Mallaba
JF-Expert Member
- Jan 30, 2008
- 2,554
- 47
Waacheni tu CCM wazidi kujizika wenyewe, na hapo sijui hata kama watajinusuru na ghadhabu ya wananchi.
Sasa kwa akili timamu eti nchi ina miaka 50 ya uhuru shule zimechoka namna hii kweli?
NYIE CCM nawauliza kweli namna hii? eti wewe JK unayelia lia na kabla dhahma haijakukuteni tuambie mmefanya nini miaka yote hii? Nchi uchumi mbovu, hebu niambieni CCM, mikoa ya kusini gridi ya taifa haijafika miaka 50 ya uhuru kweli? Mikoa ya magharibi gridi ya taifa haijafika kweli nchi hii itaendelea? sasa umeme ndo huo mmewapa mafisadi na Dowans ndo kila kitu kweli uchumi wa nchi hii utaimarika?
Wewe Pinda unajidai muungwana wakati unatetea mafisadi sitaki kukusikia ni chui ktk ngozi ya kondoo. kwa nini tupate shida kwa ajili ya kikundi cha watu wachache hawa?
Please CCM ondokeni kwa amani mmeshindwa kuongoza nchi hii, mnakashfa nyingi sana kuanzia za Loliondo, mpaka leo Dowans, hakuna mwana CCm anaytetea maslahi ya wananchi leo wanatetea mafisadi tuuu