono. Jee fedha zinatoka wapi?
   
 8. K

  Kambarage Member

  #8
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tabaka la watawala Tanzania ni sawasawa na Gaddafi kwa sababu zifuatazo:

  1. Wote wanaimani potofu kuwa serikali yao inapendwa sana na wananchi
  2. Wote wanaamini kuwa maandamano yanachochewa na serikali/taasisi/wafadhili wa nje
  3. Wote wanaamini kuwa wananchi wanapewa kitu ili kushiriki maandamano, eg pesa/madawa ya kulevya
  4. Wote wanaamini kuwa wananchi hawana shida yoyote (eg Sophia akisema "kama kuna matatizo."
  5. Wote wametawala kwa muda mrefu sana (CCM miaka 50 na Gadaffi miaka 42)
  6. Wananchi wa nchi zote wamechoka umasikini, ufisadi, manyanyaso, ukosefu wa ajira, uporaji wa pesa za umma, etc
  7. Chama tawala Tanzania/Libya miaka yote kimekuwa kikishinda uchaguzi wa Urais na wabunge kwa kuiba kura
  8. Need I say more?
   
 9. M

  Marytina JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Sophia Simba is a sexy slave na alishatuambia wanawake tuwanyime uyumba waume zetu kama wanaunga mkono upinzani so yeye anawaza kingono kila kitu

  UGUMU WA MAISHA UNATUUMIZA/UNATUADHIRI WANAWAKE ZAIDI YA WANAUME so sophia is on the bed waiting for ***** especially when she calls for wanawake to drawback from this maandamano.
   
 10. i

  immasoft Member

  #10
  Mar 7, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  mi mgeni bado!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 11. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #11
  Mar 7, 2011
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Kuna sababu kubwa ya viongozi wengine wa CCM kukaa kimya huku Mh. Sofia Simba akiwa ni mmoja wa wachache wanaoongoza kwa kuijibu Chadema. Huyu ni mtu wa mipasho mipasho hivi, upeo wake wa kufikiri na kuchanganua mambo ni mdogo sana na ndio maana kauli zake ni za hovyo hovyo tu.

  Kumpa jukwaa la kumjadili huyu mama ni kupoteza nguvu na malengo. Kapewa kazi ya kuongea utumbo huo na hivyo sio kosa lake.
   
 12. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33

  Mi nadhani Sofia amevumbua siri kutumia intelejensia, huyo ndiyo mmoja wa Intelligence agent wa serikali,aliyetoa habari kuwa maanamano ya CDM arusha yatakuwa na uvunjifu wa amani. hahahah
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  its a good sign kwamba serikali inayumba kwani kila mtu sasa anabwabwaja tu!!! adn they are running from their own shadows
   
 14. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2011
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  Not mad, sick- she must be sick, terribly sick! You simply do not thrush out an argument by asking your good gender to disengage from the other side! WHY single out women! Secondly what evidence is there to suggest that those attending the rallies are being paid and being paid from funds sourced outside the country! Just reminds me of those other sick persons blaming everything on being religiously/Tribally marginalized! Bureee kabisa!
   
 15. N

  Ngao One Member

  #15
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Wewe usiwe ****. Wananchi wa EGYPT waliandamana mfululizo kwa siku 18 mpaka wakamg'oa Mubarak madarakani. Je, nani aliwapa pesa na walitumia bajeti gani?

  Wananchi wanapodai haki yao hujitolea kwa hali na mali na wako tayari kulipa gharama yoyote ile ikiwemo JASHO, MACHOZI na DAMU.

  Kwa taarifa yako tu, baada ya uchaguzi wa mwaka 2010, CHADEMA sasa inapewa ruzuku ya shilingi milioni 200 kwa mwezi. Hizi ni pesa tosha kugharamia maandamano ya nchi nzima. Wala huhitaji pesa za wafadhili.
   
 16. a

  asakuta same JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 15,065
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 0
  crapppppp!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  huyo mama na ccm yake na wengine wote wenye mawazo hayo wote bongo zao zitakuwa na matatizo.
  fedha hizo za mikutano iliyofanyika kanda ya ziwa ni mchango wa wanachama mbalimbali(pipoz power) ikiwemo kila mbunge wa chadema kuchangia laki nne na nusu na kiwango kingine kutoka kwenye ruzuku. na hii mikutano haijagharimu mabilioni kama wanavyofikiria.
   
 17. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #17
  Mar 7, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hivi Sofia simba ni kiongozi wa wapi vile? Sio ubao wa matangazo aqmbao hauna mwenyewe? Nasikia mtu yeyote anaweza kwenda kuandika pale, kwa hiyo sidhani kama asemayo ni ya kwake, katumwa kuwa kisemeo. Logic na asemayo naona siku zote haviendani
   
 18. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #18
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mfa maji haachi kutapatapa ccm wanambwela hadi naona kifo chao kinakaribia. Huyu mama si mzima anatakiwa kupelekwa milembe eti cdm inawalipa pesa watu waandamane huu ni ushankupe na uzandiki wa hali ya juu. Huwezi ukawalipa umati mkubwa kama wa maandamano ya shinyanga. Na bdo mtambwela hadi ifike 2015 wananchi watakuwa wamejua wapi kuna mazezeta na wapi kuna viongozi wa kweli. Huu moto hauzimiki kwa maji ya mgao. Huu moto unahitaji maji yote ya bahari ya hindi sio ya dawasco.
   
 19. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #19
  Mar 7, 2011
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 1,827
  Trophy Points: 280
  CCM ndo wamezoea kuwapa hela watu ili waje kwenye mikutano. pia wamekua wakiwatumia wasanii njaa kama Orijino Comedy na wengine kuweza kuwavutia watu waje kwenye mikutano. wanadhani na CHADEMA wanafanya hivyo. Wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea uraisi wa CCM pale Mwanza nilipotoka nje ya uwanja nilishuhudia watu wakishikana mashati wamedhulumiana pesa walikua wameletwa na mabasi kutoka vijijini. Washabiki wa CHADEMA wanakuja wenyewe uwanjani tena wengine wanaendesha baiskeli kwa umbali mrefu kuja kumsikiliza Dr wa ukweli
   
 20. W

  WEMBE WENGE Senior Member

  #20
  Mar 7, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HAO Ndiyo mawaziri wa serikali ya JK ambayo wananchi milioni arobaini wanasubiri maendeleo toka kwayo. wanaongea hoja zisizo na mashiko, kwa wananchi wenye dhiki kuu ya maisha. kwanini CDM kisipate umaarufu? " CDM ongeza kasi hilo pigo la mwisho na kumwangusha mpinzani kwa KO.

  Waziri mzima uliye na dhamana ya serikali unaweza ukawaambia watu waliokuzunguka na wanakusikiliza utumbo huo , ni aibu sana, sijaelewa Rais anangalia vigezo gani kumteua waziri. kama angetuambia CV anazoangalia tungemsaidia kwa ushauri.
  Huwezi kuamini matamshi ya watu hawa yanatolewa na kuandikwa na vyombo vya habari na wananchi kuyasoma ama kuyasikia "shame"
  Mwingine waziri mkuu mzima anasema CDM kufanya maandamano ni kwamba hawana kazi, Sasa tunamwambia muda siyo mrefu atagundua kumbe CDM walikuwa kazini.
  Hatushangai kwa serikali iliyopo madarakani kusimplify issues ndiyo kawaida yao, hata wananchi kuishi bila umeme kwao simple issue, maisha magumu na matatizo lukuki kwao wao ni simple issues they don't care it is not their responsibilities.
  Mimi nadhani huyu mama na waziri mkuu wake wanatapatapa kisiasa, wapeni maji wafe salama.
  wasalaam
   
Loading...