Serikali, CCM vimebadilika. kwanini wapinzani nao hawabadiliki?

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
Tokea serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani tumeshuhudia mabadiliko makubwa katiki nyanja mbali mbali ikiwemo kuongezeka kwa uwajibikaji wa viongozi na watumishi wa umma, kupigwa vita vya dhati kwa vitendo vya rushwa, ubadhirifu na ufujaji wa Mali za umma, kuanzishwa na kutekelezwa kwa vita ya kiuchumi yenye lengo la kuhakikisha kuwa uporaji wa maliasili zetu bila kutunufaisha kiuchumi kunakomeshwa.

Takribani masuala yote yaliyokuwa yakipigiwa kelele na wapinzani siku za nyuma ikiwemo kushamiri kwa rushwa, ubadhirifu, uporaji wa maliasili zetu n.k vinafanyiwa kazi kwa hatua mbali mbali kuchukuliwa ili kuhakikisha kuwa kero hizo zinatatuliwa.

Cha kushangaza wapinzani wameendelea kulalamika lalamika kama ilivyokuwa mwanzo. badala ya kushiriki katika utatuzi wa matatizo waliyokuwa wakilalamikia siku zilizopita.

Wakati uongozi wa nchi ukichukua hatua kuboresha maadili,utendaji, na uzalishaji wenye tija. Wapinzani hawaonekani kutambua kuwa nchi inapitia katika mabadiliko makubwa ya kifikra kwa lengo la kuhakikisha kuwa maadili mema ndio yatakuwa nguzo kuu ndani ya Utumishi wa umma iwe ni wabunge, madiwani, wenyeviti wa mitaa/vijiji au watumishi wa umma.

Ni mategemeo yangu kuwa kama ambavyo wapinzani waliweza kuongoza mijadala ya matatizo yaliyokuwa yakilibkabili taifa siku za nyuma. Hats sasa badala ya kulalamika lalamika wataendelea kuibua hoja Mpya zinazohitaji kufanyiwa Kazi. Niwashauri waache undumilakuwilu. Mathalani siku za nyuma walikuwa wakidai nfege kununuliwa, Leo zinanunuliwa wanazibeza.

Japo Jerry Muro anachukuliwa kama mropokaji. Lakini ukisikiliza kwa makini kauli zake anakosoa vitendo vya ukosefu wa maadili, ambavyo kwa mwendo wa zama hii havikubaliki. Mathalani alidai mmoja wa kiongozi mwandamizi wa chama fulani aliye Mwenyekiti wa chama husika Na Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni ana mahusiano ya kimapenzi hadi kumzalisha watoto wawili mmoja wa wabunge wa viti maalum wa chama husika

Kama tuhuma hizi ni za kweli basis ndani ya chama husika yapo matatizo makubwa ya kimaadili.

Ikiwa tuhuma hizo ni za kweli maana ta utovu huu wa kimaadili ni:-
a) Kiongozi wa chama alihonga nafasi ya ubunge wa viti maalum kwa hawara yake.
b) Kiongozi wa chama ametumia nafasi yake ya uongozi kumrubuni binti.

Kama tuhuma hizi ni za kweli. Na uongozi mzima wa chama ukakaa kimya. Ni dhahiri kuwa kitendo hiki cha uongozi mzima wa chama kukaa kimya ni kukubali kupoteza legitimacy ya kukemea vitendo vingine vya ukosefu wa maadili. Chama hiki kikiwa ndio kikuu cha upinzani, ni sawa Na site tukubali kuwa hatuna upinzani hapa nchini kutokana Na kupoteza uhalali wa kukosoa kutokana Na wao kukosa maadili
 
tulitumia kiasi gani kwenye kikao na wametulipa kiasi gani
milioni 50 Kila kijiji vip
laptop kwa kila mwalimu
bunge live vip nalo
ajira nazo vip
kupandishwa kwa madaraja na mshahara vipi
hayo ni baadhi tu ya mapungufu ya serekali hii na ndo fimbo ya kuwachapia [HASHTAG]#2020[/HASHTAG]
 
Tokea serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani tumeshuhudia mabadiliko makubwa katiki nyanja mbali mbali ikiwemo kuongezeka kwa uwajibikaji wa viongozi na watumishi wa umma, kupigwa vita vya dhati kwa vitendo vya rushwa, ubadhirifu na ufujaji wa Mali za umma, kuanzishwa Na kutekelezwa kwa vita ya kiuchumi yenye lengo la kuhakikisha kuwa upiraji wa maliasili zetu bila kutunufaisha kiuchumi kunakomeshwa.

Takribani masuala yote yaliyokuwa yakipigiwa kelele na wapinzani siku za nyuma ikiwemo kushamiri kwa rushwa, ubadhirifu

Kwani RUSHWA na UFISADI umepungu??Kwa maana ukiwa kipenzi cha Mkullu ukitoa au kupokea RUSHWA mbona ndiyo unaongezewa CHEO?Au macho yetu
 
Mwambie magufuli abadilike atangaze mali na madeni yake kwanza. Pia asiongee uongo mfno uongo na uzushi wa kupandisha mishahara
 
Umebadilika ww, acheni kujipaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Ccm ikibadilika mjue na shetani kaokoka
 
Those are petty issues
tulitumia kiasi gani kwenye kikao na wametulipa kiasi gani
milioni 50 Kila kijiji vip
laptop kwa kila mwalimu
bunge live vip nalo
ajira nazo vip
kupandishwa kwa madaraja na mshahara vipi
hayo ni baadhi tu ya mapungufu ya serekali hii na ndo fimbo ya kuwachapia [HASHTAG]#2020[/HASHTAG]
Mbona mnajadili mambo madogo madogo sana. Hii inaonyesha jinsi gani mlivyo na fikra finyu. Ukisoma Ilani za uchaguzi za CCM na ukawa kuna mambo muhimu sana yameainishwa na yameshaanza kutekelezwa. Kwanini hamyaongelei hayo? Mnaongelea nyongeza za mishahara ilhali wengi wenu humu either ni jobless au wanafunzi, hiyo mishahara mnaijulia wapi? Yaani mtu na akili zako unapigia kelele nyongeza ya mshahara ya shilingi 8,000. Maana kwa uzoefu wangu wa mishahara ya serikali huwa nyongeza haizidi 30,000. Ajira gani unataka kama hakuna source ya ajira. Serikali inasisitiza ujenzi wa viwanda vidogo na vikubwa ili nyie mburula hapa mpate hizo ajira. Mnataka nini sasa?????. Bunge live linakusaidia nini wewe mzururaji ambaye kutwa nzima unashinda kwenye mtandao kulalamika huna ajira. Tafuta shamba ulime utakuwa umejiajiri mwenyewe. Hebu mjiongeze kidogo acheni kulia lia hovyo
 
CCM HAIJABADILIKA WW STRANGER(maana siwezi kukuita mkuu kutokana na uwongo wako)...
HALAFU USIWE UNAFANANISHA KUBADILIKA NA VITU VYA KIJINGA
 
Tokea serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani tumeshuhudia mabadiliko makubwa katiki nyanja mbali mbali ikiwemo kuongezeka kwa uwajibikaji wa viongozi na watumishi wa umma, kupigwa vita vya dhati kwa vitendo vya rushwa, ubadhirifu na ufujaji wa Mali za umma, kuanzishwa Na kutekelezwa kwa vita ya kiuchumi yenye lengo la kuhakikisha kuwa upiraji wa maliasili zetu bila kutunufaisha kiuchumi kunakomeshwa.

Takribani masuala yote yaliyokuwa yakipigiwa kelele na wapinzani siku za nyuma ikiwemo kushamiri kwa rushwa, ubadhirifu
Mabadiliko ya kijinga?Kumwaga mvinyo safi na mkatia maji taka kwenye chupa? Hovyo kabisa FISIEMU, absolute toilets!
 
Kwani RUSHWA na UFISADI umepungu??Kwa maana ukiwa kipenzi cha Mkullu ukitoa au kupokea RUSHWA mbona ndiyo unaongezewa CHEO?Au macho yetu

Hakuna kitu kinaidhalilisha CDM kama kuutangazia umma kwa nguvu kubwa kuwa viongozi wake waliowaibua na kuwapatia udhamini wa chama ni wala rushwa. Bila ya kujijua mnautangazia umma kuwa chama chenu ni cha wala rushwa
 
Zilipendwa.Tunachojali na kukifanyia kazi ni VITA DHIDI ya RUSHWA hayo mengine ni taarifa baada ya habari.Yamepitwa tunaganga yaliyopo na yajayo period
 
CCM HAIJABADILIKA WW STRANGER(maana siwezi kukuita mkuu kutokana na uwongo wako)...
HALAFU USIWE UNAFANANISHA KUBADILIKA NA VITU VYA KIJINGA

CCM imebadilika kwa kuwafaulishia wapinzani wake mliokuwa mkiwaita mafisadi papa. Wakati CCM inatekeleza ilani yake ninyi mko busy Ufipa kuwapiga deki mafisadi uke ucafu mliowapaka. Kuwafaulishia mliowaita mafisadi papapapa sio mabadiliko hayo?
 
Zilipendwa.Tunachojali na kukifanyia kazi ni VITA DHIDI ya RUSHWA hayo mengine ni taarifa baada ya habari.Yamepitwa tunaganga yaliyopo na yajayo period
Je ni kweli kiongozi wa chama amemzalisha mbunge wa viti maalum? Kama ni kweli kwanini mnamdharau Jerry Muro?
 
Je ni kweli kiongozi wa chama amemzalisha mbunge wa viti maalum? Kama ni kweli kwanini mnamdharau Jerry Muro?

Akishamzalisha inapunguza uchumi wa nchi??Kamuulize Jerry Muro kwanini anadharauliwa,maana kama kudharauliwa lazima kwa binafsi yake kuna upumbavu anaoufanya na hivyo siwezi kuwajibia hao wengine kwanini wanamdharau.

Ila Jibu waweza kulipata kwake Jerry Muro.
 
Akishamzalisha inapunguza uchumi wa nchi??Kamuulize Jerry Muro kwanini anadharauliwa,maana kama kudharauliwa lazima kwa binafsi yake kuna upumbavu anaoufanya na hivyo siwezi kuwajibia hao wengine kwanini wanamdharau.

Ila Jibu waweza kulipata kwake Jerry Muro.[/QUOTE

Kama tuhuma hizo ni za kweli, hapo Hanna chama msubiri kipindi cha 2015-2020 kiishe ndio mtavuna mnachopanda. Aidha kitendo cha madiwani khongeka fedha xa kipuuzi ni ishara kuwa wagombea walikuwa wanaokotwa hovyo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom