Serikali, Chadema bado hapatoshi - VIONGOZI WA DINI WAONYA, WATAKATA MWAFAKA HARAKA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali, Chadema bado hapatoshi - VIONGOZI WA DINI WAONYA, WATAKATA MWAFAKA HARAKA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 13, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Saturday, 12 November 2011 21:06[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Katibu Mkuu wa Chadema,Dk Wilbroad Slaa
  [​IMG]

  VIONGOZI WA DINI WAONYA, WATAKATA MWAFAKA HARAKA

  Na Waandishi wetu

  MSUGUANO kati ya Serikali na Chadema sasa ni bayana kufuatia kauli mbalimbali za viongozi wa Serikali kukosoa hadharani mwenendo na utendaji wa chama hicho kikuu cha upinzania nchini.


  Hatua hii imekuja wakati hali tete ya kisiasa ikiendelea kugubika Jiji la Arusha huku Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiri hadharani kuwa maandamano yanayofanywa na Chadema kwa kaulimbiu ya 'Nguvu ya umma,' yanainyima usingizi serikali.


  Mbali na Pinda, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulungo, amekuja juu na kudai kuwa harakati zinazoendeshwa sasa na Chadema, hazina nia njema na kwamba ni mkakati wa maksudi kutaka mkoa huo usitawalike.


  Wachunguzi wa mambo ya siasa nchini wanatafsiri kauli za viongozi hao kuwa zimefungua ukurasa mpya unaodhihirisha kuwepo msuguano mkubwa na wazi kati ya Serikali na Chadema.


  Kwa muda mrefu Chadema imekuwa ikilaumu mambo kadhaa ikiwemo kunyimwa vibali vya maandamano na makada wake kuswekwa rumande na kudai kwamba nyuma ya matukio hayo, kuna mkono wa Serikali.


  Mwanzoni mwa wiki hii viongozi wa Chadema akiwamo, Katibu Mkuu wake, Dk Wilbroad Slaa na Mwanasheria wa chama hicho, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu walikamatwa kwa kosa la kufanya mkusanyiko bila kibali cha polisi katika Uwanja wa NMC mjini Arusha.


  Hata hivyo, hatua hiyo inaonekana kupingwa na baadhi ya viongozi wa dini, wanasiasa na wafanyabiashara mkoani Arusha kwa maelezo kwamba vurugu, vitisho na matumizi ya vyombo vya dola kamwe hayawezi kuleta suluhu ya migogoro ya kisiasa na kushauri kuwepo mazungumzo na majadiliano kati ya makundi husika.


  Kauli za viongozi wa dini
  Wakizungumza na Mwananchi Jumapili kwa nyakati tofauti jana, Askofu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer na Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Wilaya ya Arusha, Abbas Ramadhani Mkindi ‘Darweshi,' kwa pamoja waliwataka viongozi wa serikali na vyama vya siasa mkoani Arusha, kuacha ubabe, vitisho na kuhasimiana badala yake waonyeshe nia ya kweli kumaliza mgogoro huo.
  "Hali ni mbaya Arusha katika nyanja zote. Kisiasa kuna machafuko yanayotuathiri wote, waliomo na tusiokuwemo. Katika matatizo na machafuko haya, huwezi kunyooshea kidole mtu au chama chochote cha siasa, muhimu hivi sasa ni kufanyika majadiliano bila ubaguzi wala kudharauliana ili turejeshe amani mjini mwetu," alishauri Askofu Laizer alipozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu.


  Askofu huyo, alisema Arusha inahitaji viongozi makini wanaozingatia utawala wa sheria, diplomasia na wenye staha katika kushughulikia changamoto zilizopo, kama mgawanyiko mkubwa wa kiitikadi ulioibuka kati ya wafuasi wa CCM na Chadema.


  Kongozi huyo wa kidini mwenye ushawishi na msimamo usioyumba katika mambo yanayohusu jamii, alisema vitisho vya watawala na matumizi ya vyombo vya dola haviwezi kutatua tatizo la Arusha, bali vinaweza kupooza kwa muda na baadaye mambo hayo yataibuka kwa nguvu na mbinu mpya na kusababisha vurugu zaidi.


  Alionya kuwa si busara kupuuza madai ya Chadema na kuwashauri viongozi wa Serikali kuacha kutumia nguvu yadola kutunishiana misuli na chama hicho kwani Arusha inaelekea pabaya na likitokea la kutokea, wote watangamia.


  ''Lazima busara itumike kwa kusikiliza hoja za pande zote husika bila kubezana.'' Alishauri.


  Bila kutaja jina, Askofu Laizer alisema kauli za vitisho zinazotolewa na viongozi wa serikali Arusha, zitachochea harakati za wanaodhani wanaonewa, kutafuta haki na pengine kutumia njia za machafuko zaidi na kuchafua hali ya hewa kuliko livyo sasa.


  Askofu Lazier alivishauri vyama vya upinzani kuepusha shari kwa kudai haki zao kwa njia ya amani hata kama wanahisi kuonewa, kama ilivyo kwa Arusha ambapo vijana wa CCM (UVCCM), waliandamana na kufanya mkutano wa hadhara bila kibali cha polisi, lakini Chadema walipojaribu kufanya hivyo, walikamatwa na kushtakiwa
  kwa kusanyiko lisilo halali.


  "Vyama vya upinzani vikwepe pale sunami au upepo mkali unapovuma dhidi yao, wainame kidogo kimbunga kipite halafu waendelee mbele.


  "Vitumie wataalamu na wasomi waliojaa ndani ya vyama hivyo kutatua matatizo na migogoro inayojitokeza kwa njia ya amani na utulivu," aliasa Askofu Laizer.


  Alisema tatizo linalojitokeza nchini hivi sasa ni vyama vya upinzani kutopewa fursa ya kutekeleza na kuendesha shughuli zao za kisiasa kwa uhuru kama ilivyo kwa CCM.
  Hata hivyo, alivashauri vyama hivyo kufuata sheria na kanuni katika kudai na kutafuta haki yao .


  Kwa upande wake, Mkindi alisema viongozi serikalini wasijidanganye kuwa wanaweza kulinda amani kwa mtutu wa bunduki na kushauri vyama vinavyohasimiana vya CCM na Chadema kukutanishwa ili vijadili na kuondoa tofauti zao ili kurejesha amani na usalama Arusha.


  "Arusha imechafuka, hakuna amani. Biashara imekufa, hata mikutano ya kitaifa na kimataifa haifanyiki hapa tena kwa wingi kama ilivyozoeleka. Ufumbuzi ni watu kukaa mezani wazungumze, waadiliane na kutatua tofauti zao.


  ''Chadema wasidharauliwe hata kidogo kwa sababu wana watu wengi wanaowaunga mkono ambao wako tayari kusikiliza na kutekeleza lolote wanaloambiwa," alisema Mkindi


  Msimamo wa RC Arusha

  Katika siku za karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mulongo amekaririwa akionya kuwa vyombo vya dola vimejipanga kukabiliana na aliowaita, wavuruga amani na waleta machafuko Arusha, na kuelekeza
  mashambulizi ya moja kwa moja kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na chama chake.


  "Nikiwa mhimili na msimamizi wa amani na usalama wa mkoa, sitakubali kushuhudia mtu anavuruga amani tena Arusha. Kibaya zaidi wengi wa wanaoleta vurugu hapa wanatoka nje ya mkoa wetu. Imetosha! Tumechoka," alikaririwa mkuu huyo wa mkoa alipozungumza na viongozi na watendaji wa manispaa ya jiji hilo.  Mgogoro wa Arusha

  Tangu kumalizika uchaguzi mkuu mwaka jana na ule wa umeya, mji wa Arusha umekumbwa na mfululizo wa machafuko yanayoambatana na matumizi ya nguvu ya dola kuyakabili.


  Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, wanachama na wanachama wengine wa Chadema hadi sasa wameendelea kujikuta wahanga wa hali hiyo kwa kuswekwa ndani na kufunguliwa kesi mahakamani.


  Hadi kufikia Alhamisi wiki hii, viongozi wakuu wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Slaa, wanasiasa na wanachama kadhaa wa chama hicho, nao wamejikuta wakikabiliwa na kesi sita tofauti kwa kudaiwa kushiriki mkusanyiko usio halali na kukaidi amri halali ya polisi.


  Mwafaka CCM na Chadema

  Kwa upande wao, viongozi wa Chadema na CCM waliunga mkono hoja ya kujadilina ili kutafuta muafaka wa mgogoro wa Arusha kwa njia ya majadiliano, huku kila upande ukisisitiza kuaminiana na kuheshimiana huku Chadema wakiwatuhumu viongozi wa serikali mkoani Arusha kuwahukumu bila kuwasikiliza malalamiko na hoja zao.


  Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Mkoa wa Arusha, Ephatah Nanyaro, alisema alisema chama chake kiko tayari kujadiliana na yeyote kuhusu amani na mustakabali wa Arusha na kusisitiza kuwa lazima watawala watambue kuwa hawapigi kelele kwa lengo la kufanya mkoa usitawalike kama inavyodaiwa.


  Kwa upande wake, Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Arusha, Semmy Kiondo alisema chama chake kiko tayari wakati wowote kukutana na kujadiliana na mtu, chama au chombo chochote ikiwemo Chadema kutafuta amani na maendeleo ya Arusha lakini akasisitiza hakiko tayari kutishiwa, kunikizwa wala kubezwa kwa namna yoyote.


  Bastola ya Slaa

  Katika hatua nyingine, Jeshi la polisi mkoani Arusha limetamka ya kwamba uchunguzi wa silaha mbili za moto walizokamatwa nazo,Dk Slaa pamoja na mfuasi wa chama hicho,Daniel Ongong'o Novemba 8 mwaka huu jijini Arusha bado haujakamilika.


  Akihojiwa juu ya hatma ya uchunguzi wa silaha hizo jana Kaimu Kamanda wa Jeshi hilo, Akili Mpwapwa alisema kuwa upepelezi juu ya uhalali wa umilikaji wa silaha hizo bado haujamilika kwa kuwa uchunguzi huo sio suala la muda mfupi.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. k

  kazuramimba Senior Member

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mkuu nashindwa kukuelewa kuwa wewe ni dume au jike,CDM au Magamba,kwa sababu umekuwa ukileta habari hovyo kabisa.kama masaburi yanawasha siuende kwa mcamerun.Juz ulikuja na habari za kufagilia pandikizi la CCM zitto kabwe leo unakuja na habari ya ki nge se ambayo asilimia kubwa inaonyesha kulaumu CHADEMA wakati Magamba ndio tatizo.kama uwezo wako wakuchambua mambo umeishia hapo ni bora ungebaki na masaburi kuliko kuwa na ubongo usioutumia.
   
 3. Nicksixyo

  Nicksixyo JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 949
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Tunasubiri tuone wakumwitia mwenzake kiti cha mazungumzo.Nipo hapa chini ya mti napunga upepo,Wakichelewa tena tunawasha mwenge fasta hatulazi damu Pipooooz .........!Hadi OMEGA.:embarassed2:
   
 4. Chibidu

  Chibidu JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 387
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hivi J.K huwa anatumia vigezo gani kuchagua hawa wakuu wa mikoa? Huyu Magesa alipokuwa mkuu wa wilaya kule Bagamoyo alifanya cha maana kipi ambacho kimemfanya ampe ukuu wa mkoa? Kumbukumbu yangu inaniambia huyu jamaa hajawahi hata kushika nafasi kwenye UVCCM au serikali ya mtaa. Kama nimesahau naomba mnikumbushe. nilianza naye chuo pale mlimani mpaka tumemaliza miaka mitatu sijawahi kumsikia hata akiomba kuwa class rep. Sasa huu uzoefu wa uongozi ameutoa wapi?. Uongozi wa nchi hii unataka busara zaidi kutumika katika kuiongoza nchi kuliko kutegemea ubabe na jazba. Kitendo cha J.K kumpeleka Mageza Arusha ni sawa na kumwagia petrol kwenye moto ulioanza kuwaka. J.K mwondoe Magesa Arusha, tafuta mtu mwingine mwenye busara akaiokoe nchi. Vinginevyo mkuu wa kaya toa tamko haraka kuiokoa nchi.
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  R U Serious? Kama wewe unataka kujenga chama chako lazima Usikilize Mazuri na Mabaya; kama utapenda kusikiliza Mazuri tu ni bora Ushabikie kwingine... nani anaishi bila kushutumiwa na kujirekebisha?

  Ukitaka kusikia Mazuri tu hapa sio kwako - Ni Udicteta hili Jamvi la Jamii Forum halikufai !!!!

  Wengi Tunajifunza na Makosa ili kujiimarisha ... Tusiwe kama chama tawala - Unafiki Mwingi...
   
 6. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #6
  Nov 13, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kazuramimba,nafikiri jama habari hii kaitoa kwenye gazeti la mwananchi,lakn cha msingi serikali lazima ikubali kukaa chini izungumze na CDM haswa juu ya swala la Umeya wa Arusha ambapo ndio ccm walifanya uhuni wa hali ya juu.
   
Loading...