Serikali CCM = Sawa na mtoto kumwibia baba yake kwa nguvu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali CCM = Sawa na mtoto kumwibia baba yake kwa nguvu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shiefl, Sep 21, 2012.

 1. S

  Shiefl Senior Member

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanabodi mtakumbuka mjadala wa miaka ya kuingiza magari bila kodi ya uchakavu. Serikali ya ccm ilikurupuka kutekeleza sheria ya miaka nane bila Bunge kupitishia bajeti ya wizara ya fedha. Baadaye waziri alipobanwa kwa kuambiwa yale yote na wabunge wenyewe wa CCM akanywea. Baadaye alirudisha miaka. Lakini tangu siku zile watu wengi waliokuwa wamelipishwa ile kodi ya uchakavu wamekuwa wanadai TRA iwarudishie. TRA wakawa wanapiga dana dana eti wanasubiri mwongozo wa waziri. Hivi majuzi wanasema waliokwisha lipa basi tena hawarudishiwi. Sasa mimi ninauliza huu si uwizi wa nguvu? Ni lini serikali yetu itaona kuwa iko kwa ajili ya wananchi na siyo kwa ajili ya kuwanyanyasa? Ninaomba wabunge kwenye jamvi hili jamo hili mlifikishe inapostahili na wale wote waliolazimishwa kulipia kupitia hii kodi kandamizi warudishiwe hela zao maana huu ni ubaguzi. Ama sivyo basi tutaona huu ni ubaguzi wa wazi na utaendelee kuwatafuna viongozi hawa wadhalimu. Tuamke watz, ingekuwa Rwanda siku ya pili bajeti ya wizara ilipopitishwa tungerudishwa hela zetu
   
Loading...