Serikali, CCM vimebadilika. kwanini wapinzani nao hawabadiliki?

Wabadilike wawe wanaisapoti serikali na ccm au?
Wasibadilike kusapoti sisiem. Mantiki ya mtoa mada ni kuwa, yale waliyoyakemea mwanzo kama ni kero kisha yakafanyiwa kazi, basi wasiendelee nayo tena, bali wajikite kuibua mambo mapya ya kihujuma yafanywayo na watawala, ambayo hayajachosha masikio ya watu.
Halafu uthamani wa upinzani unazidi kuporomoka kutokana na viongozi kushindwa kubuni mambo yanakayokwenda na wakati yanayolenga kutatua kero za raia.
 
Kasome mabandiko ya Allen Kilewela na Paul Alex yanaweza kukusaidia kutibu ugonjwa wako.
 

Ukifikiria kama hao madiwani wanahongeka hovyo basi huko ndani ya CCM kuanzia White house mpaka Black house wote ni wahongeka hovyo,huwezi kukubali kuhongwa na muwekezaji wa kabila lolote kama ukiwa MZALENDO na unalipenda TAIFA lako.

Hivyo tabia huzaa sheria,kwa CCM kuhongwa na kuhonga ni CHANDA na PETE,ukisha zoea kuhonga utahonga tu,hata hao waliohongeka havyo hatujui waliambiwa nini nje ya hizo 2m.

Hivyo kwangu mimi hakuna Shetani mwema,shetani ni shetani tu.

Jeery Muro hana tofauti na hao waliohongeka ,tofauti yake leo sababu yuko CCM ndiyo tunaiona tofauti,lakini hana tofauti ya jana wala leo na hata kesho.Mchafu ni mchafu tu hata aoge ni mchafu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom